Friday, April 4, 2014

Kaoa wakati naye kaolewa 2

............. inaendelea


Basi maisha yakaendelea yule rafiki yake akawa ananipenda ananijali akija lazima aniletee zawadi, nikanunuliwa zawadi za mtoto mi meno nje.  Lakini mambo yao ni yale yale ya kujifungia chumba cha pili, tena sasa wakawa wanafunga na funguo, mi naona sawa tuu.

Ikafikia nikajifungua mtoto wa kiume wakwe zangu wakanichukua nikapumzike kwao kwa muda kama wa mwezi mmoja baada ya arobaini nikamwambia mume wangu nirudi kwangu akakataa akadai ningoje nyumba yetu iishe ili mtoto wetu afungue nyumba, sikuwa na neno.

Siku moja nikaona bora niende mara moja nikachukue nguo za kubadili maana mwili umerudi katika hali ya kawaida hivyo madira tena yamenichosha, nikaenda mtoto nikamwacha kufika nyumbani nasikia dirishani sauti ya mihemo ya mahaba sauti nzito mmh nikasogea kusikiliza vizuri nasikia ni mume wangu jamani dada nilitamani kuzimia maana nilijua kaingiza mwanamke mwingine ndani.

                                  

nikajishauri niingie kwa mlango wa uani ili nikaufunge nikianza ugomvi huyo mwanamke akose pa kupitia.
Nikaingia ndani kuangalia viatu vyote vya kiume sauti ya mahaba, i love you nyingi analia kama mtoto wee dada dunia ina mambo.




Nikasukuma mlango ulikuwa wazi nikakuta mume wangu kainamishwa analiwa kiboga anakatika huyo nilizubaa kama nimepigwa shoti, yeye hakuniona ila rafiki yake aliniona akanionyesha ishara nitoke nje, niligeuka bila kusema neno nikakaa sebuleni nasikia mume wangu anamwambia rafiki yake ahsante mume wangu, nikazimia.

Kuja zinduka nipo hospitali, ndugu na wakwe zangu wapo hapo, wananiuliza kulikoni machozi yananitoka, akadakia yule rafiki wa mume wangu kuwa nilipoenda nyumbani niliona nyoka nikapiga kelele nikaanguka bahati nzuri walikuwepo wakampiga yule nyoka na kumuua.

Nikatoa macho kama nimeibiwa nauli wakaniuliza ni kweli nikaitika kwa kichwa kukubali machozi yanazidi kunitoka basi baadae nikaruhusiwa mume wangu akanichukua kunirudisha nyumbani kwangu akidai anataka kuwa karibu nami.

Kufika nyumbani mume wangu akaniambia ni kweli yule ni mumewe , kipindi cha nyuma aliwahi kwenda uaya kwa njia za panya sasa kufika huko huyo rafiki alikuwa huko akamsaidia sana mpaka akapata uraia, hadi kufikia kuwa wapenzi wakaoana. 

aliporudi Tanzania baba yake alishasikia kuwa ana mahusiano ya jinsia moja yeye akakataa ndipo wakashauriana na huyo mumewe kuwa aoe ili kutuliza hasira ya wazazi, na ndio maana alihamaki alipoona nimebeba mimba lakini rafiki yake alimpeleka hospital kupimwa akaonekana ana uwezo wa kuzaa.

Sasa ananiomba sana nisimwache atakosa radhi ya wazazi, na pia hawezi kumuacha huyo mumewe kwani ndio anatuweka hapa mjini, ameniandikia nyumba gari mbili na huyo mumewe anafanya mpango wa safari twende wote ulaya maana wanaona hapa ninaweza toa siri.




Nishauri dada nimekonda sana silali kila akija mumewe wakijifungia tu mie machozi yananitoka mwanangu ana miezi sita tu  jamani nifanyeje waungwana mnaosoma humu naomba ushauri wenu.

Jamani anaomba ushauri mi kwangu network loading ...................????????????

Sijawahi kusikia haya Mungu wangu.




1 comment:

  1. pole sana dada yaani sijui hata nikushauri vipi ukisema umwache mtoto utalea na nani na ukisema uwe nae uendelee kuumia ukweli ni mtihani

    ReplyDelete

Toa maoni yako