Tuesday, August 18, 2015

KWANINI SASA HIVI WANAWAKE WENGI WANALEA WATOTO PEKE YAO (single mothers)

Kulea mtoto/watoto na mzazi mmoja ni tatizo kubwa sana katika jamii kama amefariki hiyo haina jinsi lakini kama wote mpo hai kuna athari wanapata watoto kama ya:-
1.  ukosefu wa maadili
2. ukosefu wa mahitaji ya msingi kwa mama asiye kazi ya maana.
3. ukosefu wa ushauri toka kwa baba
4. ukosefu wa maisha bora
tumeona watoto wangapi wapo na maisha magumu sana mpaka wanashindwa kwenda shule sababu mama hana uwezo.
wanakuwa wezi, watovu wa nidhamu na mabinti wanaanza mapenzi wakiwa wadogo sana ukiwauliza hali mbaya ya kiuchumi mama anashindwa kuwahudumia na inabidi akubali kusaidiwa na watoto, amabo kwa umri wao hawakustahili.

NINI KINASABABISHA KUWA SINGLE MOTHER

Nafikiri upande wa uvumilivu umekuwa mdogo kwa pande zote 2 yaani kwa baba na mama wa mtoto/watoto.
zamani bibi/mama zetu walikuwa wanavumilia mengi sana akiwa ananyonyesha basi hata amsikie mumewe ana mchepuko au aujue alikuwa hawezi kusema lolote kwa kuwa analea.
Na walikuwa wakivumilia visa na vituko vingi sana toka kwa waume zao ukimuuliza anasema hawezi kuondoka watoto bado wadogo wacha awalee wakue kwanza.

Na hata katika maisha yao kwa familia niliyotoka mie sijawahi kumsikia mama akihadithia uovu wa baba hata siku moja japo kwa shoga yake au kwa jirani.
Sio kwamba walikuwa hawakosani hapana lakini watoto tulikuwa hatujui saa ngapi wanagombana na saa ngapi wanapatana.

Salute kwa mama yetu katulea na mpaka sasa yupo na baba wana miaka 46 ya ndoa.

Wenza wa sasa hatuna maadili yaani ndoa zimekuwa ili mradi mmewaona viongozi wa dini ikapita dua basi lakini maisha mnayapeleka kama movie ya vichekesho.
Hakuna mwenye amri na mwingine akatekeleza wote mafahari ndani ya zizi moja lazima mmoja atoke.

Mdada ukiachana na mwenza wako  unatamba nitamlea mwanangu na nitamtunza kwa hali yoyote nisimuone kuja mtaka mtoto.  hizo huwa ni hasira na kutokuona mbele au kutothamini ubora wa mtoto.

Pia wadada mnadanganywa kubeba mimba kwanza ndio akuoe ili aonekane kidume basi kama ana uwezo kidogo ndio utajiachia na kumwamini kuliko Mungu aliyekuumba matokeo hakuoi unabaki kulea mtoto na sometimes na matumizi asilete.
unamwaminije mtu mliyekutana meno thelethini na ushee kinywani jamani ningewaona wa maana kama mngefunga hata mkataba kuwa asipokuoa umshitaki hivi hivi unaachia goli anafunga kweli?
ah wadada sometime akili zetu anajua aliyetuumba kwa kweli.
hebu tuvumilie kwa ajili ya watoto ili wakue katika malezi mazuri na bora wakijitegemea wanapunguza mzigo kwa wazazi kuliko wakikosa elimu wakawa na tabia za ajabu kila siku mama polisi kwenda kumtolea mtoto dhamana kashikwa kwa wizi au ukahaba.
turudi kwenye historia ya wazazi wetu ili tuokoe vizazi vyetu.
okay

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako