Thursday, April 3, 2014

kaoa wakati naye kaolewa

Ahsante dada kwa kutupa fursa hii ya kutoa ya moyoni,

Kwanza nampa pole huyo dada akaze moyo Mungu atamsaidia,

Mi yangu makubwa zaidi dada



Mi nina miaka 25, baada ya kumaliza form four, nikapata bahati ya kupata mchumba pande la mwanaume, mzuri, mtanashati yaani dada ukimwona utasema kweli, nami hata sikujivunga nikakubali haraka haraka, kazi alisema ye ni mfanya biashara.

Basi maandalizi yakafanywa binti nikafundwa nikafundika maandalizi ya kwenda kumuhendo mume wangu.
ndoa ikafungwa kwa fahari jamani tulipendeza wenyewe nikikumbuka nalia kama mtoto.

Basi tulienda honeymoon siku ya kwanza tukalal akadai ana presha ya ndoa kesho yake asubuhi ndio tukafanya tendo la ndoa.

wakati tunafanya akawa ananiambia nimpapase kwenye makalio basi nikimshika anasisimkwa na kuniambia kazana nikifanya hivyo yeye ndio anapata speed  mpaka tukamaliza.

Ukweli dada lile jambo lilinishangaza sana mpaka likaninyima raha kwani sikuolewa na bikra hivyo mapenzi nilikuta nishaanza pia hata kwenye mafunzo sikusikia kitu hiki.
Basi ikawa ndio mapenzi yetu kama treni ya kizamani mpaka uchochee kuni ndio liongeze mwendo.

Nikaenda uliza wakubwa nyumbani wakaniambia haina neno ndio mambo ya digital hayo mumeo  kazoea mambo ya kizungu, basi maisha yakaendelea. 

Sasa kitu kingine alikuwa anaaga anasafiri lakini sehemu anayokwenda ukimuagiza kitu cha huko harudi nacho madai yake ye mvivu wa kubeba mizigo, nikitaka out ananitafutia rafiki yake niende naye yeye anadai hapendi mambo ya kutoka toka basi mi natoka narudi namkuta amelala au anaangalia tv.

Baada ya miezi minne nikashika uja uzito heee wacha alete maneno anadai sio wake nimueleze niliko upata, nikamueleza yeye ndie mume wangu sasa aanipe nani mwingine, mwishowe akaniomba nimsamehe alikuwa anataka uhakika kama yake kweli.

Sasa alikuwa na rafiki yake huyo ana pesa sana na hata ikitokea shida nyumbani basi akimpigia hata usiku wa manane anatuma.  Kila mara anakuja nyumbani na huwa wanaingia chumba cha pili na kuniambia nisiingie huko wenyewe wanapanga mambo yao ya biashara.



Siku moja alikuja rafiki yake huyo wakaingia chumbani kama kawaida mume wangu akasahau simu ikaita 
nikampelekea ile nafungua mlango nikakuta wamekubatiana nikatoka mbio mume wangu akanifuata na kuniambia walikuwa wanapongezana wamepata mafanikio kwenye biashara, baadae rafiki naye akatoka akanipa dollar 1000 akanikumbatia na kuniambia nina kismeti cha biashara sana wamepata mafanikio sana tangu nilivyo olewa nikachekelea mwenyewe kumbe dada wewe mmh

itaendelea......................


No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako