Monday, March 10, 2014

Baadhi ya Wanaume ni kuku wa kienyeji

Kwa maoni ya wasomaji wangu wapendwa wameomba niirudie post hii sijui kwa nini

Hebu tuangalie hawa wanaume wa tabia hii.


Mwanaume umeoa mke na labda mmeshapata watoto kisha kunakuwa na house girl au shemeji.

Mkeo ni hodari mashaallah anakufanyia mambo yote muhimu, kitandani ndio usiseme kafundwa akafundika anakupa mapenzi mazito mpaka unaomba pooo.



Tena basi hana hiyana muda wowote ukitaka penzi anakupa bila wasi wasi.

kwa kawaida hasa kwa ma house girl wengi huwa washamba hawajajua mambo ya kujipendezesha kama mtoto wa kike atakiwavyo.   Tena sometime walikotoka hata mambo ya kuoga vizuri hajui labda maji yalikuwa mail kadhaa.  Tena wengine wanakuwa na umri mdogo sana.





Ndio we na mkeo mnaanza kazi ya kumuelekeza usafi na kazi za ndani, dukani wapi, sokoni n.k
Binti huyu anakuwa na adabu sana tena kwenye zile mila za kupiga  magoti ndio kabisa hata kukusogelea wewe baba ndani ya nyumba ni kazi.

Ukirudi kazini ukikaa sebuleni yeye yulee chumbani au jikoni hathubutu kabisa kukaa pale ulipo.

Kinachonishangaza we baba mtu mzima na akili zako timamu usiku unamwacha mkeo chumbani kwenu kwenye kitanda kizuri mashuka safi huenda mkeo ni maridadi amekinyunyizia marashi unaenda kwa kile kitoto.




Jamani unaenda tafuta mapenzi gani anayoyajua yule mtoto au ni uharibifu hufikirii kama ni mwanao angefanyiwa vile ungejisikiaje. Tena unamjaza mimba na unakuwa wa kwanza kunfukuza nyumbani, aende wapi na ujauzito ule aulee nani, alikotoka huenda walikuwa wanamtegemea akipata kamshahara awatumie na wao.  Sio ndio kutengeneza machangu na watoto wa mtaani.

Tafadhalini jamani hasa nyie wenye pesa zenu wengine utamuona sehemu ya starehe ana katoto kadogo kama mjukuu wake anakapa denda uuh huwa natamani kufa Mungu anistirie wanangu jamani nikikukuta naye nakulamba risasi.

Mtoto wa mwenzio ni wako jamani tuwahurumie maisha ya dhiki yanawatosha kuwa adhabu kwao.






Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako