UZURI WA MWANAMKE

Mwanamke kwa kawaida ana sura tatu (3).
(i) Sura ya nje (Reception)
(ii) Sura ya pili ya mwanamke mazingira ( tabia ,usafi wa nyumba nk)
(iii) Sura ya tatu ya mwanamke ni mfumo mzima wa uzazi mf uke na maeneo nyeti nk
Hii ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya
mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi muda wote. Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na
ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo. Hii huchangia matatizo makubwa kiafya ukianza na magonjwa kama UTI , muwasho, fangasi na matatizo mbalimbali yanayoenda mpaka kwenye kizazi na kusababisha matatizo makubwa baadae kama ugumba na kansa
Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa
kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako
kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama.
Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani
VIHATARISHI VYA AFYA YA SEHEMU NYETI NA
UZAZI KWA UJUMLA
(i) Kuchangia nguo za ndani na vifaa vya kuogea, hii huwapata sana wanafunzi
(ii) Vyoo vya kuchangia (public toilets)
maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk.
(iii) Kutotumia maji safi na salama.
utakuta kuna ndoo ya maji chooni imeweka
ukungu hujui maji yana muda gani usitumie
kwani maji haya hukaa bakteria hatari
(iv) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio
salama.
wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri.
(v) Bakteria
Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani.
Mfano unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kuanika juani au kupiga pasi kabla ya kuvaa.
(vi) kutokufanya usafi ipasavyo kwa maeneo nyeti
mwanamke ana miswaki 2 wa mdomoni na wa kikeni sukutua utoe siagi inayoganda kwa bibi ili kukuacha msafi na kuondoa harufu mbaya.
sasa we dada unaefuga/kuunga kucha kidole cha kati hutaweza jisafisha vizuri na kama utaweza ina maana utajijeruhi kwa bibi na kusababisha vidonda kwani ngozi yake ni nyepesi sana.
kumbuka unapokuwa na mpasuko wowote husababisha kupata m
aambukizi haraka sana.
Lakini pia jinsi ya kujisafisha unapopata choo kikubwa usithubutu kujisafisha kwa kutoa mkono nyuma kuleta kwa bibi kwani kinyesi kina bacteria hatari ambao watashambulia kwa bibi.