Friday, September 11, 2015

UZURI WA MWANAMKE


UZURI WA MWANAMKE
















Mwanamke kwa kawaida ana sura tatu (3).


 (i) Sura ya nje (Reception)


(ii) Sura ya pili ya mwanamke mazingira ( tabia ,usafi wa nyumba nk)


(iii) Sura ya tatu ya mwanamke ni mfumo mzima wa uzazi mf uke na maeneo nyeti nk


Hii ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya
mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi muda wote. Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na
ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo. Hii huchangia matatizo makubwa kiafya ukianza na magonjwa kama UTI , muwasho, fangasi na matatizo mbalimbali yanayoenda mpaka kwenye kizazi na kusababisha matatizo makubwa baadae kama ugumba na kansa

Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa
kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako
kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama.


Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani 


VIHATARISHI VYA AFYA YA SEHEMU NYETI NA


 UZAZI KWA UJUMLA


(i) Kuchangia nguo za ndani na vifaa vya kuogea, hii huwapata sana wanafunzi


(ii) Vyoo vya kuchangia (public toilets)


maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk.


(iii) Kutotumia maji safi na salama.


utakuta kuna ndoo ya maji chooni imeweka


 ukungu hujui maji yana muda gani usitumie 


kwani  maji haya hukaa bakteria hatari



 (iv) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio


salama.


wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri.


(v) Bakteria
Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani.


Mfano unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kuanika juani au kupiga pasi kabla ya kuvaa.


 (vi) kutokufanya usafi ipasavyo kwa maeneo nyeti

   
  mwanamke ana miswaki 2 wa mdomoni na wa kikeni sukutua utoe siagi inayoganda kwa bibi ili kukuacha msafi  na kuondoa harufu mbaya.
sasa we dada unaefuga/kuunga kucha kidole cha kati hutaweza jisafisha vizuri na kama utaweza ina maana utajijeruhi kwa bibi na kusababisha vidonda kwani ngozi yake ni nyepesi sana. 
kumbuka unapokuwa na mpasuko wowote husababisha kupata m
aambukizi haraka sana.

Lakini pia jinsi ya kujisafisha unapopata choo kikubwa usithubutu kujisafisha kwa kutoa mkono nyuma kuleta kwa bibi kwani kinyesi kina bacteria hatari ambao watashambulia kwa bibi.


(vii) kufanya tendo la ndoa lisilo salama


CHUKUA TAHADHARI MAPEMA , KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

Tuesday, August 18, 2015

KWANINI SASA HIVI WANAWAKE WENGI WANALEA WATOTO PEKE YAO (single mothers)

Kulea mtoto/watoto na mzazi mmoja ni tatizo kubwa sana katika jamii kama amefariki hiyo haina jinsi lakini kama wote mpo hai kuna athari wanapata watoto kama ya:-
1.  ukosefu wa maadili
2. ukosefu wa mahitaji ya msingi kwa mama asiye kazi ya maana.
3. ukosefu wa ushauri toka kwa baba
4. ukosefu wa maisha bora
tumeona watoto wangapi wapo na maisha magumu sana mpaka wanashindwa kwenda shule sababu mama hana uwezo.
wanakuwa wezi, watovu wa nidhamu na mabinti wanaanza mapenzi wakiwa wadogo sana ukiwauliza hali mbaya ya kiuchumi mama anashindwa kuwahudumia na inabidi akubali kusaidiwa na watoto, amabo kwa umri wao hawakustahili.

NINI KINASABABISHA KUWA SINGLE MOTHER

Nafikiri upande wa uvumilivu umekuwa mdogo kwa pande zote 2 yaani kwa baba na mama wa mtoto/watoto.
zamani bibi/mama zetu walikuwa wanavumilia mengi sana akiwa ananyonyesha basi hata amsikie mumewe ana mchepuko au aujue alikuwa hawezi kusema lolote kwa kuwa analea.
Na walikuwa wakivumilia visa na vituko vingi sana toka kwa waume zao ukimuuliza anasema hawezi kuondoka watoto bado wadogo wacha awalee wakue kwanza.

Na hata katika maisha yao kwa familia niliyotoka mie sijawahi kumsikia mama akihadithia uovu wa baba hata siku moja japo kwa shoga yake au kwa jirani.
Sio kwamba walikuwa hawakosani hapana lakini watoto tulikuwa hatujui saa ngapi wanagombana na saa ngapi wanapatana.

Salute kwa mama yetu katulea na mpaka sasa yupo na baba wana miaka 46 ya ndoa.

Wenza wa sasa hatuna maadili yaani ndoa zimekuwa ili mradi mmewaona viongozi wa dini ikapita dua basi lakini maisha mnayapeleka kama movie ya vichekesho.
Hakuna mwenye amri na mwingine akatekeleza wote mafahari ndani ya zizi moja lazima mmoja atoke.

Mdada ukiachana na mwenza wako  unatamba nitamlea mwanangu na nitamtunza kwa hali yoyote nisimuone kuja mtaka mtoto.  hizo huwa ni hasira na kutokuona mbele au kutothamini ubora wa mtoto.

Pia wadada mnadanganywa kubeba mimba kwanza ndio akuoe ili aonekane kidume basi kama ana uwezo kidogo ndio utajiachia na kumwamini kuliko Mungu aliyekuumba matokeo hakuoi unabaki kulea mtoto na sometimes na matumizi asilete.
unamwaminije mtu mliyekutana meno thelethini na ushee kinywani jamani ningewaona wa maana kama mngefunga hata mkataba kuwa asipokuoa umshitaki hivi hivi unaachia goli anafunga kweli?
ah wadada sometime akili zetu anajua aliyetuumba kwa kweli.
hebu tuvumilie kwa ajili ya watoto ili wakue katika malezi mazuri na bora wakijitegemea wanapunguza mzigo kwa wazazi kuliko wakikosa elimu wakawa na tabia za ajabu kila siku mama polisi kwenda kumtolea mtoto dhamana kashikwa kwa wizi au ukahaba.
turudi kwenye historia ya wazazi wetu ili tuokoe vizazi vyetu.
okay
am back baada ya kupata email, na sms nyiingi za kurudisha hii blog hatimaye nimekubaliana nanyi sasa mtaendelea kupata mada za mahusiano kama kawa.

kwa wale wapya karibuni sana humu ni mada za kujenga ndoa zenu itifaki inazingatiwa mtaelimik, mtaburudika  na mtafurahi yaah i promise that.
kwa mwenye maswali, maoni au ushauri kuhusu mahusiano naomba aulize kwa email, notification au sms.
kama litahusu jamii nitalijibu humu laa masuala ya binafsi nitamjibu private.
tupo katika kuelimishana na kukumbushana pale penye mapungufu
enjoy it
Johari Orig back again to you

Monday, May 5, 2014

MAPENZI IMARA HULETWA NA MWANAUME

Ndio kwa kila kona mwanaume anahusika sana kwanini



  • Mwanaume ndie anatongoza na ndie mwenye kuchagua yupi anamfaa kuishi naye Mwanamke hata umpende namna gani huwezi kumlazimisha uishi naye.
  • Mwanaume ndie mtunzaji wa familia kwa asilimia nyingi hata mwanamke akiwa na kipato bado mwanaume ndie anajulikana ndani kuwa msimamizi na mtekelezaji wa mipango yote.
  • Mwanaume ndie anaruhusiwa kumdhibiti mwanamke kama kumpa ruhusa na kumpangia muda wa kurudi, kumruhusu kufanya kazi, biashara, hata kusafiri ki matembezi.
  • mwanaume ndie mwenye wajibu wa kutaka kitu na kukataa mfano marafiki wa mke, chakula, mavazi mkewe avaeje n.k
  • Mwanaume akiwa hataki chakula cha usiku huwezi mlazimisha hata ufanyeje kwani maumbile yake hayawezi fanya kazi mpaka mwenyewe apende, kinyume na mwanamke hata kama hutaki mwanaume atajisevia tuu.  Pia ndie mpangaji wa magoli kama mawili au matatu au kamoja huwezi mlazimisha aendelee.
  • Mwanaume ana ushawishi mkubwa sana kumridhisha mwanamke na hata kama anamuongopea mwanamke si rahisi kujua kwa wakati huo.
  • Mwanaume akiamua kutulia na mkewe hata atokee jini hataweza kumbadili.
Sasa wewe mwanaume una mke mzuri wa sura na tabia mpaka marafiki zako wanakuonea wivu, michepuko ya nini?
Ndani unakuwa kama shetani unacheka asubuhi mchana ushanuna, salaam kwa mkeo ya nadra unatoka kazini ukifika nyumbani huna tabasamu, huna salaam ya bashasha kwa mpenzi mkeo.

kama mmepata watoto ndio linageuka jina lake mama sikujua, au mama kidole hee huoni haya ulipokuwa unamfukuzia ulikuwa unamwita nani? ile sweetie, my love. honey baby imeishia wapi?

Kama hamna mtoto ndio unamkata jina hata mbele za watu wee Johari, Jane, Maimuna n.k kama mtoto mdogo heshima na thamani yake iko wapi ukimwita mke wangu utapungukiwa nini?

Humtimizii mkeo mahitaji, humrembi ukafurahia urembo wake  huna habari na bajeti ya vipodozi ni bora ukahonge mchepuko laki mbili akasuke wakati mkeo hata elf kumi ya kusukia  inakushinda kumpa.

Mchepuko unautoa out kwenye hotel nzuri mnamaliza laki kadhaa mkeo nyumbani dagaa na mchicha havina mwanzo wala mwisho wa mwezi, na hizo hotel hujawahi mpeleka tangu umemuoa.

Kurudi kwako usiku wa manane kila siku foleni za Dar nzima zinakukuta wewe tuu, siku akikuona mapema ujue huna hela.




Hata siku ya weekend ambapo ni muda mzuri wa kukaa na mpenzi mkeo naye akadeka kidogo kwa mumewe ndio kwanza utapanga safari zisizo kuwa na msingi akikuuliza unamwambia wacha ukatafute hela atakula nini.  heee alifuata kula kwako?  Jiangalizieni 

Na siku utakayojaaliwa kuwa nyumbani ni mazogo yasio na sababu ili mradi karaha mtindo mmoja mpaka mkeo anaomba Mungu upigiwe simu uondoke looh.

Siku utakayoamua kumpa mapenzi ndio kabisaaa maana huna rai unamkamata mwanamke kama unagombana nae kumtomasa kama unakanda ngano akitoka hapo hoi hana kiungo  kisicho  maumivu.

Ulimuolea nini?  Ukahangaika kumtongoza, ukachukua namba za simu ukapanga mipango ikapangika ulimaliza soli za viatu ukampa ahadi zingine hazitekelezeki,  mpaka ukamtoa kwao kwa vigele gele hiyo michepuko yako ilikuwa wapi?

Kila siku kumtoa hila mkeo kama wewe umekamilika vile kosa dogo kwako kubwa siku hiyo utasema usiku kucha mkeo halali masikini anaishia kulia tuu kaomba msamaha huelewi ndio kwanza kakutia funguo ya kashfa, matusi ya reja reja.


Ukweli wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa si kwa mapenzi bali labda kwa ajili ya watoto, mali wamechuma wote sasa anaona akiondoka ataenda kuanzaje maisha, wengine mashinikizo ya wazazi, wengine wanaionea aibu jamii kuwa wataonekana wameshindwa ndoa zao.


Mwanamke akitoka kwako anawachukia wanaume  dunia nzima na kulipiza kisasi  kwa sababu yako.

Mwanaume jitahidi kumpenda mkeo.



Wednesday, April 23, 2014

FAIDA YA TENDO LA NDOA KI AFYA





Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili.
Wataalamu wanasema kwamba unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.


  • Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.  Kuongeza mwendo wa damu.
  • Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili. hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji
  • Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
  • Hupunguza maumivu wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu  ya viungo [arthritis]  maumivu ya shingo [Whiplash]  na maumivu ya kichwa
  • Ulinzi wa tezi ya kibofu [mwanaume] Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu [prostate] yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini.
  • Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa maji maji hayo yenye madhara.
  • Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.
  • Hupunguza mfadhaiko wa moyo.
  • Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini.
  • Wale wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
  • Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume [testosterone] na za kike [Oestogen]
  • Faida nyingine inayopatikana kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.
  • Hata hivyo baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.
  • Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima.  Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.  Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali  yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo [Cardiovascular].
  • Hupunguza baridi na mafua
  • Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
Jambo la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi katika njia sahihi tena usioukuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa.  Ina maana kwa wenye ndoa zao tuu.

Friday, April 4, 2014

Kaoa wakati naye kaolewa 2

............. inaendelea


Basi maisha yakaendelea yule rafiki yake akawa ananipenda ananijali akija lazima aniletee zawadi, nikanunuliwa zawadi za mtoto mi meno nje.  Lakini mambo yao ni yale yale ya kujifungia chumba cha pili, tena sasa wakawa wanafunga na funguo, mi naona sawa tuu.

Ikafikia nikajifungua mtoto wa kiume wakwe zangu wakanichukua nikapumzike kwao kwa muda kama wa mwezi mmoja baada ya arobaini nikamwambia mume wangu nirudi kwangu akakataa akadai ningoje nyumba yetu iishe ili mtoto wetu afungue nyumba, sikuwa na neno.

Siku moja nikaona bora niende mara moja nikachukue nguo za kubadili maana mwili umerudi katika hali ya kawaida hivyo madira tena yamenichosha, nikaenda mtoto nikamwacha kufika nyumbani nasikia dirishani sauti ya mihemo ya mahaba sauti nzito mmh nikasogea kusikiliza vizuri nasikia ni mume wangu jamani dada nilitamani kuzimia maana nilijua kaingiza mwanamke mwingine ndani.

                                  

nikajishauri niingie kwa mlango wa uani ili nikaufunge nikianza ugomvi huyo mwanamke akose pa kupitia.
Nikaingia ndani kuangalia viatu vyote vya kiume sauti ya mahaba, i love you nyingi analia kama mtoto wee dada dunia ina mambo.




Nikasukuma mlango ulikuwa wazi nikakuta mume wangu kainamishwa analiwa kiboga anakatika huyo nilizubaa kama nimepigwa shoti, yeye hakuniona ila rafiki yake aliniona akanionyesha ishara nitoke nje, niligeuka bila kusema neno nikakaa sebuleni nasikia mume wangu anamwambia rafiki yake ahsante mume wangu, nikazimia.

Kuja zinduka nipo hospitali, ndugu na wakwe zangu wapo hapo, wananiuliza kulikoni machozi yananitoka, akadakia yule rafiki wa mume wangu kuwa nilipoenda nyumbani niliona nyoka nikapiga kelele nikaanguka bahati nzuri walikuwepo wakampiga yule nyoka na kumuua.

Nikatoa macho kama nimeibiwa nauli wakaniuliza ni kweli nikaitika kwa kichwa kukubali machozi yanazidi kunitoka basi baadae nikaruhusiwa mume wangu akanichukua kunirudisha nyumbani kwangu akidai anataka kuwa karibu nami.

Kufika nyumbani mume wangu akaniambia ni kweli yule ni mumewe , kipindi cha nyuma aliwahi kwenda uaya kwa njia za panya sasa kufika huko huyo rafiki alikuwa huko akamsaidia sana mpaka akapata uraia, hadi kufikia kuwa wapenzi wakaoana. 

aliporudi Tanzania baba yake alishasikia kuwa ana mahusiano ya jinsia moja yeye akakataa ndipo wakashauriana na huyo mumewe kuwa aoe ili kutuliza hasira ya wazazi, na ndio maana alihamaki alipoona nimebeba mimba lakini rafiki yake alimpeleka hospital kupimwa akaonekana ana uwezo wa kuzaa.

Sasa ananiomba sana nisimwache atakosa radhi ya wazazi, na pia hawezi kumuacha huyo mumewe kwani ndio anatuweka hapa mjini, ameniandikia nyumba gari mbili na huyo mumewe anafanya mpango wa safari twende wote ulaya maana wanaona hapa ninaweza toa siri.




Nishauri dada nimekonda sana silali kila akija mumewe wakijifungia tu mie machozi yananitoka mwanangu ana miezi sita tu  jamani nifanyeje waungwana mnaosoma humu naomba ushauri wenu.

Jamani anaomba ushauri mi kwangu network loading ...................????????????

Sijawahi kusikia haya Mungu wangu.




Thursday, April 3, 2014

kaoa wakati naye kaolewa

Ahsante dada kwa kutupa fursa hii ya kutoa ya moyoni,

Kwanza nampa pole huyo dada akaze moyo Mungu atamsaidia,

Mi yangu makubwa zaidi dada



Mi nina miaka 25, baada ya kumaliza form four, nikapata bahati ya kupata mchumba pande la mwanaume, mzuri, mtanashati yaani dada ukimwona utasema kweli, nami hata sikujivunga nikakubali haraka haraka, kazi alisema ye ni mfanya biashara.

Basi maandalizi yakafanywa binti nikafundwa nikafundika maandalizi ya kwenda kumuhendo mume wangu.
ndoa ikafungwa kwa fahari jamani tulipendeza wenyewe nikikumbuka nalia kama mtoto.

Basi tulienda honeymoon siku ya kwanza tukalal akadai ana presha ya ndoa kesho yake asubuhi ndio tukafanya tendo la ndoa.

wakati tunafanya akawa ananiambia nimpapase kwenye makalio basi nikimshika anasisimkwa na kuniambia kazana nikifanya hivyo yeye ndio anapata speed  mpaka tukamaliza.

Ukweli dada lile jambo lilinishangaza sana mpaka likaninyima raha kwani sikuolewa na bikra hivyo mapenzi nilikuta nishaanza pia hata kwenye mafunzo sikusikia kitu hiki.
Basi ikawa ndio mapenzi yetu kama treni ya kizamani mpaka uchochee kuni ndio liongeze mwendo.

Nikaenda uliza wakubwa nyumbani wakaniambia haina neno ndio mambo ya digital hayo mumeo  kazoea mambo ya kizungu, basi maisha yakaendelea. 

Sasa kitu kingine alikuwa anaaga anasafiri lakini sehemu anayokwenda ukimuagiza kitu cha huko harudi nacho madai yake ye mvivu wa kubeba mizigo, nikitaka out ananitafutia rafiki yake niende naye yeye anadai hapendi mambo ya kutoka toka basi mi natoka narudi namkuta amelala au anaangalia tv.

Baada ya miezi minne nikashika uja uzito heee wacha alete maneno anadai sio wake nimueleze niliko upata, nikamueleza yeye ndie mume wangu sasa aanipe nani mwingine, mwishowe akaniomba nimsamehe alikuwa anataka uhakika kama yake kweli.

Sasa alikuwa na rafiki yake huyo ana pesa sana na hata ikitokea shida nyumbani basi akimpigia hata usiku wa manane anatuma.  Kila mara anakuja nyumbani na huwa wanaingia chumba cha pili na kuniambia nisiingie huko wenyewe wanapanga mambo yao ya biashara.



Siku moja alikuja rafiki yake huyo wakaingia chumbani kama kawaida mume wangu akasahau simu ikaita 
nikampelekea ile nafungua mlango nikakuta wamekubatiana nikatoka mbio mume wangu akanifuata na kuniambia walikuwa wanapongezana wamepata mafanikio kwenye biashara, baadae rafiki naye akatoka akanipa dollar 1000 akanikumbatia na kuniambia nina kismeti cha biashara sana wamepata mafanikio sana tangu nilivyo olewa nikachekelea mwenyewe kumbe dada wewe mmh

itaendelea......................