Monday, May 5, 2014

MAPENZI IMARA HULETWA NA MWANAUME

Ndio kwa kila kona mwanaume anahusika sana kwanini



  • Mwanaume ndie anatongoza na ndie mwenye kuchagua yupi anamfaa kuishi naye Mwanamke hata umpende namna gani huwezi kumlazimisha uishi naye.
  • Mwanaume ndie mtunzaji wa familia kwa asilimia nyingi hata mwanamke akiwa na kipato bado mwanaume ndie anajulikana ndani kuwa msimamizi na mtekelezaji wa mipango yote.
  • Mwanaume ndie anaruhusiwa kumdhibiti mwanamke kama kumpa ruhusa na kumpangia muda wa kurudi, kumruhusu kufanya kazi, biashara, hata kusafiri ki matembezi.
  • mwanaume ndie mwenye wajibu wa kutaka kitu na kukataa mfano marafiki wa mke, chakula, mavazi mkewe avaeje n.k
  • Mwanaume akiwa hataki chakula cha usiku huwezi mlazimisha hata ufanyeje kwani maumbile yake hayawezi fanya kazi mpaka mwenyewe apende, kinyume na mwanamke hata kama hutaki mwanaume atajisevia tuu.  Pia ndie mpangaji wa magoli kama mawili au matatu au kamoja huwezi mlazimisha aendelee.
  • Mwanaume ana ushawishi mkubwa sana kumridhisha mwanamke na hata kama anamuongopea mwanamke si rahisi kujua kwa wakati huo.
  • Mwanaume akiamua kutulia na mkewe hata atokee jini hataweza kumbadili.
Sasa wewe mwanaume una mke mzuri wa sura na tabia mpaka marafiki zako wanakuonea wivu, michepuko ya nini?
Ndani unakuwa kama shetani unacheka asubuhi mchana ushanuna, salaam kwa mkeo ya nadra unatoka kazini ukifika nyumbani huna tabasamu, huna salaam ya bashasha kwa mpenzi mkeo.

kama mmepata watoto ndio linageuka jina lake mama sikujua, au mama kidole hee huoni haya ulipokuwa unamfukuzia ulikuwa unamwita nani? ile sweetie, my love. honey baby imeishia wapi?

Kama hamna mtoto ndio unamkata jina hata mbele za watu wee Johari, Jane, Maimuna n.k kama mtoto mdogo heshima na thamani yake iko wapi ukimwita mke wangu utapungukiwa nini?

Humtimizii mkeo mahitaji, humrembi ukafurahia urembo wake  huna habari na bajeti ya vipodozi ni bora ukahonge mchepuko laki mbili akasuke wakati mkeo hata elf kumi ya kusukia  inakushinda kumpa.

Mchepuko unautoa out kwenye hotel nzuri mnamaliza laki kadhaa mkeo nyumbani dagaa na mchicha havina mwanzo wala mwisho wa mwezi, na hizo hotel hujawahi mpeleka tangu umemuoa.

Kurudi kwako usiku wa manane kila siku foleni za Dar nzima zinakukuta wewe tuu, siku akikuona mapema ujue huna hela.




Hata siku ya weekend ambapo ni muda mzuri wa kukaa na mpenzi mkeo naye akadeka kidogo kwa mumewe ndio kwanza utapanga safari zisizo kuwa na msingi akikuuliza unamwambia wacha ukatafute hela atakula nini.  heee alifuata kula kwako?  Jiangalizieni 

Na siku utakayojaaliwa kuwa nyumbani ni mazogo yasio na sababu ili mradi karaha mtindo mmoja mpaka mkeo anaomba Mungu upigiwe simu uondoke looh.

Siku utakayoamua kumpa mapenzi ndio kabisaaa maana huna rai unamkamata mwanamke kama unagombana nae kumtomasa kama unakanda ngano akitoka hapo hoi hana kiungo  kisicho  maumivu.

Ulimuolea nini?  Ukahangaika kumtongoza, ukachukua namba za simu ukapanga mipango ikapangika ulimaliza soli za viatu ukampa ahadi zingine hazitekelezeki,  mpaka ukamtoa kwao kwa vigele gele hiyo michepuko yako ilikuwa wapi?

Kila siku kumtoa hila mkeo kama wewe umekamilika vile kosa dogo kwako kubwa siku hiyo utasema usiku kucha mkeo halali masikini anaishia kulia tuu kaomba msamaha huelewi ndio kwanza kakutia funguo ya kashfa, matusi ya reja reja.


Ukweli wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa si kwa mapenzi bali labda kwa ajili ya watoto, mali wamechuma wote sasa anaona akiondoka ataenda kuanzaje maisha, wengine mashinikizo ya wazazi, wengine wanaionea aibu jamii kuwa wataonekana wameshindwa ndoa zao.


Mwanamke akitoka kwako anawachukia wanaume  dunia nzima na kulipiza kisasi  kwa sababu yako.

Mwanaume jitahidi kumpenda mkeo.



No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako