Tuesday, December 31, 2013
TALK ABOUT LOVE - Madhara ya mapenzi
Natumaini mmeamka salama na leo tunakutana tena hapa, mi pia sijambo, kwa wale wanaoumwa basi nawaombea kwa Mungu wapone haraka na kuendelea na harakati za kila siku.
MADHARA YA MAPENZI
Ni makubwa sana yanayumbisha dunia inasababisha watu kuwa wakatili kama wanyama, heshima na utu unatoweka, mtu anadhalilika mbele ya jamii, familia inasambaratika na kupelekea watoto kukosa huduma bora kama kusoma, mahitaji muhimu, na hatimaye kupatikana watoto wa mitaani.
Chanzo chake ni nini
- Kuvunja uaminifu mmoja wenu
- Kuishi kwa mazoea
- Thamani ya mapenzi kupungua
- Migogoro isiyokwisha.
KUVUNJA UAMINIFU
Inapotokea mmoja wenu akavunja uaminifu ina maana akawa na mpenzi mwingine wakati mko pamoja basi ujue ndani mabadiliko yataonekana kwa sababu moyo ni mmoja hauwezi kupenda watu wawili na ukawa sawa. Hivyo hupelekea mwenza kuona hajaliwi, habembelezwi kama zamani, kauli zinakuwa za mkato, heshima inapungua, inafikia kujibizana mbele za watu kama maadui fulani.
KUISHI KWA MAZOEA
Ni kwa wapenzi ambao mwanzo walikuwa wanajishughulisha sana kwa wapenzi wao mfano kwa mwanaume:-
Mwanzo wa mapenzi
anakuwa simu kila mara,
majina ya mapenzi yote utaitwa mara baby,honey,sweetheart,na mengine mengi ya mapenzi,
zawadi mbali mbali,
shopping za haja,
anawahi kurudi nyumbani na siku za mapumziko hatoki labda kwa dharura,
muda wote anapenda akuone na kila unachovaa lazima akusifie,
huomba msamaha pindi anapokosea n.k.
kwa mwanamke:-
anakuwa msafi muda wote,
hufanya vitu vinavyompendeza mumewe kama kupika chakula n.k.
hatoki nyumbani bila ruhusa ya mumewe na akitoka hurudi haraka ili asimuudhi mumewe,
hujipamba kadiri anavyoweza ili amvutie mumewe
huongea sauti laini na taamu tena ya chini ili ampendeze mumewe
anahakikisha mpenziwe anamuogesha na kumtayarishia nguo, viatu n.k
akikosa huomba radhi kwa magoti huku akibembeleza na kulia ili asamehewe na kuahidi kutorudia tena.
Baada ya muda mfupi wa maisha haya ya pamoja.
haya yote mazuri hutoweka hasa kwa wanawake kama alifanya haya alikuwa hajaolewa,
akishaolewa tu baaasi hugeuka na kuwa hivi:-
- chakula cha usiku - yaani tendo la ndoa inakuwa mpaka mwanaume alazimishe na siku zingine hapati kabisa kwa visingizio vya kuchoka na viugonjwa vya usiku asubuhi kapona.
- asubuhi mwanaume ataondoka mwanamke kalala na kama hawana msaidizi basi ataondoka bila kupata japo kikombe cha chai.
- akirudi toka kazini hapati hata pole na akirudi na mzigo atautua nwenyewe ndani
- bedroom hakutandikwi kama zamani
- chakula kinapikwa sivyo ndivyo na hata wakati wa kula hakai nae ili kumpa kampani
- kama ana marafiki basi kutwa ye na marafiki
- Shughuli zote za mjini ni zake ukitaka usitake ataenda.
- hajali tena vaa yako wala kukuweka uwe maridadi
- ukimsema kosa basi hukimbilia kuomba talaka au kutishia kutimka kwao.
- Hulazimisha mambo hata huna uwezo nayo.
Kwa wanaume:
- Simu za mara kwa mara hutoweka na hukupigia kama ana shida au kuna dharura
- Yale majina mazuri hufa na kuitwa kwa jina lako au la mtoto wenu "mama fulani"
- Mikutano, foleni za barabarani, inakuwa sababu ya yeye kurudi usiku wa manane
- Kosa kidogo atakusema kama mtoto na hata kukupiga
- Hajali mahitaji muhimu na hupanga pesa ya matumizi kila siku inatosha/haitoshi juu yako.
- Anakuwa mwenye hasira mara kwa mara na majibu ya mkato yasiyokauka mdomoni.
- Kila siku inakuwa afadhali ya jana.
THAMANI YA MAPENZI KUPUNGUA
Hii nayo ni tatizo kwani mapenzi yakipungua thamani pia huisha ndio utakuta zamani wapenzi walikuwa pamoja kila mahali sasa wanatangulizana mmoja upande huu mwingine kule, kutoheshimiana ndani na nje ya nyumba, hutoleana maneno yasio faa bila kujali, kutoleana siri za ndani kwa marafiki au ndugu, n.k.
MIGOGORO ISIYOKWISHA
inatokea baada ya kushindwa kuambiana kweli, iwapo mwenzio kakosea mwambie kwa lugha nzuri ili ajue lile jambo wewe hupendi, asiweze kulirudia.
ukinyamaza unatengeneza uadui wa ndani kwa ndani, ambao hautajenga bali utabomoa mapenzi yenu, kwani hasira hujenga chuki, nayo hujenga uadui nao hujenga dharau ambayo huzaa mgogoro ambao hupelekea kuachana.
BAADA YA HAPO
- kuna wengine huapa hawatapenda tena milele
- Wengine huwa na visasi vya kuwaumiza wengine kulipa alivyoumizwa yeye
- Wengine huamua kutokuwa na mpenzi na badala yake huangalia sinema za ngono mitandaoni, kupiga punyeto n.k
- hupelekea baadhi yao wakawa kwenye mahusiano ya jinsia moja wakidhani ndio wanaepuka kuumizwa.
- wengine huoa na kuacha au kubadili wapenzi mara kwa mara, kwani wanakuwa hawana tena imani na wapenzi wanao wapata wakidhani ni kama wale walio waumiza.
- wengine huathirika kisaikolojia hata umpende umfanyie mahaba unayo yajua wewe wala haonyeshi dalili ya kuridhika.
TAHADHARI KUPENDA MTU ALIYETENDWA WENGI HUWA HAWANA MAPENZI YA KWELI.
Ok tataaaa kwa leo
Monday, December 30, 2013
TALK ABOUT LOVE - Nini faida ya mapenzi
Assalaam alaykum wasomaji wangu wapendwa,
Habari za weekend nadhani mliifurahia vya kutosha na kwa wale mliopata matatizo basi poleni ni moja katika safari ya maisha.
Haya leo tuendelee na mada yetu usichoke kunifuatilia kwani hii mada ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku nitajitahidi kuchambua ili tuelewe.
NINI FAIDA YA MAPENZI
Mungu alipomuumba Adamu alimuona ni mpweke akamuumbia Hawa (Eva) ili awe mwenza wake, na pia wazae watoto waijaze dunia kama vitabu vya Mungu vinavyo tuambia.
kuwa katika mapenzi kuna faida nyingi sana
- kuwa na akili timamu
- kupata watoto
- kujenga familia
- kuheshimika
Kuwa na akili timamu
Tendo la ndoa humfanya mtu awe na akili timamu, busara, uvumilivu wa changamoto mbali mbali, usamehevu, maamuzi sahihi, usikivu, kujiona ni binadamu kamili.
Kupata watoto
Nayo ni moja ya faida ya mapenzi kwani hata vitabu vya Mungu vimehimiza watu wazae, na vimeelekeza jinsi ya kuwazaa na kuwalea. Pia hakuna Taifa lolote duniani linalokataza wananchi wake wasizae, bali huhimiza watu wazae watoto wanao weza kuwatunza.
Pia kikawaida ndoa nyingi watu hutarajia wapate watoto, ndio maana familia za ndoa hiyo huhangaika sana hospital na kwingineko ili kuleta furaha kwenye ndoa hiyo.
Kujenga familia
Mnapokuwa kwenye mapenzi mkaishi pamoja, tayari mnakuwa mmetengeneza familia kwani ndugu wa mwanaume na mwanamke hupata fursa ya kuwatembelea na kuweza kufurahia umoja wenu. kila mmoja hujihisi hawezi kuishi bila ya mwenzie na hasa kwa wanaume, mke akisafiri utaona anasema mwenye nyumba hayupo bwana. Pia dunia ilianza kama familia ya Adamu na Hawa (Eva).
Kuheshimika
Mapenzi huleta heshima kwa kila mtu kwanza hujiheshimu mwenyewe, pia hufanya watu wakuheshimu unapokuwa mapenzini, kwani utakuwa huna tena mambo ya kuwa na wapenzi wengi muda wote utakuwa unamfikiria mpenzi wako na kuona anakutosha kwa kila kitu, na hujiona umekua, mwenye majukumu juu mpenzi wako, kupanga ratiba ya nyumbani kwako ikiendana na ile ya shughuli zako za kila siku. Pia wanaokutamani watakuheshimu kwani utakuwa busy na mpenzi wako.
Ahsante kwa kunipa muda wako tuonane tena katika kuangalia MADHARA YAKE
UNAWEZA TOA MAONI YAKO
Friday, December 27, 2013
TALK ABOUT LOVE
KWA NINI TUNAPENDA.
Asalaam alaykum wapenzi wasomaji wangu,
Leo hebu tutazame KWA NINI TUNAPENDA.
Kwanza tumeelewa kuwa mapenzi ni maumbile, hivyo hakuna mtu ambaye anayeweza kuyakwepa na hayana tarehe wala umri kwani hayazeeki mapenzi unazeeka mwili tu.
KUNA KUPENDA KWA AINA MBILI
- KUPENDA KIMUONEKANO
- KUPENDA KWA DHATI
KUPENDA KIMUONEKANO
Ni kumpenda mtu kutokana na alivyo, kama umbo, sura, mali, umaarufu n.k
tatizo kikiondoka kile ambacho umempendea na mapenzi huishia hapo hapo.
Mfano:- umempenda mtu kwa sura au umbo lake
akipata ajali au akiumwa na kubadilika kwa sura au umbo lake basi hutampenda tena.
Mali au umaarufu
pia kama ulimpendea mali akifilisika tu basi huna haja nae tena.
Na hii inatokea sana kwa wanawake ambao waliolewa na wanaume kwa ajili ya mali. Mali ikiisha tu visa na karaha ndani, migogoro isiyo sababu, talaka inaombwa pasipo kosa, heshima na utii alokuwa nao unatoweka bila kujali huyu mwanaume alimsaidia vipi wakati ana mali.
Na huenda hata kufirisika kakusababisha yeye mfano:-
- Kutaka vitu vya gharama kubwa kama asset za ndani, magari, madini, shopping za kila mara.
- Kujaza familia yake nyumbani ambayo haina mwendelezo wa kimaisha, na hata mwanaume akiwasaidia mfano, kuwapa mitaji huila na kurudi kuja tegemea hapo.
- Mwanamke kuomba mitaji mikubwa ya biashara ambayo hana elimu nayo na muda mfupi biashara inakufa.
Umaarufu
Hawa ndio mapenzi yao ya muda mfupi sana, ukimpenda mtu kwa ajili ya umaarufu tegemea kulizwa tuu hakuna kingine.
kwani wao wenyewe hata kama wanapenda lakini kwa vile wanajijua ni maarufu hawakosi mpenzi basi hata kama anakupenda, mazingira waliyo nayo yatakupa shida sana na mwishowe utasarenda.
angalia Mastaa wengi duniani hawadumu na wapenzi wao.
Pia kwa Staa hivyo hivyo atapendwa na wengi sana lakini umaarufu ukiisha baasi.
MAPENZI YA DHATI
Ni mapenzi ya aina yake kwa kweli, maana yanateka roho na mwili, huwezi jizuia hata kama utajaribu vipi.
Dalili zake:-
- Kila umuonapo au umuwazapo basi mapigo ya moyo huenda mbio na hutamani uwe nae muda wote.
- Akipatwa na jambo mfano, kaumwa, kapata ajali au kagombana n.k utajikuta akili na mawazo yako yote yanashughulishwa na hilo jambo hutajali kingine chochote mpaka uhakikishe lile jambo kaondokana nalo.
- Hujitolea kwa hali na mali kuhakikisha mpenzi wako anakuwa na furaha muda wote.
- Kila mara humuwazia mazuri mpenzi wako hata uambiwe labda mpenzi wako anakusaliti wala huamini tena aliyekwambia utamfanya adui wa penzi lenu.
- Kila kitu kinachokuhusu wewe na maisha yako utataka mpenzi wako ajue.
- Utapenda utangaze ulimwengu mzima kuwa unampenda fulani
- Huwa mwaminifu sana hata kama kuna mtu anakutaka kimapenzi basi huona kama mpenzi wako anakuona, na wengine hudiriki kuwaambia wapenzi wao wanapongozwa.
- hujitahidi sana kufanya mambo yanayompendeza mpenzi wako mfano wengi labda alikuwa na tabia ya ulevi, uzinzi, dharau akaacha kwa sababu mpenzi wake hataki.
- hukubali kuishi maisha yoyote aliyo nayo mpenzi wake na huridhika na kila anachopewa hata kama kidogo na cha thamani ya chini kiasi gani
- Yupo tayari kufa kwa kupigania penzi na sio tayari kuliacha penzi life.
Na mengine mengi yanayofanana na haya.
Ok tuonane tena kwa sehemu yetu nyingine ya TALK ABOUT LOVE
Si vibaya ukitoa maoni yako
Thursday, December 26, 2013
KWA NINI TUNAPENDA
KWA NINI TUNAPENDA?
Kwanza kabisa tuelewane kuwa kuna kupenda na kutamani
KUTAMANI
NI kumtamani mtu kwa ajili ya tendo yaani unakuwa na hamu ya kufanya nae ngono kisha baada ya hapo utakuwa unamtafuta pindi utapopata hamu tena.
Na hii ina madhara makubwa sana kuliko faida, hasa kwa wanawake wa kiafrika.
Kwanini?
kwa sababu wanawake wa kiafrika hasa wa Kitanzania maadili na mwenendo wao mwanamke hata awe mzuri hutegemea atongozwe na mwanaume.
Sasa kiakili hasa ambao wapo kwenye foolish age huona raha sana kutongozwa na hata huweza ongea mbele ya wenzake kuwa ametongozwa na fulani.
Bila kuwa mwangalifu hukubali kuingia kwenye mahusiano bila kufikiria mara mbili na hasa kama aliyemtongoza atakuwa na uwezo, maarufu au mzuri, ndio kabisa.
Bila kuchunguza kama huyu mtu alikuwa anamtamani na sio kumpenda.
UTAJUAJE KAMA HUYU MWANAUME ANAKUTAMANI?
1. Hajali kujua mambo yako yaani mwonekano wako katika jamii
2. anakupa sifa zingine hata huna
3. huwa na pupa ya kutaka tendo la ngono kila mnapokutana na si maongezi mengine
4. hajali mawasiliano yako yaani kama simu akupigie yeye wewe ukipiga anaweza asipokee.
5. hana adabu katika maongezi na mbele za watu hutaka kujionyesha kuwa yeye mpenzi wako.
Ni baadhi tu ya dalili za mwanaume anayemtamani mwanamke.
FAIDA
hakuna faida kwa mwanaume kama huyu zaidi ya kujeruhi moyo wako
MADHARA
ni makubwa sana tena yanaharibu mfumo mzima wa vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla
Baada ya tendo la ngono:-
1. Sifa alizokuwa anakupa, we mzuri na nini vinakata
2. Majina mara baby, honey, sweetheart yanakufa utaitwa jina ulilopewa na wazazi wako.
3. Mawasiliano ya mara kwa mara yanapungua na sababu nipo busy, mikutano, safari
visingizio viingi.
4. Kama alikuwa anakutoa out zinapungua kama sio kwisha kabisa, na kama ulikuwa unapewa
pesa ya taksi sasa utaambiwa kopa atalipa wakati hatalipa, au panda dala dala.
5. kama ulitoa shida basi kutakuwa na visingizio visivyokuwa na idadi
6. Ole wako umwambie una mimba majibu yake yatakuwa hivi:-
a. Wee nani kakwambia kubeba ndio tulivyokubaliana ah utajua mwenyewe na ole wako unitaje.
b. Hapana sio yangu mtu mwenyewe una mabwana chungu nzima unadhani sijui, habari zako
zote ninazo.
c. Mmmh basi tuitoe bwana mi si unajua nina mke nyumbani sasa unadhani akijua itakuwaje.
d. Ah basi nitaitunza lakini usinitaje iwe siri yetu
na mengine mengi majibu yasiyo na mwelekeo ukiona hivyo ujue imekula kwako.
MATOKEO YAKE
- unaathirika kisaikolojia na kuwachukia wanaume wote duniani
- magonjwa ya zinaa, ukimwi n.k
- kama utazaa mtoto pia nae hatakuwa na furaha kama watoto wenzie wenye baba na mama.
- hatakuwa na matunzo bora kama mama huna uwezo
- hatasoma vizuri na wengi huishia la saba.
- kama mtoto wa kike mara nyingi nae huishia kuzalishwa akiwa na umri mdogo.
- umasikini unakuwa kwa kasi ya ajabu.
- Taifa linakosa nguvu kazi.
haya na mengine mengi sana ambayo yanawakuta wanawake kwa jambo moja tu KUTAMANI
Tuonane tena msomaji hapa hapa
`
Tuesday, December 24, 2013
MAPENZI NI NINI
Tunaanza kuchambua maswali yetu tuliyo yaweka jana hapa na tuanze na swali la kwanza
MAPENZI NI NINI
Kwa haraka haraka ukiulizwa mapenzi ni nini utajibu ni wawili wapendanao kitu ambacho sio kweli
ingekuwa kweli wapendanao wasingekuja kuachana.
Ukweli ni kwamba, mapenzi ni maumbile yana roho yanatembea na kuishi kama alivyo mwanadamu.
KWANINI?
Kwa sababu jiulize umependa mara ngapi ukaumizwa mara ngapi na iliapa mara ngapi kuwa hutopenda tena na ukarudi ukapenda.
Na wakati unapenda unakuwa kama mtu ambaye unaishi maisha ya raha ya pekee ambayo unadhani hakuna yeyote dunia hii anaefaidi mapenzi kama wewe.
na ukitendwa unaiona dunia haifai, hakuna raha duniani, aliyekutenda unamuona adui wa maisha yako, ukiona watu wanapendana unawaona wajinga na kuwafikiria nao watayapata yaliokukuta wewe.
Ndani ya moyo wako utajuta na kusononeka kwanini ulipenda, kwanini ulitumia muda wako na pesa pengine katika kudumisha mapenzi yako. na hupelekea mpaka ukaapa kuwa hutopenda tena na kuwaonya watu kuhusu kuendekeza mapenzi.
Je ni kweli hutopenda tena?
tuonane hapa hapa
Monday, December 23, 2013
TALK ABOUT LOVE
Leo hebu tuongee kuhusu mapenzi
1. mapenzi ni nini
2. kwanini tunapenda
3. nini faida ya mapenzi
4. nini madhara ya mapenzi
5. hivi kuna mwalimu wa mapenzi kweli
6. nani anastahili kupenda
7. nani anastahili kupendwa
8. kwanini hatuwezi kuishi bila mapenzi
basi na mengine mengi tutayapa hapa hapa stay tuned
1. mapenzi ni nini
2. kwanini tunapenda
3. nini faida ya mapenzi
4. nini madhara ya mapenzi
5. hivi kuna mwalimu wa mapenzi kweli
6. nani anastahili kupenda
7. nani anastahili kupendwa
8. kwanini hatuwezi kuishi bila mapenzi
basi na mengine mengi tutayapa hapa hapa stay tuned
Friday, December 20, 2013
MAWAZIRI WANNE WA SERIKALI YA JAMHURI YA TANZANIA WANG'OKA KATIKA NAFASI ZAO KUTOKANA NA RIPOTI MBAYA YA OPERATION TOKOMEZA UJANGILI.
MHE. JUMA KAGASHEKI - Mali ya asili na Utalii
MHE. MATHAYO DAVID MATHAYO - Mifugo na Uvuvi
MHE. SHAMSI VUAI NAHODHA - Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE: EMANUEL NCHIMBI - Mambo ya ndani
MHE. JUMA KAGASHEKI - Mali ya asili na Utalii
MHE. MATHAYO DAVID MATHAYO - Mifugo na Uvuvi
MHE. SHAMSI VUAI NAHODHA - Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE: EMANUEL NCHIMBI - Mambo ya ndani
Subscribe to:
Posts (Atom)