Tuesday, December 31, 2013

TALK ABOUT LOVE - Madhara ya mapenzi







Natumaini mmeamka salama na leo tunakutana tena hapa, mi pia sijambo, kwa wale wanaoumwa basi nawaombea kwa Mungu wapone haraka na kuendelea na harakati za kila siku.

MADHARA YA MAPENZI
Ni makubwa sana yanayumbisha dunia inasababisha watu kuwa wakatili kama wanyama, heshima na utu unatoweka, mtu anadhalilika mbele ya jamii, familia inasambaratika na kupelekea watoto kukosa huduma bora  kama kusoma, mahitaji muhimu, na hatimaye kupatikana watoto wa mitaani.

Chanzo chake ni nini

  1. Kuvunja uaminifu mmoja wenu 
  2. Kuishi kwa mazoea
  3. Thamani ya mapenzi kupungua 
  4. Migogoro isiyokwisha.
KUVUNJA UAMINIFU
Inapotokea mmoja wenu akavunja uaminifu ina maana akawa na mpenzi mwingine wakati mko pamoja basi ujue ndani mabadiliko yataonekana kwa sababu moyo ni mmoja hauwezi kupenda watu wawili na ukawa sawa.  Hivyo hupelekea mwenza kuona hajaliwi, habembelezwi kama zamani, kauli zinakuwa za mkato, heshima inapungua, inafikia kujibizana mbele za watu kama maadui fulani.

KUISHI KWA MAZOEA 
Ni kwa wapenzi ambao mwanzo walikuwa wanajishughulisha sana kwa wapenzi wao mfano kwa mwanaume:-
Mwanzo wa mapenzi 
 anakuwa simu kila mara,
 majina ya mapenzi yote utaitwa mara baby,honey,sweetheart,na mengine mengi ya mapenzi,
 zawadi mbali mbali,
 shopping za haja,
 anawahi kurudi nyumbani na siku za mapumziko hatoki labda kwa dharura, 
muda wote anapenda akuone na kila unachovaa lazima akusifie,
huomba msamaha pindi anapokosea n.k.

kwa mwanamke:-
anakuwa msafi muda wote,
hufanya vitu vinavyompendeza mumewe kama kupika chakula n.k.
hatoki nyumbani bila ruhusa ya mumewe na akitoka hurudi haraka ili asimuudhi mumewe,
hujipamba kadiri anavyoweza ili amvutie mumewe
huongea sauti laini na taamu tena ya chini ili ampendeze mumewe
anahakikisha mpenziwe anamuogesha na kumtayarishia nguo, viatu n.k
akikosa huomba radhi kwa magoti huku akibembeleza na kulia ili asamehewe na kuahidi kutorudia tena.

Baada ya muda mfupi wa maisha haya ya pamoja.
 haya yote mazuri hutoweka hasa kwa wanawake kama alifanya haya alikuwa hajaolewa,
 akishaolewa tu  baaasi hugeuka na kuwa hivi:-
  • chakula cha usiku - yaani tendo la ndoa inakuwa mpaka mwanaume alazimishe na siku zingine hapati kabisa kwa visingizio vya kuchoka na viugonjwa vya usiku asubuhi kapona.
  • asubuhi mwanaume ataondoka mwanamke kalala na kama hawana msaidizi basi ataondoka  bila kupata japo kikombe cha chai.
  • akirudi toka kazini hapati hata pole na akirudi na mzigo atautua nwenyewe ndani
  • bedroom hakutandikwi kama zamani 
  • chakula kinapikwa sivyo ndivyo na hata wakati wa kula hakai nae ili kumpa kampani
  • kama ana marafiki basi kutwa ye na marafiki
  • Shughuli zote za mjini ni zake ukitaka usitake ataenda.
  • hajali tena vaa yako wala kukuweka uwe maridadi
  • ukimsema kosa basi hukimbilia kuomba talaka au kutishia kutimka kwao.
  • Hulazimisha mambo hata huna uwezo nayo.
Kwa wanaume:
  • Simu za mara kwa mara hutoweka na hukupigia kama ana shida au kuna dharura
  • Yale majina mazuri hufa na kuitwa kwa jina lako au la mtoto wenu "mama fulani"
  • Mikutano, foleni za barabarani, inakuwa sababu ya yeye kurudi usiku wa manane
  • Kosa kidogo atakusema kama mtoto na hata kukupiga
  • Hajali mahitaji muhimu na hupanga pesa ya matumizi kila siku inatosha/haitoshi juu yako.
  • Anakuwa mwenye hasira mara kwa mara na majibu ya mkato yasiyokauka mdomoni.
  • Kila siku inakuwa afadhali ya jana.
THAMANI YA MAPENZI KUPUNGUA
Hii nayo ni tatizo kwani mapenzi yakipungua thamani pia huisha ndio utakuta zamani wapenzi walikuwa pamoja kila mahali sasa wanatangulizana mmoja upande huu mwingine kule, kutoheshimiana ndani na nje ya nyumba, hutoleana maneno yasio faa bila kujali, kutoleana siri za ndani kwa marafiki au ndugu, n.k.

MIGOGORO ISIYOKWISHA
inatokea baada ya kushindwa kuambiana kweli, iwapo mwenzio kakosea mwambie kwa lugha nzuri ili ajue lile jambo wewe hupendi, asiweze kulirudia.
ukinyamaza unatengeneza uadui wa ndani kwa ndani, ambao hautajenga bali utabomoa mapenzi yenu, kwani hasira hujenga chuki, nayo hujenga uadui nao hujenga dharau ambayo huzaa mgogoro ambao hupelekea kuachana.

BAADA YA HAPO
  • kuna wengine huapa hawatapenda tena milele 
  • Wengine huwa na visasi vya kuwaumiza wengine kulipa alivyoumizwa yeye
  • Wengine huamua kutokuwa na mpenzi na badala yake huangalia sinema za ngono mitandaoni, kupiga punyeto n.k
  • hupelekea baadhi yao wakawa kwenye mahusiano ya jinsia moja wakidhani ndio wanaepuka kuumizwa.
  • wengine huoa na kuacha au kubadili wapenzi mara kwa mara, kwani wanakuwa hawana tena imani na wapenzi wanao wapata wakidhani ni kama wale walio waumiza.
  • wengine huathirika kisaikolojia hata umpende umfanyie mahaba unayo yajua wewe wala haonyeshi dalili ya kuridhika.
TAHADHARI KUPENDA MTU ALIYETENDWA WENGI HUWA HAWANA MAPENZI YA KWELI.

Ok tataaaa kwa leo




No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako