Friday, December 27, 2013

TALK ABOUT LOVE






KWA NINI TUNAPENDA.


Asalaam alaykum wapenzi wasomaji wangu,
Leo hebu tutazame KWA NINI TUNAPENDA.
Kwanza tumeelewa kuwa mapenzi ni maumbile, hivyo hakuna mtu ambaye anayeweza kuyakwepa na hayana tarehe wala umri kwani hayazeeki mapenzi unazeeka mwili tu. 

KUNA KUPENDA KWA AINA MBILI
  1. KUPENDA KIMUONEKANO
  2. KUPENDA KWA DHATI

KUPENDA KIMUONEKANO
Ni kumpenda mtu kutokana na alivyo, kama umbo, sura, mali, umaarufu n.k
tatizo kikiondoka kile ambacho umempendea na mapenzi huishia hapo hapo.

Mfano:- umempenda mtu kwa sura au  umbo lake
akipata ajali au akiumwa na kubadilika kwa sura au umbo lake basi hutampenda tena.

Mali au umaarufu
pia kama ulimpendea mali akifilisika tu basi huna haja nae tena.
Na hii inatokea sana kwa wanawake ambao waliolewa na wanaume kwa ajili ya mali.  Mali ikiisha tu visa na karaha ndani, migogoro isiyo sababu, talaka inaombwa pasipo kosa, heshima na utii alokuwa nao unatoweka bila kujali huyu mwanaume alimsaidia vipi wakati ana mali. 
Na huenda hata kufirisika kakusababisha yeye mfano:-
  • Kutaka vitu vya gharama kubwa kama asset za ndani, magari, madini, shopping za kila mara.
  • Kujaza familia yake nyumbani ambayo haina mwendelezo wa kimaisha, na hata mwanaume akiwasaidia mfano, kuwapa mitaji huila na kurudi kuja tegemea hapo.
  • Mwanamke kuomba mitaji mikubwa ya biashara ambayo hana elimu nayo na muda mfupi biashara inakufa.
Haya na mengine mengi humfanya mwanaume afilisike na thamani na utu wake huishia hapo.  Na hata wapo wanaume wanao wapenda wanawake kwa ajili ya mali pia lakini sio wengi sana kama wanawake.

Umaarufu
Hawa ndio mapenzi yao ya muda mfupi sana, ukimpenda mtu kwa ajili ya umaarufu tegemea kulizwa tuu hakuna kingine.  
kwani wao wenyewe hata kama wanapenda lakini kwa vile wanajijua ni maarufu hawakosi mpenzi basi hata kama anakupenda, mazingira waliyo nayo yatakupa shida sana na mwishowe utasarenda.
angalia Mastaa wengi duniani hawadumu na wapenzi wao.
Pia kwa Staa hivyo hivyo atapendwa na wengi sana lakini umaarufu ukiisha baasi.

MAPENZI YA DHATI
Ni mapenzi ya aina yake kwa kweli, maana  yanateka roho na mwili, huwezi jizuia hata kama utajaribu vipi.
Dalili zake:-
  • Kila umuonapo au umuwazapo basi mapigo ya moyo huenda mbio na hutamani uwe nae muda wote.
  • Akipatwa na jambo mfano, kaumwa, kapata ajali au kagombana n.k  utajikuta akili na mawazo yako yote yanashughulishwa na hilo jambo hutajali kingine chochote mpaka uhakikishe lile jambo kaondokana nalo.
  • Hujitolea kwa hali na mali kuhakikisha mpenzi wako anakuwa na furaha muda wote.
  • Kila mara humuwazia mazuri mpenzi wako hata uambiwe labda mpenzi wako anakusaliti wala huamini tena aliyekwambia utamfanya adui wa penzi lenu.
  • Kila kitu kinachokuhusu wewe na maisha yako utataka mpenzi wako ajue.
  • Utapenda utangaze ulimwengu mzima kuwa unampenda fulani 
  • Huwa mwaminifu sana hata kama kuna mtu anakutaka kimapenzi basi huona kama mpenzi wako anakuona, na wengine hudiriki kuwaambia wapenzi wao wanapongozwa.
  • hujitahidi sana kufanya mambo yanayompendeza mpenzi wako mfano wengi labda alikuwa na tabia ya ulevi, uzinzi, dharau akaacha kwa sababu mpenzi wake hataki.
  • hukubali kuishi maisha yoyote aliyo nayo mpenzi wake na huridhika na kila anachopewa hata kama kidogo na cha thamani ya chini kiasi gani
  • Yupo tayari kufa kwa kupigania penzi na sio tayari kuliacha penzi life.
Na mengine mengi yanayofanana na haya.
Ok tuonane tena kwa sehemu yetu nyingine ya TALK ABOUT LOVE
Si vibaya ukitoa maoni yako







No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako