Assalaam alaykum wasomaji wangu wapendwa,
Habari za weekend nadhani mliifurahia vya kutosha na kwa wale mliopata matatizo basi poleni ni moja katika safari ya maisha.
Haya leo tuendelee na mada yetu usichoke kunifuatilia kwani hii mada ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku nitajitahidi kuchambua ili tuelewe.
NINI FAIDA YA MAPENZI
Mungu alipomuumba Adamu alimuona ni mpweke akamuumbia Hawa (Eva) ili awe mwenza wake, na pia wazae watoto waijaze dunia kama vitabu vya Mungu vinavyo tuambia.
kuwa katika mapenzi kuna faida nyingi sana
- kuwa na akili timamu
- kupata watoto
- kujenga familia
- kuheshimika
Kuwa na akili timamu
Tendo la ndoa humfanya mtu awe na akili timamu, busara, uvumilivu wa changamoto mbali mbali, usamehevu, maamuzi sahihi, usikivu, kujiona ni binadamu kamili.
Kupata watoto
Nayo ni moja ya faida ya mapenzi kwani hata vitabu vya Mungu vimehimiza watu wazae, na vimeelekeza jinsi ya kuwazaa na kuwalea. Pia hakuna Taifa lolote duniani linalokataza wananchi wake wasizae, bali huhimiza watu wazae watoto wanao weza kuwatunza.
Pia kikawaida ndoa nyingi watu hutarajia wapate watoto, ndio maana familia za ndoa hiyo huhangaika sana hospital na kwingineko ili kuleta furaha kwenye ndoa hiyo.
Kujenga familia
Mnapokuwa kwenye mapenzi mkaishi pamoja, tayari mnakuwa mmetengeneza familia kwani ndugu wa mwanaume na mwanamke hupata fursa ya kuwatembelea na kuweza kufurahia umoja wenu. kila mmoja hujihisi hawezi kuishi bila ya mwenzie na hasa kwa wanaume, mke akisafiri utaona anasema mwenye nyumba hayupo bwana. Pia dunia ilianza kama familia ya Adamu na Hawa (Eva).
Kuheshimika
Mapenzi huleta heshima kwa kila mtu kwanza hujiheshimu mwenyewe, pia hufanya watu wakuheshimu unapokuwa mapenzini, kwani utakuwa huna tena mambo ya kuwa na wapenzi wengi muda wote utakuwa unamfikiria mpenzi wako na kuona anakutosha kwa kila kitu, na hujiona umekua, mwenye majukumu juu mpenzi wako, kupanga ratiba ya nyumbani kwako ikiendana na ile ya shughuli zako za kila siku. Pia wanaokutamani watakuheshimu kwani utakuwa busy na mpenzi wako.
Ahsante kwa kunipa muda wako tuonane tena katika kuangalia MADHARA YAKE
UNAWEZA TOA MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako