Leo naomba niseme na wewe mume au mwanaume umeishi na mkeo/mpenzio na kwa makubaliano mazuri kabisa mkaamua mpate mtoto.
Kazi inaanzia hapo, karaha za mimba kila mtu anazijua kuanzia ikiwa changa mpaka kujifungua.
Mkeo hali chakula kizuri, anachagua vyakula, mara katapika, halali usingizi mzuri, anakasirika bila sababu, anaweza kumchukia mtu bila kisa au akakupenda wewe mumewe mpaka akawa anakaa na shati lako chafu akinusa mwenyewe anajisikia raaaha mustarehe. Au akakuchukia mpaka ukatamani kuhama nyumba.
Hayo yote mume inabidi uyavumilie ni ya muda, akijifungua yataisha.
Basi inatakiwa urudi nyumbani mapema ili umliwaze kwa maneno mazuri, msaidie anapokuwa anahitaji msaada, mtoe out siku moja moja ili aliwazike.
Maana kubeba roho mbili jamani kazi hivyo, msione wengine wanazitoa mimba mkaona makatili, sometime na nyie huwa sababu unapunguza mapenzi ndani, karaha mtindo mmoja, unamuona mkeo anatapika unachukia na kukunja uso kama kafanya kusudi unashika njia yulee asiitoe kwanini maana anaona inamnyima raha, inampotezea mume.
Haya mtoto akizaliwa mnatakiwa mshirikiane katika kumlea, umerudi umemkuta amejisaidia mtoe pampas mvike nyingine, analia msaidie mkeo kumbembeleza toka nae utembee nae kidogo huenda mkeo ana kazi jikoni, ikibidi muogeshe, cheza naye ili mkeo naye apumzike.
Lakini kinyume ndio kwanza unatafuta mchepuko wako mwenyewe, unajipoooza hukooo unarudi saa nane za usiku unamgongea huna hata huruma mwenzio kashinda na madhila yote hayo bado huenda ndio kwanza kapata usingizi unamtia karaha nyingine.
Mlipo oana ukaapa utamtunza kwa shida na raha ulidhani shida gani nyingine?
Ina maana we unapenda uitwe baba fulani tu lakini shida zote za mimba, mtoto mama ndio astahmili.
We naye mtaonana mtoto akikua ili utie mimba nyingine uendelee na michepuko yako.

Halafu unalalamika mtoto hakupendi anampenda mama yake atakupendaje naye mpaka anajua kuongea hakuoni kama unafanya kazi kwenye dala dala unatoka alfajiri unarudi usiku.
Matokeo yake mapenzi ndani yanaisha yanabaki mazoea, tangu mlikuwa mnaitana honey, baby, sweetheart,darling na mengineyo majina ya mahaba mpaka mnafikia kuitana "we baba/mama fulani ina maana hunisikii".
Kila ukiingia nyumbani kwako sura umeikunja kama unaenda vitani. Ukija na marafiki unawatambulisha huyu ndio mama watoto, sio kipenzi mke wangu ulivyokuwa huna haya.
Ndio si mapenzi yameisha mnabaki mnalea tu watoto hata wageni wakija wanajua tofauti zenu kila mtu anamlalamikia mwenzie ndio chanzo kumbe chanzo mtoto.
Mhurumie mpenzio/mkeo anapokuwa mjamzito au analea leeni wote jamani.
BAKI NJIA KUU MICHEPUKO INAUA FAMILIA.
Toa maoni yako