Sunday, February 9, 2014

Mwanamke hulka

Habari za weekend wapendwa,
Mi kwangu ilikuwa poa sana 

Leo naomba niseme na wewe mke wa mtu




Jamani kuna wadada wengine akiwa kwenye mahusiano anakuwa na tabia nzuri, mpole, mwenye adabu, msafi, mnyenyekevu mpaka ndugu na jamaa wa mwanaume wanakubali huyu ndie mwanamke wa kuoa.

Ndoa ikifungwa Mungu wangu hata sijui binadamu wengine wameumbwaje, mi siwezi kuigiza kabisa. Ataanza kero ndani ya nyumba, mumewe na familia yake kama ipo watashika adabu.

Mara umegomba bila sababu kosa kidogo utauvuta mdomo, haueleweki kama foleni za barabarani, utadhani ulilazimishwa kuolewa.

Mumeo amerudi amechoka na kazi na vurugu za kazini badala ya kupata utulivu anaambulia maumivu,  ndio unakuta anampigia rafiki yake "ee bwana uko wapi tukutane pale basi" kumbe alikuwa hana nia ya kutoka anakimbia kero zako.
unakuta mwanaume anakonda kama anaumwa we ndio unanenepa tuu hata haya huna.

Na hakuna maneno yanayowaumiza wanaume kama haya:-

Ndio unarudi saa hizi mi sipendi kabisa kesho ukichelewa utafute mlango wa kugonga. [kesho yake asiporudi je]

Pesa unayoniachia hata haitoshi kabisa. [kama ndio uwezo wake je]

Mbona hukurudi na mkate kesho tunanywea nini chai. [we kwenda dukani huwezi]

Mi leo sitaki kupika kama vipi tukale chips. [ndivyo mlivyopanga]

Mama yako anakera nimevaa ile nguo mpya kanitazama kama nini sijui alitaka umnunulie yeye.

[angekuangalia mama yako mzazi je]

Ndugu zako wana maneno sana siwataki humu ndani au chagua kati ya ndugu zako au mimi.
[wangekuwa nduguzo je]

Jirani kanunua dish na sie tununue. [maisha ya kuiga]

Mashtaka ya watoto kama alivunja kikombe, sijui huyu alikataa kwenda wapi basi yote mambo ya kutwa nzima unamlundikia. [we huwezi kuwaonya ]


Nimepita pale mtaa wa pili yule dada akanicheka.   [kwa hiyo akapigane]
  
Ina maana hii ndio nguo umeona naweza kuvaa mie mpelekee dada yako mi siwezi kuvaa nguo kama hii.    [zawadi hiyo]

Malalamiko kila ndugu, jamaa, rafiki unamwelezea mume wangu hivi mume wangu vile. [unamtia aibu]

Kama mume anajua kupika basi magonjwa yatakuwa hayaishi kila ikifika jioni ili akirudi kazini apike.
Siri za ndani zote unaongea kwa majirani na marafiki.

Maneno ya mitaani sijui mama fulani kapigwa huyu kasutwa yanamhusu nini muda huo unatakiwa muongelee mapenzi yenu na maendeleo ya maisha yenu.

Ndio akitoka kazini akakae na marafiki mpaka usiku wa manane maana ndio wanaoweza kumpa faraja.

Jamani tuwaonee huruma watoto wa wanawake wenzetu, familia zao zinawalaumu kuwa wanatuendekeza, na sie pia tunawapa joto hasira mmh ki ukweli tubadilike.

Nyumba ndogo wakati mwingine tunazileta wenyewe mwanaume ni mtoto kila siku anapenda adekezwe, aoshwe, avishwe, sasa ukiwa mama wa kambo kwa mumeo atakuthamini vipi?  

Ushauri wangu tuwe kama panya tuume na kupuliza, unapokazana kuomba hela kazana na kumhudumia vizuri mume jamani, 
Sio madhali ndoa ya kifo kitutenganishe basi unaona hapa hakuna kuachana  lakini kumbuka furaha na amani ndani ya nyumba ikikosekana hata wewe mwenyewe utaiona ndoa chungu.  Na mwishowe kuachiwa nyumba mwanaume anaondoka na suruali zake.

Badilika ndoa sio pete ni amani na upendo ndani ya nyumba.
Tchao

Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako