Thursday, February 6, 2014

MAPENZI SIO CHAKULA CHA USIKU TUU.


Leo tuongelee upande wa waume zetu.



Mwanaume nyumbani kwako ndio mahali pa faraja umetoka kuhangaika machovu ya kazini unapozea home kwa kuiona familia yako ipo salama wamekula, unapanga nao mikakati ya kesho, sio unakuwa mkali kama pili pili, mkeo na watoto wakikuona wanachanganyikiwa.

Mwanaume unaandaliwa kila kitu kuanzia mavazi, chakula, maji ya kuoga na vinginevyo, kumwambia mkeo ahsante washindwa.

Mwanaume unatoka kwenda kazini hata busu kwa mkeo hakuna, ile kumuaga tuu mwenzio shida.
Unarudi kazini ukifika nyumbani mkeo anakupokea kwa furaha na bashasha basi hata kutabasamu na kumuonyesha furaha mkeo hakuna zaidi ya kuitika kwa kichwa au mmmh. Wakati mwenzio alikuwa hana raha anawaza utarejea saa ngapi ili awe nawe.

Mnakaa sebuleni kama mtu na mkwewe kila mtu kochi lake, basi we jicho  kwenye tv tena channel unayotaka, maongezi na mkeo huna zaidi ya kumuuliza kama chakula tayari, na mnapokula kimya kama maadui hata kumsifia mkeo kama chakula kizuri inashindikana, basi kama kazidisha chumvi kidogo ndio utamgomba kama mtoto.

Ukitoka hapo unapanda kitandani kimya unamwacha mkeo kwenye wakati mgumu, hajui leo utakula chakula cha usiku ama laa.  Basi masikini mwanamke huyu baada ya kumaliza shughuli zake za kukuandalia mavazi yako viatu abrash mwenyewe atapanda kitandani kimya kimya, ole wake akutupie hata mkono unautupa “mi  nimechoka bwana”. Na hata kama ukikitaka basi hakuna maneno mazuri zaidi ya mkono kumpelekea kuwa akae tayari maana we ndio unataka.

Ndani mwenu upate muda wa kucheza na mpenzio/mkeo utani kidogo sio kila wakati we busy na simu au magazeti mkeo akikusemesha unamjibu kwa karaha.

Kama unavuta sigara ndio utapanda nazo hadi kitandani bila kujali mwenzio anaichukuliaje harufu ya sigara. 
Mkeo/mpenzio akikosea basi utamsema  chumbani ambako ni nyie wawili tuu ndio mnaokitumia, sio kumsema  mbele ya familia au  hata mbele za watu mpaka anajiona hafai kuitwa mwanadamu.
Matendo haya hata kama mkeo anakupenda namna gani hatakuwa na furaha maishani mwake, ile akikuona tu basi roho yake inamwenda mbio kama kaona simba.

Ukitoka hatamani urudi na ukirudi anaomba usiku uche ili uondoke.


Haya ndio niliyoyaona kwenye maswali ya wanawake wengi.






Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako