Haya mwana dada alipomkuta mganga kachafuka, ilibidi amwambie ajisafishe kwenye bwawa akamwazima kitenge ajifunge safari ya kurudi ikaanza. Walipofika nyumbani mganga akamwuliza mwana dada
Tuliishia pale mganga alipopiga mweleka baada ya kumuona simba akikupuliwa manyoya ya shingo,
Mganga: kuanzia asubuhi mpaka jioni huwa unafanya nini kwa ajili ya mumeo?
Mwanadada: wafanyakazi wapo tena nimeweka wanne kwa ajili ya mume wangu
Mganga: siku anayorudi mumeo huwa unampokeaje?
Mwanadada: huwa namgombeza kwa nini harudi mapema au huwa analala wapi yaani huwa nachukia sana kwani najitahidi kumgharamia, pesa za matumizi nampa lakini bado ananifanyia hivyo.
Mganga: basi nitakupa hiki kitu uweke chini ya ulimi wako kisha akija mumeo useme sauti ya upole ili asikione kwani akikiona tu dawa itaharibika, baada ya siku saba kisha urudi.
akampa kichangarawe kidogo sana akamwambia asikiteme labda wakati wa kula na kulala.
Mwanadada akarudi nyumbani basi akaweka kile kitu.
Jioni mumewe aliporudi akashangaa anakaribishwa kwa sauti nzuri ya upole, , wakati alizoea makelele majirani wote walikuwa wanazima redio. akamuuliza mkewe kama anaumwa mkewe akamjibu yuko sawa.
Mmh siku hiyo akaona maajabu kakaribishwa chakula mkewe hakubanduka mezani mpaka kamaliza kula, kapelekwa bafuni kasingwa jamani eeeh, karudishwa chumbani vizuri bila kelele. Sasa akaanza kuwaza atatokaje maana alizoea mkewe akianza kugomba tu yeye anapata kisingizio cha kutoka eti anakimbia kelele.
Siku hiyo kelele hakuna ataondokaje? Ikabidi awe mpole akalala asubuhi mkewe upole ndio ukazidi na ukarimu, mpaka mume akaogopa tena akaona labda anamlainisha ili amuuwe.
Zilipotimu siku saba mwana dada akarudi kwa mganga na zawadi na pesa za kutosha huku akiwa amefurahi sana mganga kaweza kumrudisha mumewe nyumbani, mganga akamuuliza je umefanikiwa?
akajibu tena asilimia 200, basi mganga akamwambia siku akiacha masharti aliyompa mumewe ataondoka tena.
Mpendwa msomaji wangu hivi kweli ilikuwa ni dawa au matendo ya mwana dada ndiyo yalimrudisha mume nyumbani? Jibu unalo.
MAPENZI HAYANA MGANGA
Week end njema
Toa maoni yako
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako