Tuesday, February 18, 2014

Mimba si ugonjwa mpende mkeo

Assalaam alaykum wapendwa wasomaji wangu,

Leo naomba niseme na wewe mume au mwanaume umeishi na mkeo/mpenzio na kwa makubaliano mazuri kabisa mkaamua mpate mtoto.



Kazi inaanzia hapo,  karaha za mimba kila mtu anazijua kuanzia ikiwa changa mpaka kujifungua.

Mkeo hali chakula kizuri, anachagua vyakula, mara katapika, halali usingizi mzuri, anakasirika bila sababu, anaweza kumchukia mtu bila kisa au akakupenda wewe mumewe mpaka akawa anakaa na shati lako chafu akinusa mwenyewe anajisikia raaaha mustarehe.  Au akakuchukia mpaka ukatamani kuhama nyumba.

Hayo yote mume inabidi uyavumilie ni ya muda, akijifungua yataisha.

Basi inatakiwa urudi nyumbani mapema ili umliwaze kwa maneno mazuri, msaidie anapokuwa anahitaji msaada, mtoe out siku moja moja ili aliwazike. 

Maana kubeba roho mbili jamani kazi hivyo, msione wengine wanazitoa mimba mkaona makatili, sometime na nyie huwa sababu unapunguza mapenzi ndani, karaha mtindo mmoja,  unamuona mkeo anatapika unachukia na kukunja uso kama kafanya kusudi unashika njia yulee asiitoe kwanini maana anaona inamnyima raha, inampotezea mume.

Haya mtoto akizaliwa mnatakiwa mshirikiane katika kumlea, umerudi umemkuta amejisaidia mtoe pampas mvike nyingine, analia msaidie mkeo kumbembeleza toka nae utembee nae kidogo huenda mkeo  ana kazi jikoni, ikibidi muogeshe, cheza naye ili mkeo naye apumzike.

Lakini kinyume ndio kwanza unatafuta mchepuko wako mwenyewe, unajipoooza hukooo unarudi saa nane za usiku unamgongea huna hata huruma mwenzio kashinda na madhila yote hayo bado huenda ndio kwanza kapata usingizi unamtia karaha nyingine.

Mlipo oana ukaapa utamtunza kwa shida na raha ulidhani shida gani nyingine?

Ina maana we unapenda uitwe baba fulani tu lakini shida zote za mimba, mtoto mama ndio astahmili.
We naye mtaonana mtoto akikua ili utie mimba nyingine uendelee na michepuko yako.



Halafu unalalamika mtoto hakupendi anampenda mama yake atakupendaje naye mpaka anajua kuongea hakuoni kama unafanya kazi kwenye dala dala unatoka alfajiri  unarudi usiku.

Matokeo yake mapenzi ndani yanaisha yanabaki mazoea, tangu mlikuwa mnaitana honey, baby, sweetheart,darling na mengineyo majina ya mahaba mpaka mnafikia kuitana "we baba/mama fulani  ina maana hunisikii".

Kila ukiingia nyumbani kwako sura umeikunja kama unaenda vitani.  Ukija na marafiki unawatambulisha huyu ndio mama watoto, sio kipenzi mke wangu ulivyokuwa huna haya.

Ndio si mapenzi yameisha mnabaki mnalea tu watoto hata wageni wakija wanajua tofauti zenu kila mtu anamlalamikia mwenzie ndio chanzo kumbe chanzo mtoto.

Mhurumie mpenzio/mkeo anapokuwa mjamzito au analea leeni wote jamani.

BAKI NJIA KUU MICHEPUKO INAUA FAMILIA.













Toa maoni yako

Monday, February 17, 2014

Mpe raha mumeo kwa vyote

Habari za weekend wapendwa wasomaji wangu, pia za Valentine nadhani iliisha vyema kwa wale walioumizwa poleni sana,
maana kuna malalamiko nimetumiwa ya kila aina haki ya Mungu mapenzi siku hizi hakuna uuuwiiii,
wengine walizimiwa simu
wengine waliongopewa misiba, foleni, safari za ghafla duuh kwa ujumla poleni sana.
ukiona hivyo kura ya kui enjoy naye Valentine haikuwa yako subiri labda mwaka ujao kaazi kweli kweli.



Haya leo tuangazie ndoa zetu jamani 
Mke ni pambo ndani ya nyumba tena ni ua ridi linalonukia kwa kila aliye karibu nalo.
Ina maana mke unatakiwa ujipambe kwa tabia zilizo nzuri, umaridadi uvuke mipaka, huruma na mapenzi ya dhati visitengane kwa mumeo na familia yake kwa ujumla.

Hakikisha chumbani unatandika shuka kila baada ya siku mbili, fukiza udi, umepata maua ya yasmin, rose tupia ndani umekosa basi hata air fresh inayonukia vizuri pulizia ndani.
Kisha mwenyewe jipambe kwa lotion, pafyum au mafuta mazuri yenye harufu laini unajipaka wanja wako, poda bibi weye ili mradi sura iwe na mvuto akikuona uchovu wa kutwa nzima wote uishe ahisi faraja tena aone kachelewa haswaa kurudi nyumbani.

Baada ya usafi wa kina, maana wadogo zetu na wanetu siku hizi wananuka kwa bibi jamani, sijui malezi au ujuaji umewazidi?  Au ndio kuanza tiyari bado mapema? Wanaume wengi wanalalamika kwa hili, we mdada hasa unafuga au kuunga makucha mareefu unajisafisha vipi? 

Masikio machafu, mdomo tangu ulipopiga mswaki asubuhi mpaka kesho tena mmh, pua, kwapa, shingo kwenye pachi pachi zoote, nywele unaunga au unasukia nywele za bandia mwezi hadi  miwili bila kuzisafisha na joto la dar hili bichwa linanuka kama umefunika maiti ya panya,  mmmh wadada usafi wa haja unahitajika.

Kwenye mambo ya chakula cha usiku ndio kabisaaa, ujue uanamke wako hapo ndio unatakiwa uuonyeshe.
Haya ukiwa uwanjani mwenzetu ndio unalala tuu unasubiri ushikwe, uchokoze, basi hata kuinua mkono wako  ukapapasa kama kipofu washindwa heee weyee.  Ndio mwanamume huyo akitoka hapo hakutaki tena .

Lazima ujue mumeo/mpenzio anashikwa wapi akashikika, anapapaswa wapi akapapasika, anaguswa wapi akagusika hiyo ni shughuli yako mdada usidanganyike na porn ile ni biashara na sio asili yetu waafrika haswaa.   Sauti yako inatakiwa iwe nyororo yenye kudeka yenye kuchombeza kwa maneno mazuri, siyo wakati huo ndio uutumie kuomba pesa, au shida yako ulokuwa nayo, tunakosea.

ukishikwa onyesha kuhisi na akikuumiza sema hapo unaniumiza, kama unasikia raha sema ili ajue wapi akikushika unasisimkwa, sura iwe laini  macho yawe malegevu, akikutazama azidi kusisimkwa. 

Kulia hakukatazwi lakini kiwe cha kweli siyo makelele akikuangalia mwanaume macho makavu, sura umeikunja kama umelamba ndimu kelele nyiingi wizi mtupu. Hujihangaishi umetulia tuu zako kelele, hapana ule ni uwanja wa mashindano kati yenu kila mtu anatakiwa ajitume aonyeshe ujuzi jamani. Mwili wako ulainishe uunyumbuliishe kama huna mfupa, siyo unatulia kama unaombewa.

Tena mweleze kama umefika au bado hili ni tatizo la wanawake weengi sana hawafiki na wala hawafurahii tendo kwa sababu hawawi huru katika tendo yaani ili mradi atimize wajibu wake baasi.  Hapana unatakiwa kuongea na kujituma ili nawe ufike kileleni,  usipofika una hatari ya kuumwa kiuno kila mara.

Leo kama ameshinda mumeo kesho jitahidi manjonjo nawe umlize tena kwa kelele haswaaa.

Baada ya hapo kamuogeshe mumeo msinge, msafishe kwa mapenzi na huruma fyeka misitu yote abaki msafii.
Hakuna dawa zaidi ya hii tekeleza uone kama mumeo atachepuka.
Lazima abaki njia kuu.








Toa maoni yako

Friday, February 14, 2014

NDOA INA RAHA YA PEKE YAKE

                             

Jamani naomba niseme na nyie mnaojiita wapendanao miaka kumi na ushee mmekaa bila kufunga ndoa mnazaa watoto mpaka wanakwenda sekondari nyie bado mnapimana mnataka mpate futi ngapi?

Wengine mmeanza mapenzi tangu mko sekondari, chuo mpaka mmepata kazi bado hamjajuana tabia mnategemea mjuane kivipi wakati mnalala kitanda kimoja mnaamka pamoja mnashinda pamoja khaa nyie muogopeni Mungu basi duuuh.

Wengine mna pete za uchumba mpaka zimepauka ndoa haifungwi tangu mliitwa  watarajiwa mpaka watu wamewazoea.

Hebu kaeni chini mtafakari nini kimewazuia nyinyi msifunge ndoa, kama kuna kikwazo ni kipi na kinatoka kwa nani na kitaisha lini?
Kuishi bila ndoa ni sawa na wanyama kwani ndani hamna sheria hakuna anayeweza kumuwajibisha mwenzie kila mtu ana madaraka yasiyo rasmi.

kama wazazi wa upande mmoja hawataki mnafikiri wakifa ndio watakubali?

Kama tabia yake mbaya mwache atapata watakae lingana tabia unamzeesha wa nini wakati huna mpango wa kumuoa?

Wengine anakaa na mwanamke huku anatafuta mchumba taratibu akishakamisha mipango yake anasingizia wazazi wamemlazimisha kuoa, nyie wanaume wenye tabia hii muogopeni Mungu.

Wacha niwaambie ukweli,
Mapenzi ya kweli yanapatikana kwenye ndoa peke yake, humo mtapata furaha, haki, wajibu wa kila mmoja  wenu, sheria, baraka, fahari  n.k
Hata familia zenu zitakuwa na nafasi katika nyumba yenu katika shida na raha zenu.

Hakuna dini hata moja inayokubali watu waishi  bila ndoa.


                                                   


Wengine utasikia ooh tunajipanga kwanza kwani mtaishi maisha gani kuliko hayo mliyo nayo sasa,  mbona hamkusubiri kwenye ngono, mnaona sifa kujitangaza kuwa mnazini, mnataka harusi ya kifahari haijapata kutokea halafu iweje.
Hata mkienda kwenye nyumba za ibada hamuoni aibu kumkosea Mungu kwa sababu za kijinga.

Niko na wewe mdada uliyehama kwenu ukaenda kuishi na mwanaume ambaye hata hajajitambulisha kwenu, unadhani umewafurahisha wazazi wako?  hujui kama umewatia aibu familia yako wanashindwa hata pa kuweka sura zao, kila wanapopita wanachekwa kwa uliyoyafanya, haya mwenzetu  ukigombana na huyo mwanaume huwa unashtaki wapi.  Akikufukuza unarudi wapi au ndio safari ya maisha ya bila mwelekeo inaanza.

Umejirahisi sana kiukweli hata akikuoa ndoa haina msisimko kama ile ambayo ungetulia kwenu ukatoka na baraka za wazazi, vigere gere na nderemo. 

 Wazazi wakajifaharisha mbele ya jamii kuwa wanajua kulea mtoto wao katoka nyumbani na ndoa.


Bado hujachelewa rudi kwenu huyo mwanaume kama kweli anakupenda aje akuoe.

Ukiolewa unaheshimika, unaaminika, unathaminika popote pale si rahisi mtu kukufananisha na malaya wa barabarani.
Ona wivu shost  mwanaume anakuzeesha bila ndoa nawe unakubali tuu. 



Ni hayo tuu mpenda ukweli akiambiwa wala hanuni.


Toa maoni yako

Sunday, February 9, 2014

Mwanamke hulka

Habari za weekend wapendwa,
Mi kwangu ilikuwa poa sana 

Leo naomba niseme na wewe mke wa mtu




Jamani kuna wadada wengine akiwa kwenye mahusiano anakuwa na tabia nzuri, mpole, mwenye adabu, msafi, mnyenyekevu mpaka ndugu na jamaa wa mwanaume wanakubali huyu ndie mwanamke wa kuoa.

Ndoa ikifungwa Mungu wangu hata sijui binadamu wengine wameumbwaje, mi siwezi kuigiza kabisa. Ataanza kero ndani ya nyumba, mumewe na familia yake kama ipo watashika adabu.

Mara umegomba bila sababu kosa kidogo utauvuta mdomo, haueleweki kama foleni za barabarani, utadhani ulilazimishwa kuolewa.

Mumeo amerudi amechoka na kazi na vurugu za kazini badala ya kupata utulivu anaambulia maumivu,  ndio unakuta anampigia rafiki yake "ee bwana uko wapi tukutane pale basi" kumbe alikuwa hana nia ya kutoka anakimbia kero zako.
unakuta mwanaume anakonda kama anaumwa we ndio unanenepa tuu hata haya huna.

Na hakuna maneno yanayowaumiza wanaume kama haya:-

Ndio unarudi saa hizi mi sipendi kabisa kesho ukichelewa utafute mlango wa kugonga. [kesho yake asiporudi je]

Pesa unayoniachia hata haitoshi kabisa. [kama ndio uwezo wake je]

Mbona hukurudi na mkate kesho tunanywea nini chai. [we kwenda dukani huwezi]

Mi leo sitaki kupika kama vipi tukale chips. [ndivyo mlivyopanga]

Mama yako anakera nimevaa ile nguo mpya kanitazama kama nini sijui alitaka umnunulie yeye.

[angekuangalia mama yako mzazi je]

Ndugu zako wana maneno sana siwataki humu ndani au chagua kati ya ndugu zako au mimi.
[wangekuwa nduguzo je]

Jirani kanunua dish na sie tununue. [maisha ya kuiga]

Mashtaka ya watoto kama alivunja kikombe, sijui huyu alikataa kwenda wapi basi yote mambo ya kutwa nzima unamlundikia. [we huwezi kuwaonya ]


Nimepita pale mtaa wa pili yule dada akanicheka.   [kwa hiyo akapigane]
  
Ina maana hii ndio nguo umeona naweza kuvaa mie mpelekee dada yako mi siwezi kuvaa nguo kama hii.    [zawadi hiyo]

Malalamiko kila ndugu, jamaa, rafiki unamwelezea mume wangu hivi mume wangu vile. [unamtia aibu]

Kama mume anajua kupika basi magonjwa yatakuwa hayaishi kila ikifika jioni ili akirudi kazini apike.
Siri za ndani zote unaongea kwa majirani na marafiki.

Maneno ya mitaani sijui mama fulani kapigwa huyu kasutwa yanamhusu nini muda huo unatakiwa muongelee mapenzi yenu na maendeleo ya maisha yenu.

Ndio akitoka kazini akakae na marafiki mpaka usiku wa manane maana ndio wanaoweza kumpa faraja.

Jamani tuwaonee huruma watoto wa wanawake wenzetu, familia zao zinawalaumu kuwa wanatuendekeza, na sie pia tunawapa joto hasira mmh ki ukweli tubadilike.

Nyumba ndogo wakati mwingine tunazileta wenyewe mwanaume ni mtoto kila siku anapenda adekezwe, aoshwe, avishwe, sasa ukiwa mama wa kambo kwa mumeo atakuthamini vipi?  

Ushauri wangu tuwe kama panya tuume na kupuliza, unapokazana kuomba hela kazana na kumhudumia vizuri mume jamani, 
Sio madhali ndoa ya kifo kitutenganishe basi unaona hapa hakuna kuachana  lakini kumbuka furaha na amani ndani ya nyumba ikikosekana hata wewe mwenyewe utaiona ndoa chungu.  Na mwishowe kuachiwa nyumba mwanaume anaondoka na suruali zake.

Badilika ndoa sio pete ni amani na upendo ndani ya nyumba.
Tchao

Toa maoni yako

Friday, February 7, 2014

MNAOJIANDAA NA VALENTINE-NGONO MNAYAJUA HAYA?

Valentine hiyooo inakuja   wake/waume za watu roho juu, 


Watu ndio wameanza booking mapema, tena karibu asilimia 75 ni wapenzi tuu sio wa ndoa tena usikute mke wa mtu au mume wa mtu. 

Haya kuna kipya kipi wenzetu mnaenda kukifanya ambacho kitawafanya baada ya hapo mfunge ndoa?  Kabla ya hapo hamkuwa na mapenzi ya kutoka pamoja?

Au wewe mke wa mtu/mume wa mtu mapenzi gani utaenda onyesha huko wakati umeshindwa kuonyesha mapenzi hayo nyumbani kwako.

Kwanza kwa wadada, 
Kupendwa na mume/mke wa mtu ni adhabu sana kwani akipigiwa simu na mumewe/mkewe inabidi unyamaze kimya wadanganyanee I love you makiss meengi umetulia kweli? 

Pia ni mwongo mkubwa kama anamuongopea aliyemuoa mbele ya viongozi wa dini au serikali akaapa kumtunza kwa raha na shida wewe atakuambia ukweli gani? 

Na wewe kaka una mke wa mtu tena anathubutu hata kukuletea pesa unachekelea, akiachwa utamuoa kweli?  Hujiulizi kama mwanaume mwenzio anamfanyia hayo kwako wewe ndio atakuwa mke mwaminifu?

Anapigiwa simu na mumewe anadanganya na wewe unachekelea na kumuuliza anasemaje huyo bwege,
bwege wewe unaetembea na mwanamke ambaye huna future naye.

Hebu zinduka dada/kaka unaependwa na mume/mke wa mtu halafu anakudanganya anakupenda yule wala hana shida nae mbona hamwambii kwenye simu kama yuko na wewe, mbona hamwachi akawa na wewe. 

Hakuna moyo unaopenda wawili kwa wewe kaka mume wa mtu una mkeo home umekazana kuchezea mioyo ya wadada, mkeo anakupenda anakupa kila upendacho amekuzalia watoto wazuri badala ya kutunza familia yako umekazana na wadada wa mjini unawaona wazuri hujui hata aliyewafanya wawe wazuri nani.

Unaingia kichwa kichwa mpaka familia yako unaiweka katika hali mbaya, wakati hivyo unavyotunza huko nje ungemtunza mkeo angependeza kuliko na huyo mnaekutana mchana usiku hujui kalala na nani.

Valentine ina maana gani kwenu, upendo gani wa siku moja kisha kila mtu anarudi kwake.  Tena kuna wengine anapaga guest kuanzia asubuhi mpaka jioni ana wapenzi watatu mpaka wanne. Mwenyewe anajisifu kweli kweli kala valentine vizuri wakati alikuwa gari la taka umezoa kwa wote kisha unaenda kutupa kwa mkeo masikini hana hili wala lile anaambulia magonjwa.

 Tumuogope Mungu jamani kuwauwa bila sababu wake/waume zetu.

Wengine wanatongozana eti siku ya valentine wakaanze ngono jamani upendo gani sasa mnaoenda kuuonyesha na ndio kwanza mnaanza baada ya valentine mapenzi chali, kila mwaka uta valentine na mpenzi mpya.
Ushauri wangu hasa nyie wakaka tafadhalini siku hiyo mchukue mkeo mpeleke hoteli nzuri ale, anywe, ikibidi hata kulala mna show  love usiku kucha  unampoza machovu ya kukufanya uwe handsome boy mjini.

Asubuhi mnarudi home taratiiiibu hadi raha wenyewe mmeshikana mikono hata Mungu hutia Baraka ndoa yenu.
Msiokuwa couple  si lazima ungonoke show love kwa mama, dada au mtu yeyote aliye rohoni mwako basi kama huna shinda kwenye mitandao uwe una like na ku comment mpaka usiku kwani utakufa.

Ni hayo tuu wapendwa kwa wapenda ukweli 








Toa maoni yako

Thursday, February 6, 2014

MAPENZI SIO CHAKULA CHA USIKU TUU.


Leo tuongelee upande wa waume zetu.



Mwanaume nyumbani kwako ndio mahali pa faraja umetoka kuhangaika machovu ya kazini unapozea home kwa kuiona familia yako ipo salama wamekula, unapanga nao mikakati ya kesho, sio unakuwa mkali kama pili pili, mkeo na watoto wakikuona wanachanganyikiwa.

Mwanaume unaandaliwa kila kitu kuanzia mavazi, chakula, maji ya kuoga na vinginevyo, kumwambia mkeo ahsante washindwa.

Mwanaume unatoka kwenda kazini hata busu kwa mkeo hakuna, ile kumuaga tuu mwenzio shida.
Unarudi kazini ukifika nyumbani mkeo anakupokea kwa furaha na bashasha basi hata kutabasamu na kumuonyesha furaha mkeo hakuna zaidi ya kuitika kwa kichwa au mmmh. Wakati mwenzio alikuwa hana raha anawaza utarejea saa ngapi ili awe nawe.

Mnakaa sebuleni kama mtu na mkwewe kila mtu kochi lake, basi we jicho  kwenye tv tena channel unayotaka, maongezi na mkeo huna zaidi ya kumuuliza kama chakula tayari, na mnapokula kimya kama maadui hata kumsifia mkeo kama chakula kizuri inashindikana, basi kama kazidisha chumvi kidogo ndio utamgomba kama mtoto.

Ukitoka hapo unapanda kitandani kimya unamwacha mkeo kwenye wakati mgumu, hajui leo utakula chakula cha usiku ama laa.  Basi masikini mwanamke huyu baada ya kumaliza shughuli zake za kukuandalia mavazi yako viatu abrash mwenyewe atapanda kitandani kimya kimya, ole wake akutupie hata mkono unautupa “mi  nimechoka bwana”. Na hata kama ukikitaka basi hakuna maneno mazuri zaidi ya mkono kumpelekea kuwa akae tayari maana we ndio unataka.

Ndani mwenu upate muda wa kucheza na mpenzio/mkeo utani kidogo sio kila wakati we busy na simu au magazeti mkeo akikusemesha unamjibu kwa karaha.

Kama unavuta sigara ndio utapanda nazo hadi kitandani bila kujali mwenzio anaichukuliaje harufu ya sigara. 
Mkeo/mpenzio akikosea basi utamsema  chumbani ambako ni nyie wawili tuu ndio mnaokitumia, sio kumsema  mbele ya familia au  hata mbele za watu mpaka anajiona hafai kuitwa mwanadamu.
Matendo haya hata kama mkeo anakupenda namna gani hatakuwa na furaha maishani mwake, ile akikuona tu basi roho yake inamwenda mbio kama kaona simba.

Ukitoka hatamani urudi na ukirudi anaomba usiku uche ili uondoke.


Haya ndio niliyoyaona kwenye maswali ya wanawake wengi.






Toa maoni yako

Saturday, February 1, 2014

ugoya wa simba 2

 Mmh jana niliwakatiza uhondo wapendwa kwa uwezo wa Mungu leo tunaendelea ........



Haya mwana dada alipomkuta mganga kachafuka, ilibidi amwambie ajisafishe kwenye bwawa akamwazima kitenge ajifunge safari ya kurudi ikaanza.  Walipofika nyumbani mganga akamwuliza mwana dada
Tuliishia pale mganga alipopiga mweleka baada ya kumuona simba akikupuliwa manyoya ya shingo, 

Mganga:         kuanzia asubuhi mpaka jioni huwa unafanya nini kwa ajili ya mumeo? 

Mwanadada:   wafanyakazi wapo tena nimeweka wanne kwa ajili ya mume wangu 

Mganga:          siku anayorudi mumeo huwa unampokeaje?

Mwanadada:   huwa namgombeza kwa nini harudi mapema au huwa analala wapi yaani huwa nachukia                               sana kwani najitahidi kumgharamia, pesa za matumizi nampa lakini bado ananifanyia hivyo.

Mganga:          basi nitakupa hiki kitu uweke chini ya ulimi wako kisha akija mumeo useme sauti ya upole ili                          asikione kwani akikiona tu dawa itaharibika, baada ya  siku saba kisha urudi.

akampa kichangarawe kidogo sana akamwambia asikiteme labda wakati wa kula na kulala.
Mwanadada akarudi nyumbani basi akaweka kile kitu.  

Jioni mumewe aliporudi akashangaa anakaribishwa kwa sauti nzuri ya upole,  , wakati alizoea makelele majirani wote walikuwa wanazima redio. akamuuliza mkewe kama anaumwa mkewe akamjibu yuko sawa.

Mmh siku hiyo akaona maajabu kakaribishwa chakula mkewe hakubanduka mezani mpaka kamaliza kula, kapelekwa bafuni kasingwa jamani eeeh, karudishwa chumbani vizuri bila kelele.  Sasa akaanza kuwaza atatokaje maana alizoea mkewe akianza kugomba tu yeye anapata kisingizio cha kutoka eti anakimbia kelele.
Siku hiyo kelele hakuna ataondokaje?  Ikabidi awe mpole akalala asubuhi mkewe upole ndio ukazidi na ukarimu, mpaka mume akaogopa tena akaona labda anamlainisha ili amuuwe.

Zilipotimu siku saba  mwana dada akarudi kwa mganga na zawadi na pesa za kutosha huku akiwa amefurahi sana mganga kaweza kumrudisha mumewe nyumbani, mganga akamuuliza je umefanikiwa?
akajibu tena asilimia 200, basi mganga akamwambia siku akiacha masharti aliyompa mumewe ataondoka tena.

Mpendwa msomaji wangu hivi kweli ilikuwa ni dawa au matendo ya mwana dada ndiyo yalimrudisha mume nyumbani?  Jibu unalo.

MAPENZI HAYANA MGANGA

Week end njema



Toa maoni yako