Sunday, March 2, 2014

Hakuna starehe duniani kama ya mapenzi

Assalaam alaykum wapendwa wasomaji wangu,

Baada ya makavu live ya mada zilizopita naomba leo niwe msikilizaji wenu nini mnataka niongeze/nipunguze, msiniambie tu nipunguze ukali wa maneno. Maana ugonjwa hauponi bila dawa chungu.
naruhusu comment, au nenda kwenye maoni na ushauri pote nitapata utakachoniandikia, bila ya wewe mi sisongi.



Haya leo nawapa raaaha sana 

Majambozi

Jamani mkiwa kwenye majambozi jitahidini kujistiri wakati wa kushusha ule mlima hasa kwenye vyumba vya uswazi.

Maana kuna style zingine mwanamke akikupa mmh linakutoka yowe kama umeangukiwa na ukuta haaahaaa.
Msifikiri tena kuleee aku mi sitaki tafsiri zenu wabongo pale pale aliporuhusu Mungu kule kwa shetani wala mi mgeni kabisa na wala sina habari nako.

                                                     
           


Mruhusu mwanandani akushike atakapo mwache autawale mwili wako afanye atachotaka, popote kama  kupeleka ulimi we aaah ndio unazidi kunyumbulika tuu.  atapopeleka mkono kazi yako kumsapoti kwa maneno ya mahaba huku nawe mkono wako unatalii,  akaa wenyewe duniani mnakuwa peke yenu, mapenzi raahaa jamani.
Hapo hakuna anae waza umasikini, shida sijui vyote vinakaa pembeni tena hata kama mnalalia mkeka raha ndio inazidi wala haipungui.

                                            

Mwanamke style eeh, mara umebinuka kama unacheza mieleka, mara umechora pembe tatu, kisha ukamalizia na sarakasi miguu ikaja usoni mbona atakutajia jina la uji haaaahaaaa.

Sio kila siku kifo cha mende kelele kama unafukuza mwizi hayo wala si mambo babu haa maharagwe kila siku hainogi.

Mpokee taratibu huku ukimchumu na kumpa pole kwa safari nzito, mtulize kifuani mwenyewe apumue kwa raha zake huku ukimtuliza kama unabembeleza mtoto alale, mwanamke manjonjo alaaaa.

             

Mwenyewe kama muungwana utasikia ahsante mke/mpenzi wangu basi na we tena unajibu kwa mahaba mazito kiss kidogo ishara kuwa umepokea ahsante yake.



Ila hakikisha mmekula na maji ya kunywa yawe karibu,  maana mkitoka hapo njaa yake na kiu sio ya kitoto mtafunguza vibanda vya chips chezea penzi zito weye, 

Ndio ukakuta mtu kanasa kwenye urimbo watu wanasemaa  wala hashughuliki, ndugu wachukie mwanaume ndio kwanza katia pamba masikioni.
Miaka inakatika lakini nyie kila siku ndio kwanza mmeonana hakuna anayemchoka mwenzie.




hakuna dawa kwenye mapenzi, mambo ujuzi babu eeh.

Leo maneno lainiii sitaki kukera mtu miye.

Toa maoni yako

Friday, February 28, 2014

Mapenzi na Usomi haviendi


Wapendwa wasomaji wangu Assalaam alakum

Sijasema watu wasisome au wasipende na hasa sie wadada


Zamani binti alikuwa anakatishwa masomo au anakatisha mwenyewe anaamua kuolewa.  Na wengine walisoma wakapata na kazi baada ya kuolewa mume akamuachisha kazi au mwenyewe akaamua kuacha kazi.
Sio wote walikuwa wajinga hapana bali kuna wengine walizidiwa na mihemko wakaona wasiwape fedheha wazazi wao kwa kubeba mimba pasipo ndoa au kuonekana malaya mbele ya jamii.

Na wale waliokuwa wanaachishwa kazi na waume zao ama waume waliona mwenendo wao uliathiri mazingira ya ndoa zao, kwani huenda mke kazi yake ni ya kutoka jioni au usiku na akawa anashindwa kutimiza wajibu wa nyumbani kwake,  wengine walikuwa wanachepuka waume zao wakagundua.

Au mke anachoka na kazi za ofisini kiasi anashindwa kuitendea haki ndoa yake maana akishikwa kitandani wimbo wa nimechoka unakuwa mdomoni.
Sasa Mwanaume uwezo wa kumtimizia mkewe anao anaamua kumuachisha kazi ili kuinusuru ndoa yao.

Au mwanamke mwenyewe anapoona majukumu ya kazini na ya nyumbani yanamshinda na hasa anapokuwa na watoto basi mwenyewe akiona mahitaji ya nyumbani mumewe anatimiza anaona bora akae alee familia yake na ndio tukatoka watoto bora leo ambao tunajivunia malezi bora.

Kimbembe zama hizi
Wadada wengi tunajitahidi kusoma haswaa na nitoe hongera sana kwa hilo, 
Na nakubali kabisa ukimuelimisha mama umeelimisha jamii nzima.
Lakini linapokuja suala la mapenzi tunafeli sana kwanini,

Kwa sababu tunaiweka elimu ya darasani mbele kuliko elimu ya maisha, hatutaki kukaa chini tukawauliza wazee wetu kwanini wamedumu kwenye ndoa zao tunawaona washamba hawakusoma kama sie. Tunasahau wao wana elimu ya maisha ambayo huipati popote isipokuwa kwao.

Pia hatutaki kujishusha mbele ya waume zetu hatujui hata lugha ya kuongea mbele ya mpenzi wako, tena tunataka tuwe sauti ya mwisho utakalo taka lifanyike we ndio bibi mipango ndani ya nyumba mwanaume kazi yake kusema sawa.  Ndoa tutaziona kwenye muvi haki ya nani.

Ukitongozwa tu basi unaanza kumuuliza maswali 
anafanya kazi wapi
ana gari
amepanga apartment au upande mzima

Hee makubwa vinahusiana nini na mapenzi, ingekuwa hivyo masikini wasingeonja hata.
Haya ndio ana vyote unampa masharti 
mara hutaki ndugu zake, kila wiki utoke out tena unamkusanyia na marafiki, bili ya salon, simu ya million.
Unadai yote hayo wakati kupika hujui, usafi ndio kabisa kwa bibi kuchafu, kuna uvundo  na kutakosaje wakati chooni unatumia toilet paper kucha umeunga vidole vyote kwa bibi kutasafika na nini. Hata miguu yako mwenyewe akuoshe wa urembo.

Humjali mwanaume kwa lolote ila yeye akujali wewe tu, humfulii, humnyooshei nguo, humpi mapenzi matamu basi akaridhika hata kitandani, wewe na gogo la mbao hamna tofauti kazi makelele tu kama unakimbiza mwizi.
Ukiambiwa oh mi nina degreee zangu hanibabaishi mtu, aliyekwambia kitandani kunahitajika degree nani.

Tunakosa elimu ya maisha,hatuoleki, tunapata wanaume wa kutuchezea, akitaka kuoa anaenda kutafuta yule aloishia form four, au kijijini kwao anamleta mwenyewe raaaha mustarehe.

Matokeo yake tunachukua vijana wasio na kazi ya maana tunawafuga ndani nao kwa kuwa wanahudumiwa kila kitu kwao ndio.  Unamhonga naye anahonga.  

Sasa zama hizi kumkuta mdada miaka arobaini hajaolewa hata ndoa moja ni kawaida sana, lakini anajisoap soap aonekane msichana, kila birthday miaka 28, utafanyaje sasa, au ulipata wa kukuzalisha kisha yuleee anakukimbia, anabaki analea mtoto.

Usomi wako unafaa ofisini tu ndani ya nyumba we unabaki kuwa mwanamke mwenye majukumu.

Wadada wengi zama hizi tunaishi peke yetu haya ni majanga.

Kwa mwenye kupenda ukweli wala hakasiriki.

Tchaoo







Toa maoni yako

Tuesday, February 25, 2014

Nyumba ndogo Mmh

Jamani mwenzenu nashindwa kabisa kuelewa kwa nyie wanaume.



Mwanamume umeoa na mmejaaliwa watoto mashaallah,  tena huenda mmeanza maisha ya dhiki ya chumba kimoja kama stoo, maana kitanda, jiko, sturi, meza, gunia la mkaa, ndoo za maji, baiskeli kama ipo mpaka kopo la chooni na brash ya kuogea humo humo.

Anavumilia dhiki mdada wa watu nawe unamwimbia nyimbo za subira huku maharage, dagaa, mchicha, sukuma wiki, ndio mboga masikini 2000 anapanga matumizi ya siku nzima.

Mungu anawajaalia kipato mnajenga nyumba yenu, mnanunua fenicha, gari ya kutembelea, maisha yanakuwa mazuri mashaallah.
Mwanamke anaona huu ndio wakati wa yeye nae ajiringe kwenye nyumba yake baada ya kuteseka kwenye nyumba za kupanga.

Heee mwanamume ndio unaanza uesharati, nyumba ndogo, mkeo humuheshimu kila siku unarudi usiku wa manane, matumizi haba, gari anaishia kuiosha, ukiulizwa unajibu fedhuli na kumuona mshamba hafai kuitwa mkeo. 

Hivi huwa ni akili zenu, makusudi au kuzidiwa maarifa?

Unakuwa nyumbani kwako ukiingia kama kunawaka moto, mkeo na watoto wanajuta,  huna maongezi mazuri kwa mkeo wala watoto, ukirudi kazini ni kukoga na kutoka mpaka usiku wa manane.


Ole wake mkeo akuulize jambo utamtolea maneno machafu na kumuona si mwanamke tena.
Inafikia nyumba ndogo anakuja mtukana mkeo nawe unamtetea na kumgandamiza mkeo, hujui kama unawaathiri hata watoto. 
Wanashindwa kuzingatia masomo kutokana na tabia zako mbaya unazofanya mbele ya watoto.

Usifikiri watoto wote wanaofeli hawana akili wengine mazingira ya majumbani yanachangia sana kuwafelisha.
Kila siku ugomvi mara umempiga mama yao , matusi ndio usiseme, huduma mbovu, watoto mpaka wanaenda shule sare zimechanika huna habari, eeh hivi we ni mume au gume gume.




Ndio utakuta hukawii kupata matatizo kazini, mara umesimamishwa au kufukuzwa kazi unarudi unajipweteka nyumbani nyumba ndogo inakutoa mbio.

Huyo huyo ulokuwa unamtukana ndio utamtegemea masikini auze vibiashara , au alikuta labda kaweka kagenge nyumbani ndio kalishe familia.

Nyumba ndogo inaendelea kuwabamiza wengine we hata hakujui na jina keshasahau looh.

Umasikini mwingine tunauzalisha wenyewe  kisha tunamsingizia Mungu

Ni hayo tuu.






Toa maoni yako

Monday, February 24, 2014

Mwanamke kujitambua

Assalaam alaykum wapendwa wasomaji wangu,

Kwa muda sasa  nilisitisha kujibu maswali yenu si kama nimewapuuza hapana, bali najibu kupitia mada kwa baadhi ya maswali ambayo yanafanana.

Leo tuangazie kwenye ndoa huko we mdada mke wa mtu, una mumeo na watoto.

Mahitaji ya nyumba hata kama uweke ma house girl kumi bado uangalizi wako unahitajika kwa kiasi kikubwa sana.

Pia unapomweka msaidizi nyumbani unatakiwa uwe mpole mchukulie kama mdogo au mtoto wako kulingana na umri wake.  Hakikisha anafanya kazi lakini anapata muda wa kupumzika, ale chakula mnachotumia hapo nyumbani sio mnapika chakula kizuri ye anaambiwa asonge ugali tena na mboga iliyobaki sio vizuri hata Mungu hapendii

Hakikisha chakula cha mumeo unapika mwenyewe kama una nafasi ya kufanya hivyo na hasa weekend tumia muda wako vizuri kukaa na mumeo ndani mzungumze mambo ya watoto, maisha na n,k

Badilisha chakula mara kwa mara sio chakula inakuwa sheria mchana ugali usiku wali kila siku iendayo kwa Mungu hapana shost utakimbiwa.

Sasa hebu niseme na wewe mke wa mtu ambaye hutaki upitwe  harusi, kitchen, pati,send-off, kigodoro, beseni, birthday party, universary na sherehe zote za mujini we za kwako.

Mumeo hana raha nawe kila siku kuomba pesa ya sare na kumrundikia kadi za michango saa zingine hata mwenye shughuli hamjui, mmh mtaendelea kweli?


Huna muda wa kuangalia hata familia yako dada wa kazi ndio anakuwa mama mwenye nyumba ajue usafi wa nyumba, afue nguo za nyumba nzima, apike chakula, ahudumie watoto, amhudumie mumeo bado ukirudi kosa kidogo tu utamfokea na kumtishia kumfukuza kazi.  Tena inawezekana kuwa ni kabinti kadogo kamemaliza la saba huko kwao hata miaka 18 bado.

Mshahara wenyewe elf 50 haifiki na akivunja glass unamkata, jamani jiulize angekuwa mwanao jee ungefurahi?  Ndio maana wengine wanageuka nyumba ndogo.

Hee mwakwetu hujui kama maisha ya familia nzima kabeba huyu binti anaweza kutia hata sumu kwenye chakula au maji kisha akaondoka zake hamjafa bado.


mbona kuna mifano mingi sana ma house girl wameshafanya tena baadhi nimeshuhudia.

Kuna familia moja ilikuwa na dada wa kazi mwenye miaka 14, mama mwenye nyumba mkatili kupita kiasi, akirudi kazini ni kumfokea mtindo mmoja hamtumi kistaarabu. Anaamshwa saa kumi na moja alfajiri na kulala saa tano usiku kila siku.

Mle ndani walikuwa na mtoto mmoja mdogo hata nursery hajaanza basi wamekaa kama mwaka hivi mtoto akaanza kuumwa mara kwa mara, ikabidi wampime vipimo vyote akagundulika ana ukimwi wakati baba na mama hawana.
Basi Doctor akawashauri wampime na house girl wakamkuta anao aliupata kwa wazazi wake na walishafariki.

Doctor akamuuliza yule house girl alifanya nini mpaka yule mtoto akaambukizwa? akajibu alikuwa anamsafisha meno kwa kutumia mswaki wake, kwa sababu yule mama hakuwa na huruma na yeye alimfanyia ukatili kupita kiasi ndio akaamua kumwambukiza mtoto wake   naye aone uchungu.

Upo hapo we  mdada unae muona house girl hana hadhi ya kuishi duniani.

Basi na mengine mengi sana wanafanya hamjui tuu, house girl wangu nilikuwa  nikimwachia pesa anunue maji ya kunywa anajaza kwenye friji ya bombani pesa kibindoni mpaka nikamfuma hata sijui maji ya bomba nimekunywa mara ngapi.  nikamwachisha kazi  asizidi kuchezea afya yangu.

Hata watoto wetu wa sasa wanaharibika kwa kukosa uangalizi wa karibu hasa wa mama.






Toa maoni yako

Thursday, February 20, 2014

Ugomvi wa wapenzi humalizwa na mapenzi

Enyi Bibi na Bwana/mke na mume mlioamua kukaa kwa hiyari zenu kuishi pamoja kiroho safi kabisa naomba niseme nanyi leo.




Bwana kabla hujampata huyo bibie ulikuwa unahaha maneno yaliisha mdomoni sifa zote ulimpa kiasi alijiona muumba alitumia muda wa ziada katika kumtengeneza.  Akakubali mkaoana /mkaishi pamoja.

Na we bibiye kabla  hamjaishi pamoja simu zilikuwa haziishi ndugu na marafiki walichoka kusikiliza sifa za huyo bwana mpaka mkafikia kufunga ndoa/kuishi pamoja.

Maneno yanakuja hapa mmekorofishana/ mmetengana

Haa mnasahau kabisa kama ndio nyie mlokuwa mnasifiana mbele za watu mpaka wanawaonea wivu.
Mnapita barabarani mmeshikana mikono viunoni kama mapenzi mnayajua peke yenu.

Kashfa na matusi kama hamkuwahi fanyiana jema hata moja,  jamani siri za ndani zote kama mmoja wenu ana kovu, anakojoa kitandani, maumbile makubwa/madogo, yote hadharani bila haya wala soni aibu gani hii yarabi.

Wengine utakuta wameishi miaka wakifunga ndoa tuu haipiti miezi wanaachana kashfa na fedheha mitaa yote. Oh yule sio type yangu kwanza ana hiki ana kile Siri zote hadharani.  Mbona uliishi naye.

Hivi nini maana ya nyumba ikajengwa, ikawekewa milango, madirisha, makomeo na mapazia juu, kisha hata kama chumba kina vitanda vitatu bado mke na mume/bibi na bwana mkalala peke yenu humo chumbani.

Maana yake mambo yote mtakayofanya humo ndani yawe ya raha au karaha yabaki humo humo ndani.

Sasa nyie mnaokorofishana mkaita watu waje wawasuluhishe ndio mnaanza kufumuliana mambo ya chumbani mpaka mlowaita wanaona aibu hapo mnajenga au mnabomoa?  Mkisha suluhishwa kesho mnapita barabarani mnashikana mikono watu wanawabeua na kuwaona wapumbavu

Hamjiulizi hao mlowaita wenyewe hawagombani,  walishaita hata siku moja muwasuluhishe?  acheni kuwapa watu faida mpaka wanawatoa akili.

Yapo mazito kweli unaweza kuita watu wakawaamua tena mkazungumza kwa adabu bila jazba wa chuki mkasaidiwa ushauri mkamaliza maisha yakaendelea.  

Ugomvi wa wapenzi humalizwa na mapenzi,we bwana  mwenzio akinuna muombe msamaha, mletee zawadi jishushe, mbembeleze, mtupie kitandani ukimshika ndipo tu ugomvi unaisha.

Nawe bibiye ukiona umeharibu basi muombe msamaha kwa sauti nyororo na kichozi cha uchokozi, hapo ushajiremba manukato wanukia jini kasingiziwa, huku unaomba msamaha mkono upo ikulu unashusha nguo moja baada ya nyingine hachomoi utapata kigoli chako cha msamaha raaaha unakoma na kukoma hilo kosa usirudie tena.


Sio kosa umefanya na bado mdomo wa ukoo unauleta ndio makofi, ngumi, unapigwa kama mwizi, ukitoka hapo mwanaume katili, mengine tunayatafuta wenyewe.

Katika moja ya vitu ambavyo wanaume hawapendi ni kuchongolewa mdomo, labda kama umeshamfanyia ule mti wa kule kwetu "inama nikuchume."
Nao pia una expire date.

Ni hayo tu wapendwa wangu.




Toa maoni yako

Wednesday, February 19, 2014

Pipi inauzwa bei ndogo sana lakini ina maganda

Leo naomba niwaambie nyie wadada mnaojiita wa mujini mnaokwenda uchi mchana kweupeee.





Mwanamke kaumbika tena Mungu kampa vionjo vingi vya kumfanya avutie hata kama kavaa gunia.
Tena katika mazingira yoyote mwanamke bado mzuri na mrembo hata aogee sabuni ya gwanji.

Sasa nasema na wewe binti, mdada unaevaa nusu nguo ukasingizia fashion unajidhalilisha, tena unajishushia heshima yako na unajitia mikosi.  Maana mwanaume wa maana hathubutu hata kukutizama mara mbili.

Unavaa nguo ambayo ukiinama kidogo makalio yote nje, juu matiti wazi unapita mitaani watu wote wanageuka kukutazama we unaona umependeza kumbe wanakushangaa na kukuonea huruma kwani huna unachokipata zaidi ya laana.

Sijui ushamba umetuzidi wa kuiga iga maana tunachanganya nguo za kuendea disco usiku ndio tunavaa kwenda kariakoo jua la utosi .  Wengine  tunajichoresha mwili kama turbo hiyo mipaja  imetepeta kama utumbo wa taulo, miguu kama chelewa madoa kama chui kisha unavaa kimini hee mwenzetu  fashion ina watu wake bibie muwe mnajitazama kwanza kabla hamjatoka loooh.

Usoni ndio umejipara  ma eye color, lipstick ng'ari ng'ari   unakuwa kama shetani basi ukipigiwa miluzi njiani roho kwatuuu unaona wameuona uzuri wako, kumbe wenzio wanakuona hamnazo.

 Kuna Mchungaji mmoja alisema 
"mdada ukiona unatongozwa sana si kwamba wewe ni mzuri bali una pepo la ngono".

Wacha nikupe shost,

Ndoa utazisikia na kuziona kwenye chereko chereko na ikitokea umeolewa hukai, huyo mwanaume alokupenda before unatembea uchi hatataka akikuweka ndani uendelee kutangaza maumbile yako, atataka uvae kiheshima ili usiendelee kumuanikia starehe yake, na wewe ndio nguo za kuvaa mwanamke timamu zinakuwasha kama alivyokuwa akisema msanii mmoja [jina kapuni] yalipomfika hadi hijabu kichwani alivaa.
Ndoa mwezi mmoja miwili chaliii.

Hao wanaopanga foleni kwa wewe kutembea uchi wanakutamani tu wakitaka kuoa wanaenda kutafuta wale wanaova sawa sawa kwani wanaona ndio wanawake waliokamilika, tena wanakuwa na hamu nao sana waone kilicho jificha ndani.

Ndio maana siku hizi mabinti warembo tena wanajitahidi mashaallah kujiremba, kwenye pochi vimejaa vipodozi kila akiona choo cha kulipia anaingia kuongeza make up na lipstik, basi kila kona ya jiji wanazurura masikini kila anae waita anaishia kuwachezea na kuwaacha.  

Mpaka sasa kumezuka kupiga picha za uchi kabisa unaweka kwenye mitandao,  halafu mtu anasema anatafuta mume, aje wapi anachokihitaji ushakianika mbele ya hadhira.

Tunasababisha wanaume siku hizi ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume umekuwa janga kwa sababu kutwa anaona mapaja, makalio na mwili wote wa mwanamke u wazi anaishia kujifinya suruali hata akirudi home kishajipigia mabao tele bila mechi.  kwa mkewe anaishia bao moja hoi, ugomvi unazuka kumbe masikini wala hakuchepuka bali hiyo michepuko ipo kila kona kama matangazo.

Tunatakiwa tujipambe sawa lakini kuna mahala pake, sio barabarani mitaa yote unakutana na watoto, wazee kuliko wazazi wako basi wote wakuone maungo yako hapana shost badilika. 


Hebu itazame pipi inauzwa bei ndogo sana sh. hamsini hadi mia lakini hawaiachi hivi hivi lazima waifunike, ina maana pipi ina thamani kuliko wewe.

Heshima ni kitu cha bure lakini ikiondoka kuirudisha ni kazi ngumu sana.

Mwanamke mpumbavu huharibu heshima yake kwa mikono yake mwenyewe.








Toa maoni yako

Tuesday, February 18, 2014

Mimba si ugonjwa mpende mkeo

Assalaam alaykum wapendwa wasomaji wangu,

Leo naomba niseme na wewe mume au mwanaume umeishi na mkeo/mpenzio na kwa makubaliano mazuri kabisa mkaamua mpate mtoto.



Kazi inaanzia hapo,  karaha za mimba kila mtu anazijua kuanzia ikiwa changa mpaka kujifungua.

Mkeo hali chakula kizuri, anachagua vyakula, mara katapika, halali usingizi mzuri, anakasirika bila sababu, anaweza kumchukia mtu bila kisa au akakupenda wewe mumewe mpaka akawa anakaa na shati lako chafu akinusa mwenyewe anajisikia raaaha mustarehe.  Au akakuchukia mpaka ukatamani kuhama nyumba.

Hayo yote mume inabidi uyavumilie ni ya muda, akijifungua yataisha.

Basi inatakiwa urudi nyumbani mapema ili umliwaze kwa maneno mazuri, msaidie anapokuwa anahitaji msaada, mtoe out siku moja moja ili aliwazike. 

Maana kubeba roho mbili jamani kazi hivyo, msione wengine wanazitoa mimba mkaona makatili, sometime na nyie huwa sababu unapunguza mapenzi ndani, karaha mtindo mmoja,  unamuona mkeo anatapika unachukia na kukunja uso kama kafanya kusudi unashika njia yulee asiitoe kwanini maana anaona inamnyima raha, inampotezea mume.

Haya mtoto akizaliwa mnatakiwa mshirikiane katika kumlea, umerudi umemkuta amejisaidia mtoe pampas mvike nyingine, analia msaidie mkeo kumbembeleza toka nae utembee nae kidogo huenda mkeo  ana kazi jikoni, ikibidi muogeshe, cheza naye ili mkeo naye apumzike.

Lakini kinyume ndio kwanza unatafuta mchepuko wako mwenyewe, unajipoooza hukooo unarudi saa nane za usiku unamgongea huna hata huruma mwenzio kashinda na madhila yote hayo bado huenda ndio kwanza kapata usingizi unamtia karaha nyingine.

Mlipo oana ukaapa utamtunza kwa shida na raha ulidhani shida gani nyingine?

Ina maana we unapenda uitwe baba fulani tu lakini shida zote za mimba, mtoto mama ndio astahmili.
We naye mtaonana mtoto akikua ili utie mimba nyingine uendelee na michepuko yako.



Halafu unalalamika mtoto hakupendi anampenda mama yake atakupendaje naye mpaka anajua kuongea hakuoni kama unafanya kazi kwenye dala dala unatoka alfajiri  unarudi usiku.

Matokeo yake mapenzi ndani yanaisha yanabaki mazoea, tangu mlikuwa mnaitana honey, baby, sweetheart,darling na mengineyo majina ya mahaba mpaka mnafikia kuitana "we baba/mama fulani  ina maana hunisikii".

Kila ukiingia nyumbani kwako sura umeikunja kama unaenda vitani.  Ukija na marafiki unawatambulisha huyu ndio mama watoto, sio kipenzi mke wangu ulivyokuwa huna haya.

Ndio si mapenzi yameisha mnabaki mnalea tu watoto hata wageni wakija wanajua tofauti zenu kila mtu anamlalamikia mwenzie ndio chanzo kumbe chanzo mtoto.

Mhurumie mpenzio/mkeo anapokuwa mjamzito au analea leeni wote jamani.

BAKI NJIA KUU MICHEPUKO INAUA FAMILIA.













Toa maoni yako