Leo naomba niwaambie nyie wadada mnaojiita wa mujini mnaokwenda uchi mchana kweupeee.
Mwanamke kaumbika tena Mungu kampa vionjo vingi vya kumfanya avutie hata kama kavaa gunia.
Tena katika mazingira yoyote mwanamke bado mzuri na mrembo hata aogee sabuni ya gwanji.
Sasa nasema na wewe binti, mdada unaevaa nusu nguo ukasingizia fashion unajidhalilisha, tena unajishushia heshima yako na unajitia mikosi. Maana mwanaume wa maana hathubutu hata kukutizama mara mbili.
Unavaa nguo ambayo ukiinama kidogo makalio yote nje, juu matiti wazi unapita mitaani watu wote wanageuka kukutazama we unaona umependeza kumbe wanakushangaa na kukuonea huruma kwani huna unachokipata zaidi ya laana.
Sijui ushamba umetuzidi wa kuiga iga maana tunachanganya nguo za kuendea disco usiku ndio tunavaa kwenda kariakoo jua la utosi . Wengine tunajichoresha mwili kama turbo hiyo mipaja imetepeta kama utumbo wa taulo, miguu kama chelewa madoa kama chui kisha unavaa kimini hee mwenzetu fashion ina watu wake bibie muwe mnajitazama kwanza kabla hamjatoka loooh.
Usoni ndio umejipara ma eye color, lipstick ng'ari ng'ari unakuwa kama shetani basi ukipigiwa miluzi njiani roho kwatuuu unaona wameuona uzuri wako, kumbe wenzio wanakuona hamnazo.
Kuna Mchungaji mmoja alisema
"mdada ukiona unatongozwa sana si kwamba wewe ni mzuri bali una pepo la ngono".
Wacha nikupe shost,
Ndoa utazisikia na kuziona kwenye chereko chereko na ikitokea umeolewa hukai, huyo mwanaume alokupenda before unatembea uchi hatataka akikuweka ndani uendelee kutangaza maumbile yako, atataka uvae kiheshima ili usiendelee kumuanikia starehe yake, na wewe ndio nguo za kuvaa mwanamke timamu zinakuwasha kama alivyokuwa akisema msanii mmoja [jina kapuni] yalipomfika hadi hijabu kichwani alivaa.
Ndoa mwezi mmoja miwili chaliii.
Hao wanaopanga foleni kwa wewe kutembea uchi wanakutamani tu wakitaka kuoa wanaenda kutafuta wale wanaova sawa sawa kwani wanaona ndio wanawake waliokamilika, tena wanakuwa na hamu nao sana waone kilicho jificha ndani.
Ndio maana siku hizi mabinti warembo tena wanajitahidi mashaallah kujiremba, kwenye pochi vimejaa vipodozi kila akiona choo cha kulipia anaingia kuongeza make up na lipstik, basi kila kona ya jiji wanazurura masikini kila anae waita anaishia kuwachezea na kuwaacha.
Mpaka sasa kumezuka kupiga picha za uchi kabisa unaweka kwenye mitandao, halafu mtu anasema anatafuta mume, aje wapi anachokihitaji ushakianika mbele ya hadhira.
Tunasababisha wanaume siku hizi ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume umekuwa janga kwa sababu kutwa anaona mapaja, makalio na mwili wote wa mwanamke u wazi anaishia kujifinya suruali hata akirudi home kishajipigia mabao tele bila mechi. kwa mkewe anaishia bao moja hoi, ugomvi unazuka kumbe masikini wala hakuchepuka bali hiyo michepuko ipo kila kona kama matangazo.
Tunatakiwa tujipambe sawa lakini kuna mahala pake, sio barabarani mitaa yote unakutana na watoto, wazee kuliko wazazi wako basi wote wakuone maungo yako hapana shost badilika.
Hebu itazame pipi inauzwa bei ndogo sana sh. hamsini hadi mia lakini hawaiachi hivi hivi lazima waifunike, ina maana pipi ina thamani kuliko wewe.
Heshima ni kitu cha bure lakini ikiondoka kuirudisha ni kazi ngumu sana.
Mwanamke mpumbavu huharibu heshima yake kwa mikono yake mwenyewe.
Toa maoni yako
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako