Monday, February 24, 2014

Mwanamke kujitambua

Assalaam alaykum wapendwa wasomaji wangu,

Kwa muda sasa  nilisitisha kujibu maswali yenu si kama nimewapuuza hapana, bali najibu kupitia mada kwa baadhi ya maswali ambayo yanafanana.

Leo tuangazie kwenye ndoa huko we mdada mke wa mtu, una mumeo na watoto.

Mahitaji ya nyumba hata kama uweke ma house girl kumi bado uangalizi wako unahitajika kwa kiasi kikubwa sana.

Pia unapomweka msaidizi nyumbani unatakiwa uwe mpole mchukulie kama mdogo au mtoto wako kulingana na umri wake.  Hakikisha anafanya kazi lakini anapata muda wa kupumzika, ale chakula mnachotumia hapo nyumbani sio mnapika chakula kizuri ye anaambiwa asonge ugali tena na mboga iliyobaki sio vizuri hata Mungu hapendii

Hakikisha chakula cha mumeo unapika mwenyewe kama una nafasi ya kufanya hivyo na hasa weekend tumia muda wako vizuri kukaa na mumeo ndani mzungumze mambo ya watoto, maisha na n,k

Badilisha chakula mara kwa mara sio chakula inakuwa sheria mchana ugali usiku wali kila siku iendayo kwa Mungu hapana shost utakimbiwa.

Sasa hebu niseme na wewe mke wa mtu ambaye hutaki upitwe  harusi, kitchen, pati,send-off, kigodoro, beseni, birthday party, universary na sherehe zote za mujini we za kwako.

Mumeo hana raha nawe kila siku kuomba pesa ya sare na kumrundikia kadi za michango saa zingine hata mwenye shughuli hamjui, mmh mtaendelea kweli?


Huna muda wa kuangalia hata familia yako dada wa kazi ndio anakuwa mama mwenye nyumba ajue usafi wa nyumba, afue nguo za nyumba nzima, apike chakula, ahudumie watoto, amhudumie mumeo bado ukirudi kosa kidogo tu utamfokea na kumtishia kumfukuza kazi.  Tena inawezekana kuwa ni kabinti kadogo kamemaliza la saba huko kwao hata miaka 18 bado.

Mshahara wenyewe elf 50 haifiki na akivunja glass unamkata, jamani jiulize angekuwa mwanao jee ungefurahi?  Ndio maana wengine wanageuka nyumba ndogo.

Hee mwakwetu hujui kama maisha ya familia nzima kabeba huyu binti anaweza kutia hata sumu kwenye chakula au maji kisha akaondoka zake hamjafa bado.


mbona kuna mifano mingi sana ma house girl wameshafanya tena baadhi nimeshuhudia.

Kuna familia moja ilikuwa na dada wa kazi mwenye miaka 14, mama mwenye nyumba mkatili kupita kiasi, akirudi kazini ni kumfokea mtindo mmoja hamtumi kistaarabu. Anaamshwa saa kumi na moja alfajiri na kulala saa tano usiku kila siku.

Mle ndani walikuwa na mtoto mmoja mdogo hata nursery hajaanza basi wamekaa kama mwaka hivi mtoto akaanza kuumwa mara kwa mara, ikabidi wampime vipimo vyote akagundulika ana ukimwi wakati baba na mama hawana.
Basi Doctor akawashauri wampime na house girl wakamkuta anao aliupata kwa wazazi wake na walishafariki.

Doctor akamuuliza yule house girl alifanya nini mpaka yule mtoto akaambukizwa? akajibu alikuwa anamsafisha meno kwa kutumia mswaki wake, kwa sababu yule mama hakuwa na huruma na yeye alimfanyia ukatili kupita kiasi ndio akaamua kumwambukiza mtoto wake   naye aone uchungu.

Upo hapo we  mdada unae muona house girl hana hadhi ya kuishi duniani.

Basi na mengine mengi sana wanafanya hamjui tuu, house girl wangu nilikuwa  nikimwachia pesa anunue maji ya kunywa anajaza kwenye friji ya bombani pesa kibindoni mpaka nikamfuma hata sijui maji ya bomba nimekunywa mara ngapi.  nikamwachisha kazi  asizidi kuchezea afya yangu.

Hata watoto wetu wa sasa wanaharibika kwa kukosa uangalizi wa karibu hasa wa mama.






Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako