Thursday, February 20, 2014

Ugomvi wa wapenzi humalizwa na mapenzi

Enyi Bibi na Bwana/mke na mume mlioamua kukaa kwa hiyari zenu kuishi pamoja kiroho safi kabisa naomba niseme nanyi leo.




Bwana kabla hujampata huyo bibie ulikuwa unahaha maneno yaliisha mdomoni sifa zote ulimpa kiasi alijiona muumba alitumia muda wa ziada katika kumtengeneza.  Akakubali mkaoana /mkaishi pamoja.

Na we bibiye kabla  hamjaishi pamoja simu zilikuwa haziishi ndugu na marafiki walichoka kusikiliza sifa za huyo bwana mpaka mkafikia kufunga ndoa/kuishi pamoja.

Maneno yanakuja hapa mmekorofishana/ mmetengana

Haa mnasahau kabisa kama ndio nyie mlokuwa mnasifiana mbele za watu mpaka wanawaonea wivu.
Mnapita barabarani mmeshikana mikono viunoni kama mapenzi mnayajua peke yenu.

Kashfa na matusi kama hamkuwahi fanyiana jema hata moja,  jamani siri za ndani zote kama mmoja wenu ana kovu, anakojoa kitandani, maumbile makubwa/madogo, yote hadharani bila haya wala soni aibu gani hii yarabi.

Wengine utakuta wameishi miaka wakifunga ndoa tuu haipiti miezi wanaachana kashfa na fedheha mitaa yote. Oh yule sio type yangu kwanza ana hiki ana kile Siri zote hadharani.  Mbona uliishi naye.

Hivi nini maana ya nyumba ikajengwa, ikawekewa milango, madirisha, makomeo na mapazia juu, kisha hata kama chumba kina vitanda vitatu bado mke na mume/bibi na bwana mkalala peke yenu humo chumbani.

Maana yake mambo yote mtakayofanya humo ndani yawe ya raha au karaha yabaki humo humo ndani.

Sasa nyie mnaokorofishana mkaita watu waje wawasuluhishe ndio mnaanza kufumuliana mambo ya chumbani mpaka mlowaita wanaona aibu hapo mnajenga au mnabomoa?  Mkisha suluhishwa kesho mnapita barabarani mnashikana mikono watu wanawabeua na kuwaona wapumbavu

Hamjiulizi hao mlowaita wenyewe hawagombani,  walishaita hata siku moja muwasuluhishe?  acheni kuwapa watu faida mpaka wanawatoa akili.

Yapo mazito kweli unaweza kuita watu wakawaamua tena mkazungumza kwa adabu bila jazba wa chuki mkasaidiwa ushauri mkamaliza maisha yakaendelea.  

Ugomvi wa wapenzi humalizwa na mapenzi,we bwana  mwenzio akinuna muombe msamaha, mletee zawadi jishushe, mbembeleze, mtupie kitandani ukimshika ndipo tu ugomvi unaisha.

Nawe bibiye ukiona umeharibu basi muombe msamaha kwa sauti nyororo na kichozi cha uchokozi, hapo ushajiremba manukato wanukia jini kasingiziwa, huku unaomba msamaha mkono upo ikulu unashusha nguo moja baada ya nyingine hachomoi utapata kigoli chako cha msamaha raaaha unakoma na kukoma hilo kosa usirudie tena.


Sio kosa umefanya na bado mdomo wa ukoo unauleta ndio makofi, ngumi, unapigwa kama mwizi, ukitoka hapo mwanaume katili, mengine tunayatafuta wenyewe.

Katika moja ya vitu ambavyo wanaume hawapendi ni kuchongolewa mdomo, labda kama umeshamfanyia ule mti wa kule kwetu "inama nikuchume."
Nao pia una expire date.

Ni hayo tu wapendwa wangu.




Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako