Friday, January 31, 2014

Ugoya wa simba

Hebu tupumzike na maswali tupate simulizi nzuuri sana ya mapenzi




Kulikuwa na mwana dada mmoja aliolewa kwa ndoa ya kifahari sana, pia alikuwa tajiri kama malkia wa nyuki.  Basi pamoja na utajiri wake wote lakini hakuwa na furaha kwenye ndoa yake, yaani mume siku zingine anarudi usiku wa manane mara nyingine alale huko huko. 
Mwana dada akaona makubwa haya akaenda kwa mganga kutafuta dawa ya kumtuliza mumewe, alipofika kwa mganga na kumuelezea shida yake mganga akamwambia tatizo lake ni kubwa mno linahitaji apate ngoya za simba zile za shingoni. akasema hakuna shida ili mradi tuu mumewe atulie nyumbani.

Siku iliyofuata akachinja mbuzi akabeba miguu na mikono akaenda porini kumtafuta simba, akafika sehemu kuna bwawa la maji pembeni kuna mti mkubwa.  Basi akapanda juu ya mti akachukua kamba akafunga ile miguu na mikono ya mbuzi kila moja na kamba yake alafu akaining'iniza chini simba alipopita kwenda kunywa maji akadaka ile miguu na mikono akala kisha akaenda kunywa maji. 
baada ya hapo yule mwanamke akashuka akaenda nyumbani, kesho yake akafanya vile vile huku nae akishuka kwenye tawi la chini, baada ya wiki moja simba akazoea kupitia pale na Mwana dada nae woga ukapungua akashuka mpaka tawi la chini kabisa siku hiyo ile anampa tu akamvuta manyoya ya shingoni simba akatoka mbio na mwana dada nae moja kwa moja mpaka kwa mganga.

Alipofika mganga alishtuka akamuuliza amenunua wapi mwana dada akamwambia ameyachomoa mwenyewe shingoni kwa simba.  Mganga hakuamini akamwambia itabidi kesho akamwonyeshe alivyoyachukua.  Basi siku ya pili mwana dada akampitia mganga wakaenda mpaka kule porini, mwanadada akamwambia mganga ajifiche pembeni ya bwawa kulikuwa na kichaka fulani hivi.

Muda wa simba ukafika akapita pale kula nyama, mwana dada naye kama kawaida yake ile anakula tu akamkupua manyoya ya shingoni  simba akatoka mbio, na mganga kule naye mweleka haja zote zikamtoka, mwana dada kumpitia akamkuta kajichafua vibaya sana.

Nini kiliendelea tukutane kesho 



Toa maoni yako

Thursday, January 30, 2014

USALITI NI MSUMARI WA MOTO


Nimepata maswali ya wasomaji weengi zaidi ya 20 wanalalamika kuhusu usaliti wa wapenzi wao naomba niwajibu kwa pamoja ili nipunguze foleni ya maswali yenu:


Kwanza kama ulisoma mada yangu ya TALK ABOUT LOVE yote utapata majibu mazuri zaidi lakini naomba nijibu tena.

Suala la mume/mke/mpenzi wako kukusaliti inatokana na mambo mengi sana haya ni baadhi tu:

Anakupenda kweli?
Maana huenda alikupenda ajili ya kitu fulani mfano mwanaume alikupenda ulikuwa na sura nzuri, umbo namba 8 sasa umejiachia kunenepa mpaka hata alivyokupendea vimetoweka, au ajali masikini umepoteza kiungo au sura imeharibika.
Kwa mwanamke huenda ulikuwa na mali, Umaarufu au umbo zuri baadaye vikatoweka.
Anayekupenda kweli hakusaliti hata ufikwe na majanga gani.


  • Kauli mbovu
Kwa mpenzio huuwa mapenzi yote yaani anakuambia vizuri utamjibu majibu ya karaha kama adui yako, tena kwa wote maana kuna wanaume pia wana midomo michafu akikupa moja unakumbuka kwenu.
  • Chakula cha usiku 
Tena hii ni sababu kubwa kuliko zote mwanaume asipopata hiyo kitu usaliti unauita peupee na ujue akisaliti mara moja ananogewa kujirudi sio rahisi.
 Kwa mwanamke ukiona mumeo anakunyima muulize vizuri kama hujamkosea jua kuna mwenzio anamchosha maana huwa hawawezi kuvumilia bila hiyo kitu.
  • Makaribisho mabovu 
Yaani ukimuona mumeo unakuwa kama umeona gari ya taka, unakunja na sura karibu inatokea kisogoni, akipata makaribisho mazuri hakumbuki hata shati.
  • Usafi/umaridadi
Mumeo anarudi kazini anakukuta mchafu  make up au nguo nzuri unavaa ukiwa na mwaliko, 
Au we dada unaefanya kazi ukianza kwenda kazini unajipara kweli kweli, ukirudi unatafuta kanguo hakana hata sura ndio unavaa we unadhani mumeo anaona waliojipara wangapi huko nje. Na hizo nguo na vipodozi alivyonunua aishie kuona unajipara wakati unatoka inaingia akilini kweli.

Pia usafi wa kwa bibi jamani tuseme ukweli kuna wadada wengine wananuka sana, kwa sababu hawapendi kutumia maji kujisafisha, mwanamke maji ndio kila kitu, pia usisahau mwanamke ana miswaki miwili, kujipara usoni hakuna maana kama hujisafishi vizuri, hamu yote humuisha mwanaume akikuta kwa bibi kuna uvundo shost, atakupa mgongo kama hakujui.
  • Matumizi 
Yanazidi kipato kila uonacho mwanamke roho inakusimama, mumeo akisema hana pesa unauvuta mdomo, akimpata anae mhurumia umelia.

Na nyie wanaume mabahili,  mkeo hajui mapato yako, humpi chakula kizuri, mavazi anayaona yanang'aa kwenye maduka, kila siku unamwimbia wimbo wa subira, dagaa lake mchicha ndio kabisa kila siku, pesa ya matumizi unampa kila siku haitoshi hata mlo wa siku, mwanamke hana hata akiba kidogo haaa weee akimpata anayempa elf kumi tu atakusaliti lazima.
  • Ugomvi wa kila mara  
Yaani hamkai pamoja lazima majirani wazime radio kuwasikiliza mnavyogombana, hata mnachogombania hakina kichwa wala miguu, mmoja wenu akiwa hayupo cm kutwa uko wapi, unarudi saa ngapi maswali meengi kama mnapendana vile.
Ndio unakuta mwanaume akitoka kazini anakaa kwanza mahali mpaka saa nne za usiku ndio unarudi na kusingizia foleni, lakini ukweli  haoni faida ya kurudi home mapema atamaliza siku vibaya. akimpata wa kumpa raha na sio karaha zako atasahau hadi jina lako.

Jamani usaliti unaumiza sana kama msumari wa moto kwenye kidonda
 Tafadhali usimsaliti mwenzio 






Toa maoni yako

Tuesday, January 28, 2014

I love you za Facebook



Amina wa Kibaha 
Dada naomba kuuliza hivi nani alileta hii mitandao ya kijamii?
Jamani ndoa yangu inang'inia mume wangu kutwa anachat na wanawake, simu ndio usiseme hatuna muda hata wa kujadili hata mambo ya familia yetu.
Tena toka ameanza mambo ya mitandao amekuwa anaomba mapenzi haramu mi siwezi basi ananuna, nikawa najiuliza mbona zamani hakuwa na mambo haya, juzi nilichungulia kwenye laptop yake mmh nilichokiona dada mavideo ya ngono  kajaza humo, 
Natamani niondoke lakini watoto wangu bado wadogo sijui hata nifanyeje ndoa yangu naipenda ina miaka sita tuu.

JIBU
Pole sana mdogo wangu,
Mbona wengi tunatumia mitandao na ndoa zetu zipo salama salimini.

Huo ni ulimbukeni wa teknolojia mwanaume weye na wala aliyeleta hakukwambia ubebe taka zote upeleke nyumbani kwako hayo maporn unayo angalia wenzio wapo kazini wanalipwa, wanakunywa madawa,  wana madaktari wao wanapimwa afya na kila kitu we ukamfanyie mkeo  hata aibu huna.

Kwanza wana mapenzi gani kuzidi yetu ya kibantu khaa uchafu mtupu,  kinachokufanya uvunje ndoa yako nini, hao unaowaona wazuri  kwenye mtandao ni make up tuu hebu kawatembelee asubuhi uwakute ndio wanaamka kama hujatapika. Hata mkeo ukimnunulia anaweza kuwashinda hao wanao kuzuzua. Hivi hujiulizi kutwa nzima wanachat na wangapi, wangapi wanaambiwa love you kama wewe, acha umburulaaa.

Mdogo wangu usiondoke pigania ndoa yako usidhani hao wanaomzuzua ni wakaaji, wao ni wabomoaji tuu utatesa watoto wako bure shost hayo magume gume yaloshindikana na mitume yasikutishe, tena jiamini wewe ndio mwenyewe wengine wote wezi.

Pia usikubali kabisa huko anako kuomba tena uwe macho maana wanajifanyaga wamepotea njia, mwache anune kama ana uwezo akumeze kabisa ukae tumboni mwake.  Atakuharibu utembee na nzi kama unauza utumbo, kisha akubwage mchana kweupee.  Jali wanao mwaya watapata shida malezi yao yanategemea umoja wenu, akizidi mpeleke kwa viongozi wa dini. 






Toa maoni yako

Monday, January 27, 2014

Nyumba ndogo


                                          

Habari za weekend wapendwa, natumaini ilikuwa poa.
Leo nitaendelea na maswali yenu yako mengi sana nadhani mengine tutayajibu baada ya mada ijayo.

Saimon wa Kenya
Habari yako  dada mi  nina miaka 30 nimeoa, ni bibi na  tuna mtoto mmoja, simuelewi mke wangu huwa anamaanisha nini kulaza mtoto katikati yetu pia hata kama mmekaa pamoja ye hana mapenzi tena na mimi bali na mtoto sasa dada nikitafuta mpango wa kando nitakosea?

JIBU
Utakosea sana kaka Saimon, mwanaume anayejiamini hutafuta suluhu ndani ya nyumba yake, huyo nyumba ndogo atakusaidia mapenzi yarudi ndani au atazidi kubomoa.  
Na ukiamua hivyo ina maana utawatenga mama na mtoto, na nyumba ndogo zilivyo mbona utasahau kama umeoa.  Kisha huyo nyumba ndogo unajuaje kama atakuwa mwaminifu kwako? 

Ndio mwanzo wa kubeba magonjwa na kuleta nyumbani, tafadhali tulia na mkeo hayo ni mambo ya mpito, kwani mwanamke akiwa mja mzito huwa katika hali ya kuathirika kisaikolojia na ndio maana huweza muona akinuna bila sababu, wengine hulia, kuchagua vyakula au nguo, kuchukia watu wa jinsia fulani bila sababu.

Sasa hali hiyo wengine huendelea mpaka anapokuwa na mtoto hupenda kuongea au kucheza na mtoto muda wote namaanisha mapenzi yote ya baba yanahamia kwa mtoto, anasahau kuwa sasa ana watoto wawili mtoto mkubwa (Mume) na mtoto mdogo.
Pia msaidie unapopata nafasi kucheza na mtoto kila umuonapo anacheza naye, akiona hivyo atafurahi kuona unamsapoti kwa anachokipenda naye  atarudisha mapenzi kwako.
   
Ok bye



Toa maoni yako

Saturday, January 25, 2014

Mapenzi ndoa - i love you kelele tuu







Halima wa Dar

Shikamoo Dada mi ninauliza hivi
Nina bwana ninaishi naye mwaka wa 5 sasa kila nikimwambia kuhusu ndoa anakuwa mkali na kuniuliza kwani nimepungukiwa nini, 
nami ninaamini tukifunga ndoa itanipa kujiamini pia kuishi hivi tunamkosea Mungu nifanyeje dada?

JIBU
Mmh jamani naomba usikwazike kwa majibu yangu,
Kosa la kwanza ni  kitendo cha wewe kwenda kuishi na mwanaume bila mwanaume kukamilisha taratibu,
umejirahisi kupita kiasi my dear, tena hata familia yako sina uhakika kama ilifurahia, kwani furaha ya wazazi ni kuona binti yao anafuata maadili .   Hee inakuwaje kwani utoke kwenu kwenda kuishi na mwanaume hivi hivi duuh kiasi yakukute. 







Kwa mila za kiafrika sijui mabara mengine ni mwanaume ndio anaesumbuka ili kukupata.  Sasa we ulipojippeleka ukamrahisishia kazi ndio maana haoni umuhimu wa ndoa, japo ni muhimu sana katika kujenga familia bora na kuanzisha ukoo.

Pili mwanzo wakati unaenda kuishi naye hukujua kuwa ni dhambi sasa baada ya kuona ndoa inaota mbawa umemkumbuka na Mungu, ni vizuri kumkumbuka Mungu kabla hujafanya jambo lako lolote.

Kisha hawa wanaume wengi wanatuliza machozi  kwa kuwa hatuwajui, mwanzo huwa wana act kuwa wanapenda kisha anaanza kukusoma taratibu tabia na mwenendo wako akiona unamridhisha basi huuachia moyo wake katika penzi,  laa akiona kuna mambo hayamridhishi baasi ataanza kukuepuka taratibu. 

 Sasa wewe uliejipeleka sina uhakika kama ameshindwa tabia yako au kakuona wa kawaida.  Lakini kaa naye muulize taratibu nini hatma ya uwili wenu atakachokujibu basi patana nacho.



 Jamani mwanaume anayekupenda atakuja kwenu atajitambulisha na kutoa mahari kisha mnaoana.  

NIWATAKIE WEEK END NJEMA





Toa maoni yako

Friday, January 24, 2014

MAANA YA MWANAMKE



Sam wa Dar

Dada mi nina tatizo naomba usipendelee kwa kuwa mwanamke mwenzio,
mke wangu hapendi kupika wala kazi za nyumbani kila kitu anafanya housemaid, hata kama usawa wenyewe basi unashindwa hatakutandika ndani mwako, ukimwelekeza ana mdomo mchafu balaa.  Naomba unisaidie bahati nzuri na humu kwenye blog yako anaingia 


JIBU

Mmmh aibu ulimtoa wapi au ndio mlikutana baa ukaona anafaa, 
Wahenga wanasema ni bora ukosee kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa.

Haya nawe mwanamke mwenzetu ulilelewa mbinguni au chini ya bahari? Mwanamke kutokujua kupika shost majanga tena  tukushushie bendera nusu mlingoti, we ni wa kike sio mwanamke, mwanamke hawezi kuwa hajui kupika, na kitanda utandikiwe khaaaa.

Nyie ndio mnaosababisha wasaidizi wanabakwa/wanabebeshwa mimba na waume zenu kisha mnawafukuza kwa taadhira, wanaenda makwao kuongeza mzigo wa umasikini, kumbe kosa lako mwenyewe.

Fahari ya mwanamke ndani ya nyumba usafi uujue, chakula cha mumeo bibi weye, chumbani  kwako ndio kabisa huyo maid hatakiwi hata kuchungulia, ukiambiwa mdomo na ndivyo walivyo wavivu wote mdomo silaha, waongo, chochote kwao sawa tuu,  kazi ni kuunga kucha na kuzitia kila aina ya  rangi sijui hata usafi wa maungo yao wanaufanyaje.

Kila siku unazusha safari ili usikae jikoni, saluni zote wanakufahamu aliyekwambia mwanaume anakula urembo nani, mapenzi sio kitandani tuu bali umjue mwanaume kula yake, vaa yake, apendavyo ufanye na anachokukataza acha, pia uwe mbunifu basi ndani ya nyumba kila mara unatakiwa um surprise mumeo kwa upambaji wa nyumba yenu. Badilika my dear maisha si lelemama hapo ulipo kuna wenzio wamepanga msitari  wanakusubiri utoke waingie.

Asikudanye mtu maisha ya ndoa yana heshima kwako na nyumbani kwenu.  Kama hufahamu kuwa mpole tafuta mtu japo umlipe akufundishe wajibu wa mwanamke  vinginevyo utawahesabu wanaume kama nguo.

Kila kitu msaidizi siku ukimkuta anakusaidia kitandani usihamaki kachukue pop corn  uangalie tv sebuleni uache muvi iendelee.
MAANA YA MWANAMKE NYUMBA

Bye

















Toa maoni yako

Thursday, January 23, 2014

NGUVU ZA ................... TALK ABOUT LOVE





Deo wa Moshi

Dada mi naomba unishauri  mi sio mwelewa sana wa mambo ya mapenzi, nina miaka 27,
nikiwa na demu wangu yaani naishia moja tuu mpaka kaanzisha ugomvi home kuwa nina demu mwingine, nifanyeje


JIBU
Pole kaka kwa matatizo hayo nasikitikita mbona ni kijana mdogo sana inakuwaje?
Hebu kama una mawazo punguza kisha onesha kujali uwapo kwenye majamboz, uambie moyo wako kuwa huyo uliyenae ndie alpha na omega huna mwingine unaempenda zaidi yake.
kisha jaribu kutumia muda kidogo katika maandalizi ya kuingia kwenye tendo,

Pia tahadhari na kuiga mambo ya porn kwani mwanaume mishipa ya nguvu za kiume ipo mwishoni na ni myembamba sana hivyo unapomruhusu mwanamke akunyonye akitumia meno huwa anakata ile mishipa taratibu mwishowe unakuwa mbete mbete.

Pia kinywa au sehemu ya nyuma ina joto kali sana kuliko ilivyokadiriwa na Muumba hivyo kama ukijizoeza hizo sehemu mbili kutumia basi una hatari ya kupoteza nguvu mapema sana kuliko unavyotarajia, na hata ukimwingilia demu sehemu ya kawaida basi hutahisi raha yoyote na kusababisha usifunge magoli ya haja.

Pia chakula jamani kinachangia sana kupoteza nguvu za kiume, hebu jaribu kula full diet uone, achana na vihepe au mkate hebu kama inawezekana, kisha penda kutafuna muhogo mbichi na karanga mbichi kama demu wako hajakukimbia.

Tafadhali usijaribu kunywa madawa hovyo yatafanya tatizo liwe kubwa badala ya kupungua.
ni hayo tuu. 

taa taaa











Toa maoni yako