Saturday, January 25, 2014

Mapenzi ndoa - i love you kelele tuu







Halima wa Dar

Shikamoo Dada mi ninauliza hivi
Nina bwana ninaishi naye mwaka wa 5 sasa kila nikimwambia kuhusu ndoa anakuwa mkali na kuniuliza kwani nimepungukiwa nini, 
nami ninaamini tukifunga ndoa itanipa kujiamini pia kuishi hivi tunamkosea Mungu nifanyeje dada?

JIBU
Mmh jamani naomba usikwazike kwa majibu yangu,
Kosa la kwanza ni  kitendo cha wewe kwenda kuishi na mwanaume bila mwanaume kukamilisha taratibu,
umejirahisi kupita kiasi my dear, tena hata familia yako sina uhakika kama ilifurahia, kwani furaha ya wazazi ni kuona binti yao anafuata maadili .   Hee inakuwaje kwani utoke kwenu kwenda kuishi na mwanaume hivi hivi duuh kiasi yakukute. 







Kwa mila za kiafrika sijui mabara mengine ni mwanaume ndio anaesumbuka ili kukupata.  Sasa we ulipojippeleka ukamrahisishia kazi ndio maana haoni umuhimu wa ndoa, japo ni muhimu sana katika kujenga familia bora na kuanzisha ukoo.

Pili mwanzo wakati unaenda kuishi naye hukujua kuwa ni dhambi sasa baada ya kuona ndoa inaota mbawa umemkumbuka na Mungu, ni vizuri kumkumbuka Mungu kabla hujafanya jambo lako lolote.

Kisha hawa wanaume wengi wanatuliza machozi  kwa kuwa hatuwajui, mwanzo huwa wana act kuwa wanapenda kisha anaanza kukusoma taratibu tabia na mwenendo wako akiona unamridhisha basi huuachia moyo wake katika penzi,  laa akiona kuna mambo hayamridhishi baasi ataanza kukuepuka taratibu. 

 Sasa wewe uliejipeleka sina uhakika kama ameshindwa tabia yako au kakuona wa kawaida.  Lakini kaa naye muulize taratibu nini hatma ya uwili wenu atakachokujibu basi patana nacho.



 Jamani mwanaume anayekupenda atakuja kwenu atajitambulisha na kutoa mahari kisha mnaoana.  

NIWATAKIE WEEK END NJEMA





Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako