Hebu tupumzike na maswali tupate simulizi nzuuri sana ya mapenzi
Kulikuwa na mwana dada mmoja aliolewa kwa ndoa ya kifahari sana, pia alikuwa tajiri kama malkia wa nyuki. Basi pamoja na utajiri wake wote lakini hakuwa na furaha kwenye ndoa yake, yaani mume siku zingine anarudi usiku wa manane mara nyingine alale huko huko.
Mwana dada akaona makubwa haya akaenda kwa mganga kutafuta dawa ya kumtuliza mumewe, alipofika kwa mganga na kumuelezea shida yake mganga akamwambia tatizo lake ni kubwa mno linahitaji apate ngoya za simba zile za shingoni. akasema hakuna shida ili mradi tuu mumewe atulie nyumbani.
Siku iliyofuata akachinja mbuzi akabeba miguu na mikono akaenda porini kumtafuta simba, akafika sehemu kuna bwawa la maji pembeni kuna mti mkubwa. Basi akapanda juu ya mti akachukua kamba akafunga ile miguu na mikono ya mbuzi kila moja na kamba yake alafu akaining'iniza chini simba alipopita kwenda kunywa maji akadaka ile miguu na mikono akala kisha akaenda kunywa maji.
baada ya hapo yule mwanamke akashuka akaenda nyumbani, kesho yake akafanya vile vile huku nae akishuka kwenye tawi la chini, baada ya wiki moja simba akazoea kupitia pale na Mwana dada nae woga ukapungua akashuka mpaka tawi la chini kabisa siku hiyo ile anampa tu akamvuta manyoya ya shingoni simba akatoka mbio na mwana dada nae moja kwa moja mpaka kwa mganga.
Alipofika mganga alishtuka akamuuliza amenunua wapi mwana dada akamwambia ameyachomoa mwenyewe shingoni kwa simba. Mganga hakuamini akamwambia itabidi kesho akamwonyeshe alivyoyachukua. Basi siku ya pili mwana dada akampitia mganga wakaenda mpaka kule porini, mwanadada akamwambia mganga ajifiche pembeni ya bwawa kulikuwa na kichaka fulani hivi.
Muda wa simba ukafika akapita pale kula nyama, mwana dada naye kama kawaida yake ile anakula tu akamkupua manyoya ya shingoni simba akatoka mbio, na mganga kule naye mweleka haja zote zikamtoka, mwana dada kumpitia akamkuta kajichafua vibaya sana.
Nini kiliendelea tukutane kesho
Toa maoni yako

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako