.jpg)
Habari za weekend wapendwa, natumaini ilikuwa poa.
Leo nitaendelea na maswali yenu yako mengi sana nadhani mengine tutayajibu baada ya mada ijayo.
Saimon wa Kenya
Habari yako dada mi nina miaka 30 nimeoa, ni bibi na tuna mtoto mmoja, simuelewi mke wangu huwa anamaanisha nini kulaza mtoto katikati yetu pia hata kama mmekaa pamoja ye hana mapenzi tena na mimi bali na mtoto sasa dada nikitafuta mpango wa kando nitakosea?
JIBU
Utakosea sana kaka Saimon, mwanaume anayejiamini hutafuta suluhu ndani ya nyumba yake, huyo nyumba ndogo atakusaidia mapenzi yarudi ndani au atazidi kubomoa.
Na ukiamua hivyo ina maana utawatenga mama na mtoto, na nyumba ndogo zilivyo mbona utasahau kama umeoa. Kisha huyo nyumba ndogo unajuaje kama atakuwa mwaminifu kwako?
Ndio mwanzo wa kubeba magonjwa na kuleta nyumbani, tafadhali tulia na mkeo hayo ni mambo ya mpito, kwani mwanamke akiwa mja mzito huwa katika hali ya kuathirika kisaikolojia na ndio maana huweza muona akinuna bila sababu, wengine hulia, kuchagua vyakula au nguo, kuchukia watu wa jinsia fulani bila sababu.
Sasa hali hiyo wengine huendelea mpaka anapokuwa na mtoto hupenda kuongea au kucheza na mtoto muda wote namaanisha mapenzi yote ya baba yanahamia kwa mtoto, anasahau kuwa sasa ana watoto wawili mtoto mkubwa (Mume) na mtoto mdogo.
Pia msaidie unapopata nafasi kucheza na mtoto kila umuonapo anacheza naye, akiona hivyo atafurahi kuona unamsapoti kwa anachokipenda naye atarudisha mapenzi kwako.
Ok bye
Toa maoni yako
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako