Thursday, January 30, 2014

USALITI NI MSUMARI WA MOTO


Nimepata maswali ya wasomaji weengi zaidi ya 20 wanalalamika kuhusu usaliti wa wapenzi wao naomba niwajibu kwa pamoja ili nipunguze foleni ya maswali yenu:


Kwanza kama ulisoma mada yangu ya TALK ABOUT LOVE yote utapata majibu mazuri zaidi lakini naomba nijibu tena.

Suala la mume/mke/mpenzi wako kukusaliti inatokana na mambo mengi sana haya ni baadhi tu:

Anakupenda kweli?
Maana huenda alikupenda ajili ya kitu fulani mfano mwanaume alikupenda ulikuwa na sura nzuri, umbo namba 8 sasa umejiachia kunenepa mpaka hata alivyokupendea vimetoweka, au ajali masikini umepoteza kiungo au sura imeharibika.
Kwa mwanamke huenda ulikuwa na mali, Umaarufu au umbo zuri baadaye vikatoweka.
Anayekupenda kweli hakusaliti hata ufikwe na majanga gani.


  • Kauli mbovu
Kwa mpenzio huuwa mapenzi yote yaani anakuambia vizuri utamjibu majibu ya karaha kama adui yako, tena kwa wote maana kuna wanaume pia wana midomo michafu akikupa moja unakumbuka kwenu.
  • Chakula cha usiku 
Tena hii ni sababu kubwa kuliko zote mwanaume asipopata hiyo kitu usaliti unauita peupee na ujue akisaliti mara moja ananogewa kujirudi sio rahisi.
 Kwa mwanamke ukiona mumeo anakunyima muulize vizuri kama hujamkosea jua kuna mwenzio anamchosha maana huwa hawawezi kuvumilia bila hiyo kitu.
  • Makaribisho mabovu 
Yaani ukimuona mumeo unakuwa kama umeona gari ya taka, unakunja na sura karibu inatokea kisogoni, akipata makaribisho mazuri hakumbuki hata shati.
  • Usafi/umaridadi
Mumeo anarudi kazini anakukuta mchafu  make up au nguo nzuri unavaa ukiwa na mwaliko, 
Au we dada unaefanya kazi ukianza kwenda kazini unajipara kweli kweli, ukirudi unatafuta kanguo hakana hata sura ndio unavaa we unadhani mumeo anaona waliojipara wangapi huko nje. Na hizo nguo na vipodozi alivyonunua aishie kuona unajipara wakati unatoka inaingia akilini kweli.

Pia usafi wa kwa bibi jamani tuseme ukweli kuna wadada wengine wananuka sana, kwa sababu hawapendi kutumia maji kujisafisha, mwanamke maji ndio kila kitu, pia usisahau mwanamke ana miswaki miwili, kujipara usoni hakuna maana kama hujisafishi vizuri, hamu yote humuisha mwanaume akikuta kwa bibi kuna uvundo shost, atakupa mgongo kama hakujui.
  • Matumizi 
Yanazidi kipato kila uonacho mwanamke roho inakusimama, mumeo akisema hana pesa unauvuta mdomo, akimpata anae mhurumia umelia.

Na nyie wanaume mabahili,  mkeo hajui mapato yako, humpi chakula kizuri, mavazi anayaona yanang'aa kwenye maduka, kila siku unamwimbia wimbo wa subira, dagaa lake mchicha ndio kabisa kila siku, pesa ya matumizi unampa kila siku haitoshi hata mlo wa siku, mwanamke hana hata akiba kidogo haaa weee akimpata anayempa elf kumi tu atakusaliti lazima.
  • Ugomvi wa kila mara  
Yaani hamkai pamoja lazima majirani wazime radio kuwasikiliza mnavyogombana, hata mnachogombania hakina kichwa wala miguu, mmoja wenu akiwa hayupo cm kutwa uko wapi, unarudi saa ngapi maswali meengi kama mnapendana vile.
Ndio unakuta mwanaume akitoka kazini anakaa kwanza mahali mpaka saa nne za usiku ndio unarudi na kusingizia foleni, lakini ukweli  haoni faida ya kurudi home mapema atamaliza siku vibaya. akimpata wa kumpa raha na sio karaha zako atasahau hadi jina lako.

Jamani usaliti unaumiza sana kama msumari wa moto kwenye kidonda
 Tafadhali usimsaliti mwenzio 






Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako