Amina wa Kibaha
Dada naomba kuuliza hivi nani alileta hii mitandao ya kijamii?
Jamani ndoa yangu inang'inia mume wangu kutwa anachat na wanawake, simu ndio usiseme hatuna muda hata wa kujadili hata mambo ya familia yetu.
Tena toka ameanza mambo ya mitandao amekuwa anaomba mapenzi haramu mi siwezi basi ananuna, nikawa najiuliza mbona zamani hakuwa na mambo haya, juzi nilichungulia kwenye laptop yake mmh nilichokiona dada mavideo ya ngono kajaza humo,
Natamani niondoke lakini watoto wangu bado wadogo sijui hata nifanyeje ndoa yangu naipenda ina miaka sita tuu.
JIBU
Pole sana mdogo wangu,
Mbona wengi tunatumia mitandao na ndoa zetu zipo salama salimini.
Huo ni ulimbukeni wa teknolojia mwanaume weye na wala aliyeleta hakukwambia ubebe taka zote upeleke nyumbani kwako hayo maporn unayo angalia wenzio wapo kazini wanalipwa, wanakunywa madawa, wana madaktari wao wanapimwa afya na kila kitu we ukamfanyie mkeo hata aibu huna.
Kwanza wana mapenzi gani kuzidi yetu ya kibantu khaa uchafu mtupu, kinachokufanya uvunje ndoa yako nini, hao unaowaona wazuri kwenye mtandao ni make up tuu hebu kawatembelee asubuhi uwakute ndio wanaamka kama hujatapika. Hata mkeo ukimnunulia anaweza kuwashinda hao wanao kuzuzua. Hivi hujiulizi kutwa nzima wanachat na wangapi, wangapi wanaambiwa love you kama wewe, acha umburulaaa.
Mdogo wangu usiondoke pigania ndoa yako usidhani hao wanaomzuzua ni wakaaji, wao ni wabomoaji tuu utatesa watoto wako bure shost hayo magume gume yaloshindikana na mitume yasikutishe, tena jiamini wewe ndio mwenyewe wengine wote wezi.
Pia usikubali kabisa huko anako kuomba tena uwe macho maana wanajifanyaga wamepotea njia, mwache anune kama ana uwezo akumeze kabisa ukae tumboni mwake. Atakuharibu utembee na nzi kama unauza utumbo, kisha akubwage mchana kweupee. Jali wanao mwaya watapata shida malezi yao yanategemea umoja wenu, akizidi mpeleke kwa viongozi wa dini.
Toa maoni yako
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako