Monday, May 5, 2014

MAPENZI IMARA HULETWA NA MWANAUME

Ndio kwa kila kona mwanaume anahusika sana kwanini



  • Mwanaume ndie anatongoza na ndie mwenye kuchagua yupi anamfaa kuishi naye Mwanamke hata umpende namna gani huwezi kumlazimisha uishi naye.
  • Mwanaume ndie mtunzaji wa familia kwa asilimia nyingi hata mwanamke akiwa na kipato bado mwanaume ndie anajulikana ndani kuwa msimamizi na mtekelezaji wa mipango yote.
  • Mwanaume ndie anaruhusiwa kumdhibiti mwanamke kama kumpa ruhusa na kumpangia muda wa kurudi, kumruhusu kufanya kazi, biashara, hata kusafiri ki matembezi.
  • mwanaume ndie mwenye wajibu wa kutaka kitu na kukataa mfano marafiki wa mke, chakula, mavazi mkewe avaeje n.k
  • Mwanaume akiwa hataki chakula cha usiku huwezi mlazimisha hata ufanyeje kwani maumbile yake hayawezi fanya kazi mpaka mwenyewe apende, kinyume na mwanamke hata kama hutaki mwanaume atajisevia tuu.  Pia ndie mpangaji wa magoli kama mawili au matatu au kamoja huwezi mlazimisha aendelee.
  • Mwanaume ana ushawishi mkubwa sana kumridhisha mwanamke na hata kama anamuongopea mwanamke si rahisi kujua kwa wakati huo.
  • Mwanaume akiamua kutulia na mkewe hata atokee jini hataweza kumbadili.
Sasa wewe mwanaume una mke mzuri wa sura na tabia mpaka marafiki zako wanakuonea wivu, michepuko ya nini?
Ndani unakuwa kama shetani unacheka asubuhi mchana ushanuna, salaam kwa mkeo ya nadra unatoka kazini ukifika nyumbani huna tabasamu, huna salaam ya bashasha kwa mpenzi mkeo.

kama mmepata watoto ndio linageuka jina lake mama sikujua, au mama kidole hee huoni haya ulipokuwa unamfukuzia ulikuwa unamwita nani? ile sweetie, my love. honey baby imeishia wapi?

Kama hamna mtoto ndio unamkata jina hata mbele za watu wee Johari, Jane, Maimuna n.k kama mtoto mdogo heshima na thamani yake iko wapi ukimwita mke wangu utapungukiwa nini?

Humtimizii mkeo mahitaji, humrembi ukafurahia urembo wake  huna habari na bajeti ya vipodozi ni bora ukahonge mchepuko laki mbili akasuke wakati mkeo hata elf kumi ya kusukia  inakushinda kumpa.

Mchepuko unautoa out kwenye hotel nzuri mnamaliza laki kadhaa mkeo nyumbani dagaa na mchicha havina mwanzo wala mwisho wa mwezi, na hizo hotel hujawahi mpeleka tangu umemuoa.

Kurudi kwako usiku wa manane kila siku foleni za Dar nzima zinakukuta wewe tuu, siku akikuona mapema ujue huna hela.




Hata siku ya weekend ambapo ni muda mzuri wa kukaa na mpenzi mkeo naye akadeka kidogo kwa mumewe ndio kwanza utapanga safari zisizo kuwa na msingi akikuuliza unamwambia wacha ukatafute hela atakula nini.  heee alifuata kula kwako?  Jiangalizieni 

Na siku utakayojaaliwa kuwa nyumbani ni mazogo yasio na sababu ili mradi karaha mtindo mmoja mpaka mkeo anaomba Mungu upigiwe simu uondoke looh.

Siku utakayoamua kumpa mapenzi ndio kabisaaa maana huna rai unamkamata mwanamke kama unagombana nae kumtomasa kama unakanda ngano akitoka hapo hoi hana kiungo  kisicho  maumivu.

Ulimuolea nini?  Ukahangaika kumtongoza, ukachukua namba za simu ukapanga mipango ikapangika ulimaliza soli za viatu ukampa ahadi zingine hazitekelezeki,  mpaka ukamtoa kwao kwa vigele gele hiyo michepuko yako ilikuwa wapi?

Kila siku kumtoa hila mkeo kama wewe umekamilika vile kosa dogo kwako kubwa siku hiyo utasema usiku kucha mkeo halali masikini anaishia kulia tuu kaomba msamaha huelewi ndio kwanza kakutia funguo ya kashfa, matusi ya reja reja.


Ukweli wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa si kwa mapenzi bali labda kwa ajili ya watoto, mali wamechuma wote sasa anaona akiondoka ataenda kuanzaje maisha, wengine mashinikizo ya wazazi, wengine wanaionea aibu jamii kuwa wataonekana wameshindwa ndoa zao.


Mwanamke akitoka kwako anawachukia wanaume  dunia nzima na kulipiza kisasi  kwa sababu yako.

Mwanaume jitahidi kumpenda mkeo.



Wednesday, April 23, 2014

FAIDA YA TENDO LA NDOA KI AFYA





Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili.
Wataalamu wanasema kwamba unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.


  • Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.  Kuongeza mwendo wa damu.
  • Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili. hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji
  • Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
  • Hupunguza maumivu wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu  ya viungo [arthritis]  maumivu ya shingo [Whiplash]  na maumivu ya kichwa
  • Ulinzi wa tezi ya kibofu [mwanaume] Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu [prostate] yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini.
  • Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa maji maji hayo yenye madhara.
  • Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.
  • Hupunguza mfadhaiko wa moyo.
  • Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini.
  • Wale wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
  • Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume [testosterone] na za kike [Oestogen]
  • Faida nyingine inayopatikana kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.
  • Hata hivyo baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.
  • Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima.  Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.  Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali  yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo [Cardiovascular].
  • Hupunguza baridi na mafua
  • Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
Jambo la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi katika njia sahihi tena usioukuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa.  Ina maana kwa wenye ndoa zao tuu.

Friday, April 4, 2014

Kaoa wakati naye kaolewa 2

............. inaendelea


Basi maisha yakaendelea yule rafiki yake akawa ananipenda ananijali akija lazima aniletee zawadi, nikanunuliwa zawadi za mtoto mi meno nje.  Lakini mambo yao ni yale yale ya kujifungia chumba cha pili, tena sasa wakawa wanafunga na funguo, mi naona sawa tuu.

Ikafikia nikajifungua mtoto wa kiume wakwe zangu wakanichukua nikapumzike kwao kwa muda kama wa mwezi mmoja baada ya arobaini nikamwambia mume wangu nirudi kwangu akakataa akadai ningoje nyumba yetu iishe ili mtoto wetu afungue nyumba, sikuwa na neno.

Siku moja nikaona bora niende mara moja nikachukue nguo za kubadili maana mwili umerudi katika hali ya kawaida hivyo madira tena yamenichosha, nikaenda mtoto nikamwacha kufika nyumbani nasikia dirishani sauti ya mihemo ya mahaba sauti nzito mmh nikasogea kusikiliza vizuri nasikia ni mume wangu jamani dada nilitamani kuzimia maana nilijua kaingiza mwanamke mwingine ndani.

                                  

nikajishauri niingie kwa mlango wa uani ili nikaufunge nikianza ugomvi huyo mwanamke akose pa kupitia.
Nikaingia ndani kuangalia viatu vyote vya kiume sauti ya mahaba, i love you nyingi analia kama mtoto wee dada dunia ina mambo.




Nikasukuma mlango ulikuwa wazi nikakuta mume wangu kainamishwa analiwa kiboga anakatika huyo nilizubaa kama nimepigwa shoti, yeye hakuniona ila rafiki yake aliniona akanionyesha ishara nitoke nje, niligeuka bila kusema neno nikakaa sebuleni nasikia mume wangu anamwambia rafiki yake ahsante mume wangu, nikazimia.

Kuja zinduka nipo hospitali, ndugu na wakwe zangu wapo hapo, wananiuliza kulikoni machozi yananitoka, akadakia yule rafiki wa mume wangu kuwa nilipoenda nyumbani niliona nyoka nikapiga kelele nikaanguka bahati nzuri walikuwepo wakampiga yule nyoka na kumuua.

Nikatoa macho kama nimeibiwa nauli wakaniuliza ni kweli nikaitika kwa kichwa kukubali machozi yanazidi kunitoka basi baadae nikaruhusiwa mume wangu akanichukua kunirudisha nyumbani kwangu akidai anataka kuwa karibu nami.

Kufika nyumbani mume wangu akaniambia ni kweli yule ni mumewe , kipindi cha nyuma aliwahi kwenda uaya kwa njia za panya sasa kufika huko huyo rafiki alikuwa huko akamsaidia sana mpaka akapata uraia, hadi kufikia kuwa wapenzi wakaoana. 

aliporudi Tanzania baba yake alishasikia kuwa ana mahusiano ya jinsia moja yeye akakataa ndipo wakashauriana na huyo mumewe kuwa aoe ili kutuliza hasira ya wazazi, na ndio maana alihamaki alipoona nimebeba mimba lakini rafiki yake alimpeleka hospital kupimwa akaonekana ana uwezo wa kuzaa.

Sasa ananiomba sana nisimwache atakosa radhi ya wazazi, na pia hawezi kumuacha huyo mumewe kwani ndio anatuweka hapa mjini, ameniandikia nyumba gari mbili na huyo mumewe anafanya mpango wa safari twende wote ulaya maana wanaona hapa ninaweza toa siri.




Nishauri dada nimekonda sana silali kila akija mumewe wakijifungia tu mie machozi yananitoka mwanangu ana miezi sita tu  jamani nifanyeje waungwana mnaosoma humu naomba ushauri wenu.

Jamani anaomba ushauri mi kwangu network loading ...................????????????

Sijawahi kusikia haya Mungu wangu.




Thursday, April 3, 2014

kaoa wakati naye kaolewa

Ahsante dada kwa kutupa fursa hii ya kutoa ya moyoni,

Kwanza nampa pole huyo dada akaze moyo Mungu atamsaidia,

Mi yangu makubwa zaidi dada



Mi nina miaka 25, baada ya kumaliza form four, nikapata bahati ya kupata mchumba pande la mwanaume, mzuri, mtanashati yaani dada ukimwona utasema kweli, nami hata sikujivunga nikakubali haraka haraka, kazi alisema ye ni mfanya biashara.

Basi maandalizi yakafanywa binti nikafundwa nikafundika maandalizi ya kwenda kumuhendo mume wangu.
ndoa ikafungwa kwa fahari jamani tulipendeza wenyewe nikikumbuka nalia kama mtoto.

Basi tulienda honeymoon siku ya kwanza tukalal akadai ana presha ya ndoa kesho yake asubuhi ndio tukafanya tendo la ndoa.

wakati tunafanya akawa ananiambia nimpapase kwenye makalio basi nikimshika anasisimkwa na kuniambia kazana nikifanya hivyo yeye ndio anapata speed  mpaka tukamaliza.

Ukweli dada lile jambo lilinishangaza sana mpaka likaninyima raha kwani sikuolewa na bikra hivyo mapenzi nilikuta nishaanza pia hata kwenye mafunzo sikusikia kitu hiki.
Basi ikawa ndio mapenzi yetu kama treni ya kizamani mpaka uchochee kuni ndio liongeze mwendo.

Nikaenda uliza wakubwa nyumbani wakaniambia haina neno ndio mambo ya digital hayo mumeo  kazoea mambo ya kizungu, basi maisha yakaendelea. 

Sasa kitu kingine alikuwa anaaga anasafiri lakini sehemu anayokwenda ukimuagiza kitu cha huko harudi nacho madai yake ye mvivu wa kubeba mizigo, nikitaka out ananitafutia rafiki yake niende naye yeye anadai hapendi mambo ya kutoka toka basi mi natoka narudi namkuta amelala au anaangalia tv.

Baada ya miezi minne nikashika uja uzito heee wacha alete maneno anadai sio wake nimueleze niliko upata, nikamueleza yeye ndie mume wangu sasa aanipe nani mwingine, mwishowe akaniomba nimsamehe alikuwa anataka uhakika kama yake kweli.

Sasa alikuwa na rafiki yake huyo ana pesa sana na hata ikitokea shida nyumbani basi akimpigia hata usiku wa manane anatuma.  Kila mara anakuja nyumbani na huwa wanaingia chumba cha pili na kuniambia nisiingie huko wenyewe wanapanga mambo yao ya biashara.



Siku moja alikuja rafiki yake huyo wakaingia chumbani kama kawaida mume wangu akasahau simu ikaita 
nikampelekea ile nafungua mlango nikakuta wamekubatiana nikatoka mbio mume wangu akanifuata na kuniambia walikuwa wanapongezana wamepata mafanikio kwenye biashara, baadae rafiki naye akatoka akanipa dollar 1000 akanikumbatia na kuniambia nina kismeti cha biashara sana wamepata mafanikio sana tangu nilivyo olewa nikachekelea mwenyewe kumbe dada wewe mmh

itaendelea......................


Wednesday, April 2, 2014

mapenzi ya tigo ni unyama

..............inaendelea


dude lote hili unalikandamiza kwa mtoto wa mwanaume mwenzio tena njia isiyofaa huna haya


Basi dada nikawa sina raha hata nikikaa mbele za watu inabidi nijibane sana maana nikikaa vibaya tu mashuzi yananitoka pia nilipokaa lazima niloweshe.

Baada ya kuniona hivyo akaanza kunikwepa, akawa anakuja kwa mwezi mara moja anasingizia safari sometime anamtuma dereva aniletee pesa ya chakula au kuja lipa bill basi.

Mi huku nyuma nikawa naumia nikienda haja kubwa, nikaamua kwenda hospital doctor aliponiangalia akakuta ndani kuna vidonda vikubwa  basi akaniambia huyu aliyenifanyia kitendo hiki alitumia nguvu pia hakutumia vilainisho au ana dushelele kubwa kiasi alinichana wakati ailazimisha kuingia.  
pia nina maambukizi ya virus vya ukimwi, ukweli nililia sana nikaona kama dunia imesimama,
nikapewa ushauri nasaha na kuanza clinic ya wenye virus vya ukimwi na kuhusu huku nyuma 
nikafanyiwa matibabu nikaambiwa niache huo mchezo kwani sehemu ya tundu imeharibika vibaya sana.

Nikaja mwambia nilivyoambiwa na doctor hakunijibu alinyamaza kimya, asubuhi yake akagiza dreva aje achukue gari inaenda service, jioni akaja na kuniambia bora nikaugulie nyumbani kwani pale sina mtu wa kuniangalia akanipeleka mwenyewe, baada ya siku mbili nikaletewa vitu vyangu vyote na kuniambia nitakuwa simfai kwani furaha yake ni tigo sasa kwa kuwa siwezi kutoa tigo tena basi akanipa 50,000/- na kunitakia maisha mema.
 Dada hiyo ndio story yangu nimeitoa makusudi wasichana wanaokurupuka kuona mabwana wenye pesa ndio watawabadilisha kimaisha kuna manyanyaso na madhara ,makubwa sana.

Hii ndio story niliyoletewa na mdau wangu huyu inasikitisha jamani




nyie wanaume nyie hasa wenye pesa zenu ina maana mmeamua kaabisa kuifanya dunia ndio pepo yenu nashindwa hata la kusema maneno yanaishia rohoni.

Naamini ukweli kabisa wanawake wengi sana huanza kutumiwa tigo kwa kulazimishwa.  Tena waume wengine huwafanyia wake zao mchezo huu jamani, akikataa tu anamwanzishia visa mpaka ataiona ndoa chungu.

We ukimuona mpenzi/mumeo kila unavyojitahidi kitandani mwenzio hata kuguna macho makavu bao moja la kutafuta, ulikuwa unajiliza i love u zinakutoka mpaka unabaki unaguna, mikao yote umemaliza wala hasisimkwi hapo mwenzio keshaonja njia ya mavi.
au kutwa anakupapasa makalio, ukimpa staili ya mbuzi kagoma kwenda unamuona anachangamka kama katiwa funguo  kwa kuona kinyeo basi ujue keshaanza huo mchezo.

Wengine utaona akizama chumvini anazama mpaka kwenye tigo anatumbukiza ulimi madai yake mapenzi hayana kinyaa au kila akitumbikiza dushelele anajifanya anakosea njia dakika katoa anakosea tena pa kupeleka anapeleka tigo huo ndio mwanzo mkimbie huyo hata kama anakupa milioni haina thamani kwako.


Msiwaone baadhi ya wadada mjini wana magari wanaishi kifahari  ukawatamani yaliyo ndani ya vifua vyao wakikufunulia utaona bora dagaa lako unalila kwa amani.

Vitabu vya Mungu vimelaani jambo hili, miji ya Sodoma na Gomola  iliangamizwa kwa vitofari vya moto miji hiyo mpaka leo hata majani hayaoti, Mungu anatuonyesha jinsi gani analichukia jambo hili.

Kwanza katika viumbe wote duniani wanaotumia mapenzi haya ya kinyume na maumbile ni nguruwe na binadamu sasa wewe unaetumia njia hii ina maana akili zako zinafanana na nguruwe?



Tafadhali ukiwa na story yako ya mapenzi niletee iwe ya kweli nitaitoa hapa kwani ni funzo kwa wengine

Ok kama unalo la kumshauri huyu dada tafadhali niandikie kwenye MAONI.USHAURI  au comment hapo chini.


Tuesday, April 1, 2014

Mapenzi kinyume na maumbile ni hatari

Sijui ni laana au ndio kumkataa Mungu makusudi 

Msione naanza hivi jamani nina hasira baada ya mdau wangu kunipa kisa hiki:-


Dada Johari 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 28, mkazi wa hapa dar, sijaolewa na sijapata mtoto.  Nimelelewa na mama bahati mbaya baba yangu alifariki mi nikiwa nina miaka 9, kiasi ilichangia hata masomo  niishie form four.

Nilipata mwanaume mwenye hela zake na ana cheo kikubwa tu, basi nikafurahi nikaona nimepata bahati kubwa sana, na kwakuwa maisha ya kwetu  yalikuwa ya chini kiasi hamjui kesho mtakula nini.

Basi baada ya kuduu mara mbili akaniomba anipangie chumba basi nikamwambia ngoja nikamwambie mama.  Mama alikubali kwani kwa muda mfupi niliokuwa nae kiasi alichokuwa ananipa kilisaidia sana maisha yetu.
Basi akanipangia upande appartment Mikocheni  nikaona mwanaume si ndio huyu.  Baada ya mwezi akaanza kuwa ananitia vidole nyuma au akizama chumvini mpaka na kwenye tigo anatumbukiza mi naona ndio mapenzi na vile nilikuwa nasikia raha ndio kabisaa.

Tahamaki siku hiyo nikaona dushelele analiweka kwenye tigo, nikashtuka akaniambia pole pole nikawa naumia ananiambia kichwa tu baby, ukweli niliumia sana baada ya hapo machozi yananitoka nikamuuliza kwanini kanitendea vile akaniambia mbona yeye ananiridhisha kwa kila ninachokitaka sasa mimi nashindwaje kumpa anachokitaka, kama nampenda kweli basi kila siku nimpe tigo ndio furaha yake.

Nikamuuliza kama sitaki jee akaniambia niondoke home maana nitakuwa sina fadhila,  Basi nikamwambia naomba niondoke nyumbani akasema kama hivyo nimlipe gharama zake zote, laa sivyo atanifungulia kesi na atahakikisha mpaka nyumba yetu inauzwa.  Nikawa mdogo kuliko sisimizi, furaha yote ikayeyuka nikamwona kama ziraili, kesho yake akaniletea gari aina ya Noah akanitafutia mwalimu wa kunifundisha, nyumbani nako akawa anapeleka matumizi mdogo wangu wa mwisho akamtafutia shule ya sekondari boarding Kenya.  

Familia nzima ikamwona mfadhili mwema kabisa kumbe mwenzao nateketea.  Baada ya mwaka mmoja nikaanza kuvuja maji kwenye tigo nikawa navaa pedi bila kuwa kwenye siku zangu yaani we dada acha tuu.

itaendelea .................


Hajamaliza kisa chake tuendelee kesho panapo majaliwa

Wednesday, March 26, 2014

FURAHA YA NDOA

Furaha ya  ndoa hainunuliwi dukani, haitafutwi kama pesa wala haichimbwi kama madini.

Basi tunaipata wapi furaha ya ndoa?
kufunga ndoa ni jambo moja lakini furaha ya ndoa ni jambo lingine hivyo usitegemee ile furaha ya siku ya ndoa itakuwa milele.
 Furaha ya ndoa mtaitengeneza  wenyewe mume na mke ndani ya nyumba kwa:-

  • kudumisha mahaba kwa kila mmoja wenu kila siku ajitahidi kuongeza vionjo.
  • kuvumiliana kwa kutambua kuwa kila mmoja weenu ana tabia ambayo mwenzie haipendi ila anavumilia.
  • kusameheana kwa makosa madogo madogo kwa kujua kuwa nyie ni binaadamu hamjakamilika hivyo unasamehe na kufuta kwenye akili kama kilitokea nini.
  • jaribu kumfanya mwenzio ni mpya hata kama mmeishi miaka mingapi.
  • tengeneza furaha ya mwenzio kabla yeye hajatengeneza ya kwako ina maana mpendelee mwenzio kwa kumfanyia vitu anavyo vipenda kabla ya kudai kufanyiwa wewe.
  • wazazi, ndugu na jamaa hawana nafasi ndani ya mapenzi yenu wao ni washauri tuu pindi yakiwashinda kutatua nyie wawili.
  • Watoto wasiwe nguzo ya mapenzi yenu mkaishi eti kwa sababu mmezaa mnatakiwa kuishi kwa mapenzi na sio kwa kizazi
  • kauli njema ni kitu muhimu sana kinachodumisha furaha ndani hata kama kuna hitilafu kiasi gani hupozwa na kauli njema ya kila mmoja wenu
  • thamani ya kila mmoja wenu inahitajika kwani dharau ni moja ya vitu vinavyobomoa mapenzi mpaka mkaishi kama maadui wakati mlikuwa wapenzi.
Mkidumisha hayo mtaionja pepo duniani kabla ya kufa 


N.B   Jamani mwenzenu najitolea kutoa elimu hii si kwa sababu najua sana au ni mfanyaji sana wa haya mambo mi ni mtu mzima na heshima zangu kamili.  Sasa baadhi yenu comment mnazoniletea nyingi hazina maadili, wengine mnatongoza, wengine mnauliza maswali hayana msingi, hii sio blog ya kikubwa ndio maana natumia tafsida kuongea baadhi ya vitu humu, hivyo nikaona bora nisirushe comment zenu nazisoma na kuzifanyia kazi.
Kwa wale mliouliza kwanini sirushi comment zenu jibu ndio hili endeleeni tuu kuelimika mpaka nitakapoona mmetumia lugha nzuri.

Friday, March 14, 2014

JOKA LIBWELELE NALO MMH

Leo tuangalie jinsi gani ya kukabili maumbile ya mwenzio.


Kimaumbile kila mtu kaumbwa kivyake na hakuna mtu anayefanana na mwenzie lazima kuna tofauti fulani.

Sasa wengi humpenda mtu kabla ya kumjua maumbile yake hasa wanawake huwa tunakutana na surprise nyingi sana.

Humuita  mpenzi kabla ya penzi wengine hupanga hata kuoana, ahadi kem kem, kutwa simu, chatting kila wakati, I love you nyingi sana, hajajua maumbile yake anakisia tuu.

Siku inafika wanapanga kwenda banjua amri ya sita, ndio hapo utamu wa penzi na uchungu hutokea.

Mwanzo huanza kwa pupa kama wana mashindano shati kule blauzi huku, suruali pale sketi hapo vichupi vinarushwa vinakoangukia havijulikani.

Niseme ukweli wanaume ni wastaarabu sana hata akikuta bwawa la mtera basi atajitahidi afunge bao kimya kimya.
Sie wanawake mh, akikutana na kibamia basi kutwa analazimisha kirefuke, atasonya atakunja uso hali ya mapenzi itatoweka yaani mpaka mwanaume anajihisi unyonge.

Akikutana na joka libwelele ndio kabisa anaweza singizia ugonjwa wa tumbo wa ghafla, au akazua ugomvi uso na kichwa wala miguu akavaa akaondoka zake.  Na I love you zinaishia hapo hapo tena wengine yakiwazidi hutoka na taulo mbio kama kafumaniwa kumbe kakutana na kitu mkono babu weee.

Ukipenda boga penda na ua lake ulikuwa unampenda wakati ana nguo zake hukufikiria kuwa akizivua itakuwaje. 

Mambo ujuzi shost ukikuta kibamia kina staili zake ye akaridhika na we pia ukaridhika  tena ukikizoea wala hutataka tena joka libwelele.  Raha ya kibamia hata ukimwi ni ngumu kuupata kwani hakichubui.

Pia hata hilo Joka pia lina staili zake mengine ukubwa wa bure nguvu ndogo  hivyo inatakiwa ujuzi wako tu jinsi ya kulikabili na wote mkatosheka.

Kwa wanaume akikutana na bwawa au mazingira machafu huyo ndio harudi tena, hata simu yako hapokei.

Kuna wengine wana tabia mbaya ya kutangaza maumbile ya mwenzie kama yanauzwa sokoni si ukamnunulie mazuri ni vibaya sana kutoa siri za mwenzio hata kama humtaki tena.

Ushauri wangu kwa wote jaribuni kuvumiliana kwani alivyoumba Mungu hakuna wa kumkosoa na huwezi pata maumbile unayoyataka bali ukipata afadhali basi shikilia, mengine yanazungumzika, la sivyo utazipitia mpaka usahau ulianza na ya vipi.

Ukitaka hayo maujuzi niandikie kwenye MAONI/USHAURI  nitakupatia.

Thursday, March 13, 2014

Urafiki na Mapenzi

Assalaam alaykum wapendwa  wasomaji wangu,

Leo hebu tuongelee mapenzi na urafiki.




Rafiki ni mtu mzuri sana na husaidia wakati mwingine kuliko hata ndugu wa damu.
Hujitoa sana na hasa kwenye matatizo huwa mstari wa mbele mpaka tatizo linapoisha.
Pia rafiki huwa hajali kuwa wewe si ndugu wa damu bali hukutanguliza mbele kwa raha na shida.

Urafiki huu hudumu na kuwa mzuri sana kama nyie wote mkiwa hamjaoa/hamjaolewa, inapotokea mmoja kaoa/kaolewa hapo ndio utata unapoanza.

Kwa wanaume huwa mnakosea kumwamini rafiki mpaka kwa mkeo, wengi sana wamekutwa na mikasa ya marafiki kutembea na wake zao.

Unapokuwa umeoa lazima kuwe na mipaka mfano:-

Muda wa kuja rafiki nyumbani 
Rafiki aje nyumbani wewe mwenyewe ukiwepo, tena mchana na mkeo awe katika hali ya kawaida, sio anapenda kuja nyumbani we haupo au mida ya jioni ambapo mkeo kajipara kapendeza ana vikanga vyake viwili kavaa mwenyewe kwa ajili ya mumewe tahamaki rafiki huyu hapa, anamuona mkeo alivyopendeza roho inamruka anaanza kumsarandia mkeo ukiwafumania unampa mkeo talaka kumbe we ndio ulisababisha.

Au kila ukitoka rafiki ndio anakuja unapata salaam tu rafiki yako alikuwa hapa, kwanini umruhusu rafiki awe anakuja we hupo anaongea nini na mkeo.  Kwani hata kama huyu ni rafiki yako lakini na huyu ni mkeo sio mke wenu.  Rafiki aje nyumbani apikiwe ale akae atazame TV we hupo mmmh kweli.

Sehemu za kuwa pamoja na rafiki

Kuna sehemu mnaweza toka na mkeo na rafiki pamoja, tena mkeo asivae nguo za mitego wala asijipare sana, muda wote hakikisha upo pamoja na mkeo kwenye kutembea, kukaa, kama upo club hakikisha unacheza nae mwenyewe, sio unamruhusu rafiki akashike kiuno cha mkeo shanga alizovaa azihesabu.
Wakirudi kukaa wanaanza kukanyagana chini ya meza we huna habari 

Mkiwa nyumbani mara simu zinapigwa na rafiki kwa mkeo  ukiwepo rafiki anadai kapiga kwenye simu yako hajakupata.




Nimeombwa nitoe hii mada na mwanaume mmoja alikuwa na rafiki baada ya kuoa urafiki ukaendelea mpaka yeye na mkewe wamepata watoto wawili.
Sasa akaona mazoea yamepita kikomo akagombana na rafiki yake ndipo siri ikatoka kuwa hata wale watoto ni wa rafiki na baada ya ugomvi huo anawataka watoto wake alee mwenyewe, hivi kesi ipo mahakamani.

Mpooo wenye marafiki

ukiwa na chochote nimwagie hapa nami nitakitoa bila kutaja jina wala address yako 
niandikie kwenye MAONI/USHAURI 



Tuesday, March 11, 2014

Wazazi mnayajua haya

Watoto wapo likizo tumia japo dakika 30 kuongea na mwanao hali ni mbaya




Vijana wadogo hawajajua hata maisha ni nini hayo mapenzi ya jinsia mbili hawajayafaidi hata robo wanaenda kuanzisha ya jinsia moja Mungu wangu.

Hivi natafuta nani aliyesababisha haya



ukimuuliza mzazi analia na utandawazi,
ukimuuliza Mwalimu analia na mzazi
ukiiuliza jamii wanasema mambo ya digital
wote wana makosa


Hebu tuanze na wazazi
asilimia nyingi hawana muda na mafundisho ya watoto wao, Baba kazini kurudi usiku Mama kazini kurudi jioni.
Mama akifika nyumbani humuuza dada wa kazi je watoto wamekula, wameoga, walikwenda twishen akiambiwa ndio basi huwaona watoto wasikivu sana tena huwapa na zawadi.



Tena wazazi wengine hufanya matendo ya aibu mbele za watu hadharani na watoto wadogo wakiwepo wakiona dhahiri shahiri.

Baba akirudi huuliza mwl kasema nini shule kama mchango anatoa wachache wanaopitia hata daftari za mtoto, ye anachojua ni ada na mahitaji ya shule ya mtoto.

Lakini hawakumbuki huyu au hawa watoto wanatakiwa wahubiriwe nini maisha, wawe na tabia zipi, watakuja kuwa nani mbele ya safari tena unawapigia na mifano hai ya watoto watukutu nini kimewakuta na wakiwa watoto bora watafanana na nani.  huo muda wazazi wa sasa hatuna.

Mwalimu
Zamani mwl. alikuwa ni mzazi wa pili kiasi ukiwa naye unahesabu kama una mzazi wako na hata ukifanya kosa lazima atakuonya na ukizidi anawaita wazazi wako ili wamsaidie kukuonya kwa kosa unalofanya, na usiposikia unafukuzwa shule.
Sasa mmh waalimu baadhi yao wanajali maslahi yao na nimeshuhudia shule moja hapa dar st. fulani [jina kapuni]  mwl. kaachishwa kazi kwa kumfuatilia mwanafunzi mwenye utovu wa nidhamu, akiambiwa alipaswa amheshimu yule mwanafunzi kwani ndie analeta mshahara wake.


Sasa watoto wetu wanaokwenda ma boarding ndio kabisa jamani kuna tabia za ajabu sana usagaji ma ushoga wanauanzia huko.

Haya jamii nayo
Badala ya kumlea huyu mtoto hasa wanaume mnaovivua chupi vitoto vya kike mnapata raha gani kwao jamani.
Mzazi mwenzio kagharamika masikini anajinyima kula na kuvaa vizuri kwa ajili ya huyo mtoto unaamua na makusudi kumuharibia mwanaye kwa pesa na magari yako ya kifahari, tena nawe umezaa na una watoto wa kike hufikirii je ukimkuta mwanao ndio anafanyiwa hayo utajisikiaje.

Ukisha mharibia masomo yake unamtelekeza nyumbani nao kwa uchungu wa pesa zao na fedheha wanamfukuza nyumbani basi maisha na ndoto zake vinaishia hapo masikini.

Leo tunakataa ushoga kwa maneno lakini kivitendo umejaa tele hao wasagaji ndio usiseme yaani akili zetu ni kama yule anaejisaidia porini uso, anauelekeza njiani ili watu wasimchungulie mgongo anauelekeza porini hajui kama akitokea simba nyoka au mnyama yoyote wa hatari aka ye hataki watu tu wamuone.

Tukumbuke SODOMA NA GOMOLA waliangamizwa na Mungu sehemu ile mpaka leo haioti hata nyasi.

Kuna haja ya kumrudia Mungu kila mtu kwa imani yake tena na watoto wake awasisitize elimu ya dini labda tutaokoa vizazi vyetu jamani.


Toa maoni yako

Monday, March 10, 2014

Baadhi ya Wanaume ni kuku wa kienyeji

Kwa maoni ya wasomaji wangu wapendwa wameomba niirudie post hii sijui kwa nini

Hebu tuangalie hawa wanaume wa tabia hii.


Mwanaume umeoa mke na labda mmeshapata watoto kisha kunakuwa na house girl au shemeji.

Mkeo ni hodari mashaallah anakufanyia mambo yote muhimu, kitandani ndio usiseme kafundwa akafundika anakupa mapenzi mazito mpaka unaomba pooo.



Tena basi hana hiyana muda wowote ukitaka penzi anakupa bila wasi wasi.

kwa kawaida hasa kwa ma house girl wengi huwa washamba hawajajua mambo ya kujipendezesha kama mtoto wa kike atakiwavyo.   Tena sometime walikotoka hata mambo ya kuoga vizuri hajui labda maji yalikuwa mail kadhaa.  Tena wengine wanakuwa na umri mdogo sana.





Ndio we na mkeo mnaanza kazi ya kumuelekeza usafi na kazi za ndani, dukani wapi, sokoni n.k
Binti huyu anakuwa na adabu sana tena kwenye zile mila za kupiga  magoti ndio kabisa hata kukusogelea wewe baba ndani ya nyumba ni kazi.

Ukirudi kazini ukikaa sebuleni yeye yulee chumbani au jikoni hathubutu kabisa kukaa pale ulipo.

Kinachonishangaza we baba mtu mzima na akili zako timamu usiku unamwacha mkeo chumbani kwenu kwenye kitanda kizuri mashuka safi huenda mkeo ni maridadi amekinyunyizia marashi unaenda kwa kile kitoto.




Jamani unaenda tafuta mapenzi gani anayoyajua yule mtoto au ni uharibifu hufikirii kama ni mwanao angefanyiwa vile ungejisikiaje. Tena unamjaza mimba na unakuwa wa kwanza kunfukuza nyumbani, aende wapi na ujauzito ule aulee nani, alikotoka huenda walikuwa wanamtegemea akipata kamshahara awatumie na wao.  Sio ndio kutengeneza machangu na watoto wa mtaani.

Tafadhalini jamani hasa nyie wenye pesa zenu wengine utamuona sehemu ya starehe ana katoto kadogo kama mjukuu wake anakapa denda uuh huwa natamani kufa Mungu anistirie wanangu jamani nikikukuta naye nakulamba risasi.

Mtoto wa mwenzio ni wako jamani tuwahurumie maisha ya dhiki yanawatosha kuwa adhabu kwao.






Toa maoni yako

Sunday, March 9, 2014

Raha ya mapenzi uyafurahie

habari zenu wapendwa,



Asilimia nyingi sana watu huwa tunamlaumu aliyefumaniwa kuwa ni msaliti, hajatulia, malaya na anakosa hadhi machoni pa jamii.

Lakini hatuangalii upande wa pili je huyu mpaka kufikia kuchepuka amekosa nini ndani kwake.

Nakubali kuna wengine tamaa zao za fedha au za kimwili hawatosheki na wanachopata.

Lakini kuna wengine wanadhulumiwa haki zao za kitandani wakavumilia mpaka wakachoka hasa wanawake.

Tendo la ndoa limekaa kama madawa ya kulevya, ukilianza linagota kwenye akili na mwili wote unakuwa na mshawasha fulani.

Mshawasha huo ukianza akili haifanyi kazi nyingine tena itakuwa inawaza mapenzi tuu mpaka ipate ndio inatulia na hii hutokea sana kwa wanaume.

Kila mtu ana mazoea yake kwenye mapenzi wengine wamezoea mara moja kwa wiki, siku mbili, kila siku kwa siku mara mbili, wengine mpaka magoli manne wengine kamoja tu anakoroma.

Sasa inatakiwa uchague mpenzi anaendana nawe kwenye hiyo mechi,  sio we unataka kila siku unakuwa na mpenzi anaetaka mara moja kwa wiki kama hamkuachana basi lazima utachepuka.

kwanza kwenye romance wanaume wengi huwa mna haraka unatakiwa umuandae tena kwa anavyopenda yeye mfano unakazana kumpa ulimi kumbe yeye mshawasha wake upo kwenye maziwa, au unakazana kumtekenya kumbe mwenzio anapenda umrambe kama nyoka.  

Ukiona amelainika angalia na kwa bibi nako kama njia inaruhusu fuso lipite?  sio kwenye uchochoro unakazana tu kupeleka jua akisikia maumivu kidogo tu starehe yote ya mapenzi huishia hapo hapo, ndio maana inasisitizwa sana kufyeka msitu kwani nao huchangia sana kuharibu mapenzi maana nyasi moja tu hukata kama wembe.

Wanawake wengi hawawezi kusema wanataka nini sijui ni aibu au nini sasa mwanaume unatakiwa ubahatishe yaani unamgusa kila kiungo chenye mshawasha kisha angalia wapi anaguswa zaidi.  Au ye mwenyewe huenda akakuambia labda umshike kiuno usipuuze mshike huku ukikichezea sio ushike kama kinataka kuanguka huenda ndio mshawasha wake upo hapo.

Kabla ya kumaliza mwanaume muulize mpenzio kama yupo tayari mmalize wote au hata akitangulia we ukamalizia kwani akiwahi kumaliza mwanamke haina shida we pia utamaliza lakini we ukimaliza ni shida sana kwa mwanamke kwani wanaume wengi wanakuwa hawana uwezo wa kumsimamisha fupi bali ndio anazidi kulala.

Nawe mwanamke kama utatangulia kumaliza inabidi ujitahidi kuficha uchovu wako ili mpenzio nae apige goli zuri kwani ukimuonyesha dalili kuwa umemaliza basi ye nguvu ya kumaliza vizuri anakuwa hana kwa sababu anategemea masham sham yako ili mashetani yapande na kisha yatoe salaam.

msipoyaweza haya kati yenu mmoja kuchepuka ni kawaida sana kwa sababu raha ya mapenzi uyafurahie sio ufanye ili mradi utimize wajibu hata mzuka hauji.


yafanye mapenzi yawe asali na sio muarobaini.

Friday, March 7, 2014

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI



Mama Salma Kikwete 
Ni mfano bora wa wanawake kwa jinsi anavyowapigania watoto wa kike


Nawatakia heri wanawake wooote duniani katika kusherehekea siku ya WANAWAKE DUNIANI
Ingependeza baba ukampikia mama akajisikia kula chakula chako jamani, ukamtoa out, akafurahia vizuri hii siku yake.

WAKATI MWANAMKE WA MJINI  ANAPATA MUDA WA KUFANYA HAYA


Kuvaa nguo za heshima kwake joto


wengine hufikia kumkosoa Mungu wakaamua kujiumba upya mpaka wakawa kama hivi.


Haya hebu tumwangalie mwanamke wa kijijini na hii SIKU YA WANAWAKE  kama ina maana kwake kweli.

asubuhi na mapema ye safari ya shamba inaanza



shambani anafanya kazi jua/mvua yake na mtoto mgongoni


akitoka shamba lazima abebe kuni mtoto mgongoni jembe mkononi


mtoto anaumwa ajue jinsi gani ya kumtibu


maji anafuata maili kadhaa




vikiiva shambani avune



kisha muuzaji wa mazao ni yeye

OLE WAKE PESA ISIONEKANE NYUMBANI



anapigwa kama mwizi


anarushwa huko na mateke kama yuko vitani


wengine wanafikia mpaka kupoteza viungo vyao masikini


 Si ajabu ukakuta ana ndala kama hizi mwenyewe ndio anaenda kuuzia mazao




SERIKALI NA WADAU MBALI MBALI MSISHEREHEKEE HII SIKU KWENYE MA UKUMBI YA KIFAHARI MWANAMKE HALISI NI HUYU ANAETESEKA HUKO VIJIJINI

MAANA KUNA SHEREHE KILIMANJARO HOTEL SIJUI DIAMOND JUBILEE, HIVI HUYU MWANAMKE WA KIJIJINI ATAPATA JAPO KUSIKIA KITAKACHO ONGELEWA?

TUSIDANGANYANE


Toa maoni yako

Thursday, March 6, 2014

Mwanamke ajuaye mahaba

Assalaam alaykum wapendwa,

Baada ya kusema sifa za mwanaume wengi wenu mmeniomba niseme na mwanamke haya tuwemo basi

Mwanamke ajuaye mahaba huwa sifa hizi







  • huwa  hana tamaa na vitu visivyo na lazima.
  • hutunza siri na mali ya mumewe.
  • huridhika na kipato cha mumewe hata kama kidogo kiasi gani.
  • hushukuru kwa chochote anachopatiwa na mumewe hata kama hajakipenda.
  • huomba msamaha pindi akoseapo na kuahidi hatorudia tena kwa lugha laini na upole.

  • kila siku huhangaika kujipamba kwa ajili ya mumewe ikifika jioni mwenyewe shurti apambe chumbani kwake, ajipambe mwenyewe kwa  kanga nzuri na hasa ikiwa ina weupe, udi, pafyumu, poda, wanja, lipstik, nywele unazibana mtindo wa kupendeza, macho unaweka eye line, n.k 

  • Bwana akirudi kazini hupokelewa mzigo, pole na kiss kidogo kisha akampambua nguo zake, akaenda muogesha mwenyewe maruhani yakipanda huko bafuni aah anampa kigoli kimoja aondoe uchovu. Wakitoka huko anamkaribisha mezani na hapo anakuwa ameandaa tunda kwanza ampe mumewe kisha ndio ampe chakula tena tonge la kwanza shurti alishwe kisha aendelee mwenyewe.   kama kuna samaki basi mke humchambulia miba mumewe, huku akimuongelesha maneno mazuri ya mahaba.

  • Kitandani mwanamke huyu hujituma kwa ujuzi na maarifa yote kwani hasubiri kuguswa mwenyewe hujishughulisha kwa makiss, akamgusa mumewe kunako, akachezea panapo, huku akimbembeleza mumewe kwa mahaba, macho huyarembua kama mdoli, mwili wake huwa laini kila ashikwapo hunyumbulika kama ngano.

  • kwenye majamboz huwa mwepesi wa kubadili style, kiuno kama kafunga feni, huku akilalamika kwa utamu wa mahaba na kichozi cha uchokozi humtoka.
  • Hashushi mlima mpaka aone mumewe ameridhika na kumuomba naye afanye hivyo, kisha humlaza mumewe kifuani apumzike huku akimbusu na kumpa pole.
  • humshukuru mumewe kwa mahaba aliyompa na kisha humsafisha na kwenda oga tayari kwa kulala au kitu kingine 
  • Hata audhiwe na vipi na familia ya mumewe hawezi kumwambia mumewe kwani anajua ataharibu udugu wa mumewe na kuharibu furaha yao ya siku hiyo na hataweza faidi mapenzi.
  • hulegeza sauti pindi aongeapo na mumewe tena huwa mpole na msikivu.
  • asubuhi humuandalia mpenzi/mumewe nguo za kazini,viatu na sox kisha humuamsha taratibu  kwa mahaba ili mumewe asichelewe kazini.
  • anapokuwa na shida ya pesa huomba kistaarabu na akiambiwa hazipo au asubiri wala hanuni.
  • hana muda wa kupiga umbeya wala safari zisizo na kichwa wala miguu muda wote huutumia kuandaa chakula na mahitaji ya mumewe pindi arudi kazini.   


 



  • sala na maombi yake huombea ndoa yao na watoto wao wawe salama na wadumu milele.
  • Kila siku ndoa yako itakuwa mpyaaa na wala kidudumtu haingii
ukiyafanya haya mwanaume habanduki wala mzizi hauna nafasi kwako.

ni hayo tuu 

Tuesday, March 4, 2014

MWANAUME MJUZI WA MAHABA

habari zenu wapendwa 

Leo tuangalie jinsi wanaume wanaojua kupenda jamani anakupa raha mpaka unahisi wazimu.


  • humpenda mkewe/mpenziwe wazi wazi wala hafichi mahaba yake hupenda watu wajue kuwa yeye anampenda.
  • huwa mkweli na muwazi siku zote na akikosea huomba msamaha kwa upole.
  • huwa mpole kwa mke/mpenzi wake hata kama kwenye jamii ni mkali na wanamuogopa.
  •  huwa na huruma sana mfano mkewe akiumwa huwa   anahaha kutaka mkewe/mpenzi wake arejee katika hali ya uzima.
  • hufanya vitu vinavyomfurahisha mkewe/mpenzi wake kama kurudi nyumbani mapema, zawadi, kumtoa out n.k.
  • humsaidia kazi za nyumbani ili mkewe/mpenziwe asichoke kupita kiasi.
  • humfanya kuwa malkia ndani ya nyumba kwani mkewe/mpenziwe hung'ara  muda wote hata mbele za watu.

  • ni mtundu kitandani katika kumuandaa mkewe/mpenziwe na hana papara ya tendo mpaka aone amewiva maji anayaita mma.

  • hujitahidi kwenye majambozi kumridhisha mkewe/mpenziwe mpaka amalize naye ndio hushusha mlima.
  • huwa na mahaba mazito kiasi hata mkewe/mpenziwe atongozwe na nani huwa hana shida ya michepuko.
  • hupenda kuwa baba wa familia bora na si bora familia.

  • hufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya familia yake na hajishughulishi na michepuko.
  • daima hupenda familia yake iishi maisha mazuri na sio ya tabu aliyopata yeye.
Sio mwanaume mzuri kwa muonekano ndani ya nyumba yako wanakuona kama shetani vile maana huna unachofurahisha hata kimoja.





Toa maoni yako,