Thursday, March 13, 2014

Urafiki na Mapenzi

Assalaam alaykum wapendwa  wasomaji wangu,

Leo hebu tuongelee mapenzi na urafiki.




Rafiki ni mtu mzuri sana na husaidia wakati mwingine kuliko hata ndugu wa damu.
Hujitoa sana na hasa kwenye matatizo huwa mstari wa mbele mpaka tatizo linapoisha.
Pia rafiki huwa hajali kuwa wewe si ndugu wa damu bali hukutanguliza mbele kwa raha na shida.

Urafiki huu hudumu na kuwa mzuri sana kama nyie wote mkiwa hamjaoa/hamjaolewa, inapotokea mmoja kaoa/kaolewa hapo ndio utata unapoanza.

Kwa wanaume huwa mnakosea kumwamini rafiki mpaka kwa mkeo, wengi sana wamekutwa na mikasa ya marafiki kutembea na wake zao.

Unapokuwa umeoa lazima kuwe na mipaka mfano:-

Muda wa kuja rafiki nyumbani 
Rafiki aje nyumbani wewe mwenyewe ukiwepo, tena mchana na mkeo awe katika hali ya kawaida, sio anapenda kuja nyumbani we haupo au mida ya jioni ambapo mkeo kajipara kapendeza ana vikanga vyake viwili kavaa mwenyewe kwa ajili ya mumewe tahamaki rafiki huyu hapa, anamuona mkeo alivyopendeza roho inamruka anaanza kumsarandia mkeo ukiwafumania unampa mkeo talaka kumbe we ndio ulisababisha.

Au kila ukitoka rafiki ndio anakuja unapata salaam tu rafiki yako alikuwa hapa, kwanini umruhusu rafiki awe anakuja we hupo anaongea nini na mkeo.  Kwani hata kama huyu ni rafiki yako lakini na huyu ni mkeo sio mke wenu.  Rafiki aje nyumbani apikiwe ale akae atazame TV we hupo mmmh kweli.

Sehemu za kuwa pamoja na rafiki

Kuna sehemu mnaweza toka na mkeo na rafiki pamoja, tena mkeo asivae nguo za mitego wala asijipare sana, muda wote hakikisha upo pamoja na mkeo kwenye kutembea, kukaa, kama upo club hakikisha unacheza nae mwenyewe, sio unamruhusu rafiki akashike kiuno cha mkeo shanga alizovaa azihesabu.
Wakirudi kukaa wanaanza kukanyagana chini ya meza we huna habari 

Mkiwa nyumbani mara simu zinapigwa na rafiki kwa mkeo  ukiwepo rafiki anadai kapiga kwenye simu yako hajakupata.




Nimeombwa nitoe hii mada na mwanaume mmoja alikuwa na rafiki baada ya kuoa urafiki ukaendelea mpaka yeye na mkewe wamepata watoto wawili.
Sasa akaona mazoea yamepita kikomo akagombana na rafiki yake ndipo siri ikatoka kuwa hata wale watoto ni wa rafiki na baada ya ugomvi huo anawataka watoto wake alee mwenyewe, hivi kesi ipo mahakamani.

Mpooo wenye marafiki

ukiwa na chochote nimwagie hapa nami nitakitoa bila kutaja jina wala address yako 
niandikie kwenye MAONI/USHAURI 



No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako