Watoto wapo likizo tumia japo dakika 30 kuongea na mwanao hali ni mbaya
Vijana wadogo hawajajua hata maisha ni nini hayo mapenzi ya jinsia mbili hawajayafaidi hata robo wanaenda kuanzisha ya jinsia moja Mungu wangu.
Hivi natafuta nani aliyesababisha haya
ukimuuliza mzazi analia na utandawazi,
ukimuuliza Mwalimu analia na mzazi
ukiiuliza jamii wanasema mambo ya digital
wote wana makosa
Hebu tuanze na wazazi
asilimia nyingi hawana muda na mafundisho ya watoto wao, Baba kazini kurudi usiku Mama kazini kurudi jioni.
Mama akifika nyumbani humuuza dada wa kazi je watoto wamekula, wameoga, walikwenda twishen akiambiwa ndio basi huwaona watoto wasikivu sana tena huwapa na zawadi.
Tena wazazi wengine hufanya matendo ya aibu mbele za watu hadharani na watoto wadogo wakiwepo wakiona dhahiri shahiri.
Baba akirudi huuliza mwl kasema nini shule kama mchango anatoa wachache wanaopitia hata daftari za mtoto, ye anachojua ni ada na mahitaji ya shule ya mtoto.
Lakini hawakumbuki huyu au hawa watoto wanatakiwa wahubiriwe nini maisha, wawe na tabia zipi, watakuja kuwa nani mbele ya safari tena unawapigia na mifano hai ya watoto watukutu nini kimewakuta na wakiwa watoto bora watafanana na nani. huo muda wazazi wa sasa hatuna.
Mwalimu
Zamani mwl. alikuwa ni mzazi wa pili kiasi ukiwa naye unahesabu kama una mzazi wako na hata ukifanya kosa lazima atakuonya na ukizidi anawaita wazazi wako ili wamsaidie kukuonya kwa kosa unalofanya, na usiposikia unafukuzwa shule.
Sasa mmh waalimu baadhi yao wanajali maslahi yao na nimeshuhudia shule moja hapa dar st. fulani [jina kapuni] mwl. kaachishwa kazi kwa kumfuatilia mwanafunzi mwenye utovu wa nidhamu, akiambiwa alipaswa amheshimu yule mwanafunzi kwani ndie analeta mshahara wake.
Sasa watoto wetu wanaokwenda ma boarding ndio kabisa jamani kuna tabia za ajabu sana usagaji ma ushoga wanauanzia huko.
Haya jamii nayo
Badala ya kumlea huyu mtoto hasa wanaume mnaovivua chupi vitoto vya kike mnapata raha gani kwao jamani.
Mzazi mwenzio kagharamika masikini anajinyima kula na kuvaa vizuri kwa ajili ya huyo mtoto unaamua na makusudi kumuharibia mwanaye kwa pesa na magari yako ya kifahari, tena nawe umezaa na una watoto wa kike hufikirii je ukimkuta mwanao ndio anafanyiwa hayo utajisikiaje.
Ukisha mharibia masomo yake unamtelekeza nyumbani nao kwa uchungu wa pesa zao na fedheha wanamfukuza nyumbani basi maisha na ndoto zake vinaishia hapo masikini.
Leo tunakataa ushoga kwa maneno lakini kivitendo umejaa tele hao wasagaji ndio usiseme yaani akili zetu ni kama yule anaejisaidia porini uso, anauelekeza njiani ili watu wasimchungulie mgongo anauelekeza porini hajui kama akitokea simba nyoka au mnyama yoyote wa hatari aka ye hataki watu tu wamuone.
Tukumbuke SODOMA NA GOMOLA waliangamizwa na Mungu sehemu ile mpaka leo haioti hata nyasi.
Kuna haja ya kumrudia Mungu kila mtu kwa imani yake tena na watoto wake awasisitize elimu ya dini labda tutaokoa vizazi vyetu jamani.
Toa maoni yako

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako