Furaha ya ndoa hainunuliwi dukani, haitafutwi kama pesa wala haichimbwi kama madini.
Basi tunaipata wapi furaha ya ndoa?
kufunga ndoa ni jambo moja lakini furaha ya ndoa ni jambo lingine hivyo usitegemee ile furaha ya siku ya ndoa itakuwa milele.
Furaha ya ndoa mtaitengeneza wenyewe mume na mke ndani ya nyumba kwa:-
N.B Jamani mwenzenu najitolea kutoa elimu hii si kwa sababu najua sana au ni mfanyaji sana wa haya mambo mi ni mtu mzima na heshima zangu kamili. Sasa baadhi yenu comment mnazoniletea nyingi hazina maadili, wengine mnatongoza, wengine mnauliza maswali hayana msingi, hii sio blog ya kikubwa ndio maana natumia tafsida kuongea baadhi ya vitu humu, hivyo nikaona bora nisirushe comment zenu nazisoma na kuzifanyia kazi.
Kwa wale mliouliza kwanini sirushi comment zenu jibu ndio hili endeleeni tuu kuelimika mpaka nitakapoona mmetumia lugha nzuri.
kufunga ndoa ni jambo moja lakini furaha ya ndoa ni jambo lingine hivyo usitegemee ile furaha ya siku ya ndoa itakuwa milele.
Furaha ya ndoa mtaitengeneza wenyewe mume na mke ndani ya nyumba kwa:-
- kudumisha mahaba kwa kila mmoja wenu kila siku ajitahidi kuongeza vionjo.
- kuvumiliana kwa kutambua kuwa kila mmoja weenu ana tabia ambayo mwenzie haipendi ila anavumilia.
- kusameheana kwa makosa madogo madogo kwa kujua kuwa nyie ni binaadamu hamjakamilika hivyo unasamehe na kufuta kwenye akili kama kilitokea nini.
- jaribu kumfanya mwenzio ni mpya hata kama mmeishi miaka mingapi.
- tengeneza furaha ya mwenzio kabla yeye hajatengeneza ya kwako ina maana mpendelee mwenzio kwa kumfanyia vitu anavyo vipenda kabla ya kudai kufanyiwa wewe.
- wazazi, ndugu na jamaa hawana nafasi ndani ya mapenzi yenu wao ni washauri tuu pindi yakiwashinda kutatua nyie wawili.
- Watoto wasiwe nguzo ya mapenzi yenu mkaishi eti kwa sababu mmezaa mnatakiwa kuishi kwa mapenzi na sio kwa kizazi
- kauli njema ni kitu muhimu sana kinachodumisha furaha ndani hata kama kuna hitilafu kiasi gani hupozwa na kauli njema ya kila mmoja wenu
- thamani ya kila mmoja wenu inahitajika kwani dharau ni moja ya vitu vinavyobomoa mapenzi mpaka mkaishi kama maadui wakati mlikuwa wapenzi.