Wapendwa wasomaji wangu Assalaam alakum
Sijasema watu wasisome au wasipende na hasa sie wadada
Zamani binti alikuwa anakatishwa masomo au anakatisha mwenyewe anaamua kuolewa. Na wengine walisoma wakapata na kazi baada ya kuolewa mume akamuachisha kazi au mwenyewe akaamua kuacha kazi.
Sio wote walikuwa wajinga hapana bali kuna wengine walizidiwa na mihemko wakaona wasiwape fedheha wazazi wao kwa kubeba mimba pasipo ndoa au kuonekana malaya mbele ya jamii.
Na wale waliokuwa wanaachishwa kazi na waume zao ama waume waliona mwenendo wao uliathiri mazingira ya ndoa zao, kwani huenda mke kazi yake ni ya kutoka jioni au usiku na akawa anashindwa kutimiza wajibu wa nyumbani kwake, wengine walikuwa wanachepuka waume zao wakagundua.
Au mke anachoka na kazi za ofisini kiasi anashindwa kuitendea haki ndoa yake maana akishikwa kitandani wimbo wa nimechoka unakuwa mdomoni.
Sasa Mwanaume uwezo wa kumtimizia mkewe anao anaamua kumuachisha kazi ili kuinusuru ndoa yao.
Au mwanamke mwenyewe anapoona majukumu ya kazini na ya nyumbani yanamshinda na hasa anapokuwa na watoto basi mwenyewe akiona mahitaji ya nyumbani mumewe anatimiza anaona bora akae alee familia yake na ndio tukatoka watoto bora leo ambao tunajivunia malezi bora.
Kimbembe zama hizi
Wadada wengi tunajitahidi kusoma haswaa na nitoe hongera sana kwa hilo,
Na nakubali kabisa ukimuelimisha mama umeelimisha jamii nzima.
Lakini linapokuja suala la mapenzi tunafeli sana kwanini,
Kwa sababu tunaiweka elimu ya darasani mbele kuliko elimu ya maisha, hatutaki kukaa chini tukawauliza wazee wetu kwanini wamedumu kwenye ndoa zao tunawaona washamba hawakusoma kama sie. Tunasahau wao wana elimu ya maisha ambayo huipati popote isipokuwa kwao.
Pia hatutaki kujishusha mbele ya waume zetu hatujui hata lugha ya kuongea mbele ya mpenzi wako, tena tunataka tuwe sauti ya mwisho utakalo taka lifanyike we ndio bibi mipango ndani ya nyumba mwanaume kazi yake kusema sawa. Ndoa tutaziona kwenye muvi haki ya nani.
Ukitongozwa tu basi unaanza kumuuliza maswali
anafanya kazi wapi
ana gari
amepanga apartment au upande mzima
Hee makubwa vinahusiana nini na mapenzi, ingekuwa hivyo masikini wasingeonja hata.
Haya ndio ana vyote unampa masharti
mara hutaki ndugu zake, kila wiki utoke out tena unamkusanyia na marafiki, bili ya salon, simu ya million.
Unadai yote hayo wakati kupika hujui, usafi ndio kabisa kwa bibi kuchafu, kuna uvundo na kutakosaje wakati chooni unatumia toilet paper kucha umeunga vidole vyote kwa bibi kutasafika na nini. Hata miguu yako mwenyewe akuoshe wa urembo.
Humjali mwanaume kwa lolote ila yeye akujali wewe tu, humfulii, humnyooshei nguo, humpi mapenzi matamu basi akaridhika hata kitandani, wewe na gogo la mbao hamna tofauti kazi makelele tu kama unakimbiza mwizi.
Ukiambiwa oh mi nina degreee zangu hanibabaishi mtu, aliyekwambia kitandani kunahitajika degree nani.
Tunakosa elimu ya maisha,hatuoleki, tunapata wanaume wa kutuchezea, akitaka kuoa anaenda kutafuta yule aloishia form four, au kijijini kwao anamleta mwenyewe raaaha mustarehe.
Matokeo yake tunachukua vijana wasio na kazi ya maana tunawafuga ndani nao kwa kuwa wanahudumiwa kila kitu kwao ndio. Unamhonga naye anahonga.
Sasa zama hizi kumkuta mdada miaka arobaini hajaolewa hata ndoa moja ni kawaida sana, lakini anajisoap soap aonekane msichana, kila birthday miaka 28, utafanyaje sasa, au ulipata wa kukuzalisha kisha yuleee anakukimbia, anabaki analea mtoto.
Usomi wako unafaa ofisini tu ndani ya nyumba we unabaki kuwa mwanamke mwenye majukumu.
Wadada wengi zama hizi tunaishi peke yetu haya ni majanga.
Kwa mwenye kupenda ukweli wala hakasiriki.
Tchaoo
Toa maoni yako