Friday, February 14, 2014

NDOA INA RAHA YA PEKE YAKE

                             

Jamani naomba niseme na nyie mnaojiita wapendanao miaka kumi na ushee mmekaa bila kufunga ndoa mnazaa watoto mpaka wanakwenda sekondari nyie bado mnapimana mnataka mpate futi ngapi?

Wengine mmeanza mapenzi tangu mko sekondari, chuo mpaka mmepata kazi bado hamjajuana tabia mnategemea mjuane kivipi wakati mnalala kitanda kimoja mnaamka pamoja mnashinda pamoja khaa nyie muogopeni Mungu basi duuuh.

Wengine mna pete za uchumba mpaka zimepauka ndoa haifungwi tangu mliitwa  watarajiwa mpaka watu wamewazoea.

Hebu kaeni chini mtafakari nini kimewazuia nyinyi msifunge ndoa, kama kuna kikwazo ni kipi na kinatoka kwa nani na kitaisha lini?
Kuishi bila ndoa ni sawa na wanyama kwani ndani hamna sheria hakuna anayeweza kumuwajibisha mwenzie kila mtu ana madaraka yasiyo rasmi.

kama wazazi wa upande mmoja hawataki mnafikiri wakifa ndio watakubali?

Kama tabia yake mbaya mwache atapata watakae lingana tabia unamzeesha wa nini wakati huna mpango wa kumuoa?

Wengine anakaa na mwanamke huku anatafuta mchumba taratibu akishakamisha mipango yake anasingizia wazazi wamemlazimisha kuoa, nyie wanaume wenye tabia hii muogopeni Mungu.

Wacha niwaambie ukweli,
Mapenzi ya kweli yanapatikana kwenye ndoa peke yake, humo mtapata furaha, haki, wajibu wa kila mmoja  wenu, sheria, baraka, fahari  n.k
Hata familia zenu zitakuwa na nafasi katika nyumba yenu katika shida na raha zenu.

Hakuna dini hata moja inayokubali watu waishi  bila ndoa.


                                                   


Wengine utasikia ooh tunajipanga kwanza kwani mtaishi maisha gani kuliko hayo mliyo nayo sasa,  mbona hamkusubiri kwenye ngono, mnaona sifa kujitangaza kuwa mnazini, mnataka harusi ya kifahari haijapata kutokea halafu iweje.
Hata mkienda kwenye nyumba za ibada hamuoni aibu kumkosea Mungu kwa sababu za kijinga.

Niko na wewe mdada uliyehama kwenu ukaenda kuishi na mwanaume ambaye hata hajajitambulisha kwenu, unadhani umewafurahisha wazazi wako?  hujui kama umewatia aibu familia yako wanashindwa hata pa kuweka sura zao, kila wanapopita wanachekwa kwa uliyoyafanya, haya mwenzetu  ukigombana na huyo mwanaume huwa unashtaki wapi.  Akikufukuza unarudi wapi au ndio safari ya maisha ya bila mwelekeo inaanza.

Umejirahisi sana kiukweli hata akikuoa ndoa haina msisimko kama ile ambayo ungetulia kwenu ukatoka na baraka za wazazi, vigere gere na nderemo. 

 Wazazi wakajifaharisha mbele ya jamii kuwa wanajua kulea mtoto wao katoka nyumbani na ndoa.


Bado hujachelewa rudi kwenu huyo mwanaume kama kweli anakupenda aje akuoe.

Ukiolewa unaheshimika, unaaminika, unathaminika popote pale si rahisi mtu kukufananisha na malaya wa barabarani.
Ona wivu shost  mwanaume anakuzeesha bila ndoa nawe unakubali tuu. 



Ni hayo tuu mpenda ukweli akiambiwa wala hanuni.


Toa maoni yako

1 comment:

  1. Wape vidonge. Kuoa ni kutamka kwa mdomo na ndani ya moyo kuwa uko tayari kuwajibika lakini kurukaruka bila ndoa ni upungufu wa hekima na wajibu kwa mtu unayemwita mwenzio. Kamwe huo si mpango wa Mungu.

    ReplyDelete

Toa maoni yako