Thursday, January 2, 2014

Hivi kuna Mwalimu wa Mapenzi? - TALK ABOUT LOVE

Assalaam alaykum wapendwa, 
Habari za mwaka mpya natumaini wengi wetu tumesherehekea kwa amani na utulivu.
Haya ni siku nyingine tena tunaendelea na mlolongo wetu wa safari ya mapenzi na leo, tunataka kumjua nani mwalimu wa mapenzi.

HIVI KUNA MWALIMU WA MAPENZI 
Asilimia kubwa ya wengi wetu ukiwauliza swali hili, hujibu hakuna shule ya mapenzi.
kwa upande mwingine wapo sahihi kwani ni kweli hakuna shule iliyo sajiliwa rasmi kwa kufundisha mapenzi.
Pia hudhani mapenzi ni ngono, wakati hilo tendo huwa ni sehemu ya mapenzi.

Haya basi mwalimu ni nani?
Mwalimu wa kwanza ni 
  1. Moyo wako
  2. jamii

MOYO
kwanini moyo?
Kwa sababu moyo unapopenda huwa ni mwalimu mzuri sana kwani
hukufundisha jinsi gani 
utabasamu ukiwa na mpenzi wako
 maneno gani umwambie
sauti gani utumie
na kingine ni muonekano uvaeje ili akikuona ataharuki 
haya huwa mwalimu wake ni moyo kutokana na jinsi gani unavyompenda,
Ingawa sio wote wanaojali ushauri wa moyo.

JAMII
Pia ni mwalimu mzuri sana wa mapenzi, kwa sababu utasoma kwa 

  • Kukopi kutoka kwa wazazi labda ulikuwa unamuona mama/baba anamfanyia nini mwenzie.  Na ndio maana ukipata mwanaume ambaye baba yake alikuwa mpigaji,mtukanaji asilimia kubwa naye huwa hivyo hivyo.
  • Majirani, Marafiki, kusoma majarida mbali mbali blog kama hivi inasaidia sana kuona kipi uchukue ambacho kitafanya mapenzi yenu yasonge mbele.
  • Kuna makabila ambayo hutoa mafunzo kwa lugha ya kibantu huitwa "unyago, kuchezwa, Ngoma au kwa kule kwetu huita msondo, kwa wanaume "Jando".   
Kusema kweli mafunzo haya yalisaidia sana kudumisha mapenzi na ndoa kwa ujumla, kwani waliokuwa kwenye mapenzi kila mtu alijua wajibu wake na mipaka yake katika mapenzi.
kwa sababu walengwa hujifunza jinsi ya kuishi na wenza wao, na malezi ya familia.
Ingawa mafunzo ya baadhi ya makabila yana dosari kama kufundisha wanawake kuwa na wanaume zaidi ya mmoja lakini asilimia tisini yana faida sana na ndio maana ndoa za wazazi wetu zilidumu na nyingine zimendeleea kudumu mpaka leo.

Tofauti na sasa mtu mpaka anaoa/anaolewa hajui chochote zaidi ya tendo la ndoa, utakuta   mkaka au mdada anaongea siri za ndani za mpenzi wake mbele ya marafiki, wafanyakazi wenzie, n.k. Mdada huyo sasa utamkuta anajifaragua,
  •  "Mie mpenzi/mume wangu ananipenda, mara kasema mwezi huu ananinunulia gari,
  •  likizo hii tutasafiri kwa ndege,
  •  nimemwambia abadilishe zile samani ndani wiki ijayo shost ukija utakuta mambo mapya,
  • Kwangu hafurukuti nimemweka kiganjani, niseme nini asitende
  •  kuna dili anafuatilia hilo la mamilioni shost akipata tu namwambia aninunulie nyumba.
 Tena anaona raha wenzie wanavyomsikiliza hajui sometime  anahatarisha hata maisha ya mpenzi wake. 

Mkaka nae
Duh washikaji demu wangu nampenda naye ananipenda sana, yaani nikimkumbuka kazi haziendi wangu, mtoto anajituma kitandani ile mbaya, kwanza alivyo hata nikitembea naye najiona kama sienei vile, halafu sasa kwao kuna pesa yaani hata ukimpa pesa hapendi anarudisha, ameshasema nikiwa na shida nimwambie atanipa kwani ana account tangu mdogo halafu hata hajaanza kuzitumia.

 Hivi nyumba ilivyojengwa ikakatwa vyumba, kukawekwa mlango na madirisha ilikuwa kwa sababu gani?wewe ambaye mambo yako ya chumbani unayaanika kama samaki ng'onda.

Halafu kesho unagombana ooh rafiki yangu kanichukulia mpenzi wangu, si umemchuuza mwenyewe kama nguo mnadani
Yote haya ni kukosa mafunzo, mwenye mafunzo huwezi kumkuta ana haya mambo
Au wengine akikosana na mpenzi wake watu wote wanao mzunguka watajua, jinsi atakavyojitapa na maneno ya kashfa 
  • Oh yule bila mimi asingekuwa vile, 
  • Kwanza nimemsomesha, wazazi wake masikini mimi ndie niliyekuwa nawahudumia
  • Alikuwa hajui hata kuvaa 
  • Kwanza hajui usafi nilikaa naye basi tu
  • Muda wote sikuwa hata na raha bora tulivyoachana
  • Hivi yule nae mwanaume/mwanamke kweli wakiitwa wa aina yake nae atatoka
  • Mtu gani asiye na fadhila.
Na mengine mengi mpaka kutoleana siri za maungoni, ili iweje, unapata faida gani, unao waambia wakishajua wamfanye nini?

Mpenzi msomaji wangu, sababu 
Ni kuingia kwenye mapenzi bila kuyajua hasa wanawake, kisha unakuwa kichwa cha umbea mtaani, wakikuona tu wanakuita kwa bashasha ili uongee ya kwako, wengine watakupa ushauri mbaya unajikuta unaanzisha migogoro ndani isiyo na kichwa wala miguu, unaondoka kwenye ndoa yako na kuwaacha watoto wanateseka, kisha alokushauri uondoke ye ndie anakurithi. 

Wengine wanakushauri kwenda kwa waganga wa kienyeji

Aliyekuambia kuna dawa ya mapenzi nani?  
Kwa mganga  unapewa dawa kamuwekee kwenye chakula mumeo matokeo yake anakuwa zuzu, kila utakachofanya anakuangalia tuu, hana ushauri ndani, majukumu ya kulea familia yanakukabili peke yako kwani ye hata kumkanya mtoto hawezi anakusukumizia wewe, unaanza kulalamika tena mitaani kuwa hakusaidii majukumu, na wakati ulipokuwa unamwambia mganga "nataka afunge mdomo wake, mimi ndio niwe mwenye sauti, na kila ninalomwambia atii,"  
si kanyamaza sasa uone familia inavyokuharibikia hivi hivi unaiona.

Dawa ya mapenzi ni ulimi na uhodari wako katika kufanya yale yanayomfurahisha mpenzi/mume wako.
Hiyo midawa mnayopewa ni kuwatafutia maradhi tuu watoto wa wenzenu.
Na yote hii hutokana na kutopenda kuambiwa kweli, ukikosea hutaki kuomba msamaha, unalotaka lazima lifanyike, kutaka wewe ndie uwe mwenye sauti kuu ndani ya nyumba, mwenzio ashindwe hata kuwasaidia wazazi wake.  Huu ni ushetani mkubwa sana unachangia sana kuvuruga familia.

Naomba niishie hapa kwa leo,
Wapenzi Wasomaji wangu nimepokea maswali yenu, maoni ushauri nawashukuru sana kuona ninachojitahidi kukidadavua hapa kwa kiasi kikubwa naeleweka.  
Endeleeni kunitumia na ipo siku nitayajibu hapa hapa bila kutaja majina wala email zenu.

ahsanteni sana tuonane mada ijayo








No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako