Tuesday, January 21, 2014

KWANINI HATUWEZI KUISHI BILA MAPENZI

Habari za long weekend nadhani inaendelea vyema samahani kwa kukosa mada siku zilizopita ilikuwa ni nje ya uwezo wangu, nimerudi sasa naomba  tuendelee

KWANINI HATUWEZI KUISHI BILA MAPENZI

Mwanzo kabisa nilisema mapenzi yana roho yanaishi kama kiumbe hai, kwa sababu hebu fikiria mara ya kwanza unapopenda huwa unakuwaje, 
kisha kadiri siku zinavyoendelea inakuwaje 
na je penzi likifa ghafla inakuwaje

Hivyo ni kawaida ya kiumbe chochote chenye uhai kuwa katika mapenzi si wanadamu tuu hadi wadudu warukao na watambaao.
Naweza kusema ni mpango wa Mungu kwa kweli, kwani mtu yeyote asipokuwa katika mapenzi hujiona na mapungufu flani yaani kama hujielewi au dunia imekutenga kama hivyo.
Hata kiafya na kiakili pia mapenzi yanahusika kukufanya uwe na akili timamu na afya njema huwezi kuumwa hovyo hovyo mara kiuno au nyonga kwa wanawake.

Pia mtu anaposalitiwa huumia sana na kuiona dunia chungu hata kama ana mali na fahari vyote kwake si kitu hupelekea kujiona hafai tena mbele ya jamii  mpaka kufikia kujidhuru au kumdhuru mpenzi wake.

Pia hata kama ana  kisomo, cheo, au familia inamtegemea kiasi gani kwake huwa haina maana kama ameumizwa kwenye mapenzi.

Mapenzi yanaweza mbadilisha mtu tabia mpaka watu wakamshangaa  mfano labda alikuwa mwenye roho nzuri kwa familia na jamii baada ya kuingia kwenye mapenzi misaada na ule upendo aliokuwa anauonyesha kwenye familia hufa, akawa anamsikiliza mpenzi wake tuu.

Mapenzi hupelekea wengine kukosa radhi za wazazi wao, kugombana na ndugu zao mpaka wakashindwa kuzikana.

Mapenzi hufanya watu wakafukuzwa kazi, wakahama kila nyumba, wakashindwa kuishi na majirani vyema, wakawa na maadui wengi katika jamii.

Juu ya yote hayo bado watu wakaendelea kupendana bila kujali yote hayo.

AMA KWELI MAPENZI NI KITENDAWILI

Mpenzi msomaji wangu nadhani leo tumemalizia maswali yote niliyoyauliza kwenye somo letu la kwanza kabisa kuhusu mapenzi.

Naomba uhai na uzima ili tuendelee na mambo yahusuyo mapenzi mi si mjuzi sana ila napenda kushare nanyi nikijuacho kuhusu MAPENZI.
Tchao




Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako