Ni siku nyingine tena wapendwa wasomaji wapendwa, natumaini mu wazima.
NANI ANASTAHILI KUPENDA?
Unapoingia kwenye mahusiano lazima ujiulize swali hili, maana wengi wetu hupenda kulaumu upande mmoja yule hata hanipendi.
Sote tunastahili kupenda tena kwa moyo na ndio maana hata mbele ya za watu unapotaka kufunga ndoa ya aina yoyote ile lazima uulizwe kama umempenda na uko tayari kuwa nae. Na hakuna sehemu hata kwenye vitabu vya Mungu palipoandikwa alazimishwe mtu kupenda, huwa ni baadhi ya mila na desturi tena zamani siyo sasa sidhani kama taratibu hizi bado zinafanyika. Kwanini suala hili hata Mungu hakutaka lilazimishwe?
Kwa sababu bila kumpenda hutaweza kuishi naye kwa amani. Na kama kukikosekana amani ndani basi jua:-
- hamtaweza kuwa na maendeleo kwani hamtaweza kushauriana kila mtu atakuwa na lake.
- mtasumbua vizazi vyenu kwani hamtakuwa na sheria ya pamoja jinsi ya kulea watoto wenu.
- kama mwenzio ana mapenzi ya kweli atateseka kwa sababu hatapata upendo mzuri kutoka kwako.
Hivyo epuka sana kuingia kweye mahusiano bila ya kuwa na mapenzi ya kweli kwani yatakutesa hata na wewe mwenyewe hutakuwa na furaha, matokeo yake kila mtu anatafuta mpenzi wa nje wa kumpa furaha, mnabaki ndani ya nyumba mnaishi kama jela, karaha mtindo mmoja.
Katika suala hili la kupenda mara nyingi wapendaji na wanaume, kwani wanawake hupata fursa ndogo sana ya kupenda na kuishi kwenye pendo. Kwa sababu katika mila za kiafrika mwanaume ndie anaetafuta anayempenda na akimpata hasiti kumwambia.
mwanamke yeye hata kama akimpenda mwanaume hawezi kumwambia, na hata akisema asilimia kubwa huishia kudharauliwa na kuonekana ni malaya, pia mwanamke kaumbwa na aibu hasa katika masuala ya mapenzi.
Hivyo hata kama anapenda masikini huishia kuonyesha upendo, ukaribu, ucheshi, huruma kwa yule ampendae bila kuwa na matumaini kama hayo ayafanyayo yatakidhi matakwa yake.
Mwanaume nae akiona unamfanyia hivyo basi kama hana imani hujidai anakupenda akishafanya ngono nawe, anakutupa huko bila kujali atakuumiza namna gani. Wengine hufikia hata kukutangaza mbele za watu kuwa wewe ni malaya unayejitongozesha kwa wanaume, kumbe masikini ulikuwa na upendo wa kweli kwake.
Baada ya kutendwa mwanamke huyu atakacho ona bora kwake ni kugawa dozi ya maumivu kwa kila mwanaume atakaye jileta kwake, matokeo yake anakuwa malaya kweli wakati mwanzo hakuwaza wala hakutaka kuwa hivyo.
Kwa mwanaume naye vile vile tena wao ndio wanaumia sana.
kwanini?
kwa sababu wao wanahangaika kutafuta mwanamke ambaye anampenda, katika kutafuta huko hutumia pesa, zawadi mbali mbali, kumtoa matembezi ya jioni, kutafuta maneno ya mapenzi ambayo yatamvutia huyo mwanamke ili amkubali, hubadili muonekano wake ili aendane na huyo ampendaye, wengine hufika hata kukodi mavazi, magari kujiongopea anaishi sehemu nzuri au kazi yenye hadhi ili tu ampate ampendae.
Na hili la kuongopa linawaharibia wanaume wengi sana akimpenda mwanamke eti kuna msemo kuwa huwezi kumpata mwanamke mpaka umwongopee,
Wewe usijidanganye kwani inawezekana kuwa kabla hujamtamkia huyu mwanamke unampenda yeye pia alikwisha kukupenda. Hivyo ukimtamkia hufurahi moyoni kuwa njozi zake zimetimia kwa kumpata ampendae.
Sasa ukianza kumuongopea madai yako ili akupende ndio unaharibu kabisa kwani akigundua utakuwa adui yake namba moja. Utamkosa na kujuta lakini ndio hivyo tena majuto ni mjukuu.
Hivyo kupenda ni kwa kila mtu anatakiwa ampende mpenzi wake, na awe mkweli sio kujitapa ooh nimesoma Marekani na Canada, nina DEGREE NANE,MASTER SITA, PHD, jamani mapenzi na hayo mavyeti yako wapi na wapi.
Mie nikiwa nawe hutojuta nina nyumba nane nimepangisha wazungu magari ya kifahari, harusi yetu tutafunga angani, wakwe nitawapeleka UK shopping, wewe ndie utakuwa msimamizi wa mali zote hizi, hebu sema unataka nini tena. Hee unaoa mke au supervisor? Ingawa si vibaya lakini isiwe ndio kigezo cha kukubaliwa.
Hivi mapenzi yangeendana na utajiri, masikini si angekufa bila kutongoza, asikudanganye mtu mapenzi hayachagui kisomo wala pesa, yule aliyekugusa moyoni ambae ukimuona moyo unawaka kwa furaha na usipomwona hujihisi ugonjwa usio onekana hospital zote, basi huyo ndie anastahili uwe nae. Na ndio unastahili kumpa mapenzi yako ya dhati.
kwa leo nitaomba niishie hapa,
kwa maoni/maswali/ushauri niandikie kupitia mkono wako wa kulia pameandikwa MAONI/USHAURI itakuwa siri yetu na nitakujibu kwa njia hiyo hiyo ya email.
AHSANTENI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako