Thursday, January 9, 2014

Nani anastahili kupendwa? TALK ABOUT LOVE

Hellooo
wapendwa wasomaji wangu natumaini weekend ilikuwa poa mi pia kwangu ilikuwa shwari 
tuendelee...........
NANI ANASTAHILI KUPENDWA?
Nadhani wote tuna jibu moja kuwa wote tunastastahili kupendwa, jamani kupendwa raha sana asikwambie mtu, hujiona uko kwenye ulimwengu wa peke yako moyo unachanua kwa furaha.

KWANI KUPENDWA NI NINI
Ni kule kudekezwa, kupendelewa, kuchaguliwa, kubembelezwa kama mtoto, n.k.

KWA NINI UPENDWE?
Hapa sasa majibu yake lazima yawe tofauti
kwani kila mtu ana sababu iliyomfanya apendwe, na kama kungekuwa na sababu moja au mbili basi kuna watu wangekufa bila kupendwa.

Unaweza kupendwa kutokana na 
  1. Tabia yako njema 
  2. uzuri wako sura au umbo
  3. umaridadi wako katika uvaaji au mazingira unayojiweka
  4. ucheshi wako 
  5. sauti yako 
  6. umaarufu wako n.k.
Kwa upande wa wanaume wenye akili asilimia nyingi hupenda tabia, yeye anaweza kuwa malaya kweli kweli anachezea watoto wa watu kama aliwaumba yeye lakini akitaka kuoa anatafuta mwanamke mwenye tabia njema.

KWANINI
kwa sababu mwanaume mwenye akili anajua kuwa kuoa ni kuanzisha familia na ukoo sasa ili familia iwe na sifa nzuri katika jamii basi lazima apate mke bora, mwenye tabia njema.

Sio mke asiyejijua yeye ni nani ndani ya nyumba, siri za ndani anamuhaditia hadi mfanyakazi wa ndani tena usikute mdogo ki umri, nyumbani kwake akiwepo sawa asipokuwepo wala hakuna tofauti, kisha utake kupendwa utasubiri sana.

JE UNAJUA KAMA UNAPENDWA?
Labda tuseme ndio, je unajua anachokupendea? Au ili mradi tu ukiletewa zawadi, au akikuchekea  basi mwenyewe unaridhika kuwa unapendwa?
Chunguza vitu gani anapenda wewe uvifanye, na ni rahisi tu mfano:-
Chakula ukipika wakati wa kula muulize- vipi chakula kizuri eeh?  majibu yake yachunguze anaweza akajibu kwa mmh, au ndiyo, au naye akauliza kwani kapika nani, na utakapo mjibu ni wewe basi anaweza kukushauri cha kuongeza au kupunguza. Au akakifurahia sana chakula, akakisifu kuwa kizuri.

asikudanganye mtu uchawi wa kwanza wa mwanamke kwa mumewe/mpenziwe ni mapishi, mnapoteza pesa bure kwa waganga wa kienyeji dawa unayo mwenyewe.   Mapishi bi dada leo umepika hiki kesho kile, sio kila siku mchana ugali usiku wali mmh na mapishi ndio yale yale akipata wa kumbadilishia mlo kwako bai bai.
Maandalizi ya chai, tena  chakula cha asubuhi wengi sana tunafeli, mwanaume umekazana kumlisha vitafunwa vya kununua kama maandazi, chapati,mkate bajia n,k.
Hivi we kupika huwezi kweli, haya siku za kazi zinajulikana weekend je, mnashindana kulala mpaka msaidizi akugongee chai tayari, je ungeamka mwenyewe ukaiandaa kisha ukamkaribisha mumeo kwa sauti nyororo ataacha kukupenda kweli?
Kingine usafi jamani mwanamke barabarani alivyojipamba kama mdoli, mmh nenda kwake hasa chumbani hapafai, ukimuuliza atasingizia muda hana lakini wa kukaa kujipamba kwenye dressing table saa nzima anao. Au ndio msaidizi ataitwa afagie adeki chumbani kwako mwanamke looh kesho ukimkuta kitandani na mumeo toka taratibu ukashushie juisi.

Haya usafi mwingine wa mwili na huu ndio wengi wetu sijui hatuujui au ndio makusudi,  mwanamke unayejua maana ya usafi utaweka makucha kama shetani vidole vyote utajisafishaje?  Au ndio toilet paper hapana mwanamke yake maji bwana, wanawake tuna vumba afadhali ya samaki sangara, usipojua kujisafisha utasema una nuksi, kwani mwanaume atakufuatilia kwa mbwembwe akishafanya ngono nawe mara moja tuu hana hamu na wewe tena, na alivyokuahidi atakufanyia vinaishia hapo hapo.
hakupendi tena.

Kingine jamani mautundu kunako majambo wote lazima muwajibike na mfurahie lile tendo, hasa mwanamke kila mara  unatakiwa uwe na utundu mpya, hata chakula kila siku ugali maharagwe jamani si atavimbiwa.
utapendwa kweli.
mmh mengine tuulizane pole pole jamani  humu hapafai.

KWA WANAUME.
asilima nyingi wachafu, wabishi na wabinafsi sana.

UCHAFU
Mwanaume na mazingira ya usafi ni wachache sana wanaoweza, kwani ule mfumo dume unawaumiza sana. utotoni alikuwa anafuliwa nguo ananyooshewa, akirudi shule anatupa uniform dada yake kama anaye au msaidizi wa ndani aokote akafue na wengine walikuwa wanafuliwa na mama zao.

Sasa wakioa mwendelezo unakuwa vile vile, usipomwangalia anaweza soksi akavaa tuu mpaka zikanuka kama anatembea na maiti ya panya.  Shati siku mbili tatu analo tuu, wengine hata nguo ya ndani umfulie laa sivyo atavaa tuu.
Mwanamke kama alisafiri akija rudi badala ya kupumzika na uchovu wa safari atafikia usafi na uchovu wote utaisha jinsi chumbani atakavyo pakuta.
Hamu na mapenzi aliyokuja nayo mwanamke huyu yote yanaisha, halafu akupende never.

Kero ndani jamani kuna wanaume wana gubu ndani ya nyumba mpaka chefu, kadogo linakuwa kubwa, mwanaume anasema kama kafungwa kaseti looh, la chumbani mpaka nje watasikia, mbele ya wageni, watoto, wasaidizi ye ni kufoka tuu.  Sijui ndio ajulikane Mkuu wa kaya mi hata sijui kwa kweli kujifanya Mungu mtu ndani ukiingia watu wote amani hawana mapigo ya moyo yanawaenda mbio kama wamekutana na mtoa roho.
Haaa we mwanaume mwenye tabia hii utangoja sana kupendwa.

UBINAFSI
Jamani mapenzi ni kueleweshana nishike hapa ukifanya hivi mwenzio naliwazika, wanaume wengi hawapendi kueleweshwa utamwona anajiliwaza yeye tuu akimaliza hana habari kama na mwanamke ni binaadamu hupenda aliwazwe na kufika kileleni kama mwanaume.  Ole wako umwambie  hakawii kukuita malaya sijui haya mapenzi waliumbiwa wao tuu.  Hali hii humsababishia mwanamke akose furaha na atafute mtu wa kumliwaza.  Kisha we unategemea upendwe na mwanamke huyu itakuwa ngumu.

UBISHI 
yaani mfano mkeo  kakuandalia nguo za kuvaa, viatu soksi, tai kaweka tayari, asubuhi we unavikataa na kumuamsha akutayarishie vingine.  Hata mbele za watu anaweza kuongea neno we ukampinga tena kwa dharau mpaka akaona aibu, ndio utakuta wanawake wengine wanakuwa wakimya akiwa na mumewe mbele za watu sio anakosa cha kuongea anaogopa kushushuliwa.  Mara nyingi haukubali ushauri wake hata kama una manufaa kwenu kisa ni mwanamke,  mmh kupendwa hapa ngumu.

Mmh hili somo ni pana sana lakini huwa ndio kitovu cha amani ndani ya nyumba au chanzo cha migogoro vile vile.
Nikushukuru wewe ulietumia muda wako kuperuzi hapa nadhani kuna moja au mbili umepata bila shaka na kama una nyongeza tafadhali niandikie kwenye USHAURI/MAONI au nipigie kwa namba hizi 
0712 244 221
kwa leo tuishie hapa wapendwa niwatakie Jumatatu njema.















No comments: